Nimrod Mkono uso kwa uso na TAKUKURU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimrod Mkono uso kwa uso na TAKUKURU

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Jul 2, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Viongozi UWT matatani kuzipokea (kadi feki)
  [​IMG] Simanjiro kadi feki zawatokea puani


  [​IMG]
  Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono


  Hali ya kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni tete kutokana na kubainika kuwepo kwa mchezo mchafu wa kusambaza kadi feki, wakati Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ikiwahoji makada kadhaa kwa tuhuma za kupokea simu kwa njia ya rushwa.

  Simu hizo ambazo Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono, amethibitisha kumwaga kwenye jimbo lake kwa kile alichosema ni kutekeleza ahadi zake kwa wapigakura, zimewatia matatani viongozi wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) wa Wilaya ya Musoma Vijijini mkoani Mara, wanahojiwa na Takukuru.

  Mkono mwenyewe amethibitisha kutoa simu hizo huku akisema si 80 kama inavyodaiwa ila ni zaidi ya 800 akidai ni kutekeleza ahadi yake aliyoitoa kwa wapiga kura wake na kwamba zitasaidia zoezi la kukichangia chama chake, linaloendeshwa kwa njia ya simu.

  Kwa mujibu wa Kamanda wa Takukuru mkoani Mara, Elias Nyororo, tayari viongozi wanne wamekwisha kuhojiwa, wawili kati yao wamekiri kupokea simu hizo na kusema walipewa na mbunge huyo huku wenzao wakikataa.

  Kamanda huyo alisema waliohojiwa ni viongozi wa ngazi ya kata na wilaya kutoka Wilaya ya Musoma Vijijini na kwamba zoezi la kuwahoji wengine zaidi linaendelea hadi ukweli wa sakata hilo upatikane.

  “Ni kweli taarifa zipo mezani kwangu na tumeshahoji viongozi wanne, taarifa tulizonazo ni kwamba simu hizo zimetolewa na mheshimiwa Mkono, nasi tunawahoji kutokana na tuhuma zilizopo,” alisema Nyororo.

  Alisema waliohojiwa ni wawakilishi wa UWT toka kata na wilaya ya Musoma Vijijini na kwamba Takukuru itakapojiridhisha kutokana na uchunguzi wake kwamba simu hizo ‘si bure’, ndipo hatua za kisheria zitachukuliwa.

  “Hatuwezi kuwanyang'anya simu hizo kwa sasa na wala hatuwezi kuamua hatua za kuchukua hadi kwanza tuwahoji watuhumiwa wote akiwemo mheshimiwa mbunge ili tupate ukweli wake,” alisema.
  Nyororo hakutaja majina ya watuhumiwa ambao wameshahojiwa ingawa Nipashe imepata mmoja wao aliyekiri kuwekwa kitimoto.

  Ingawa hakuweka wazi zaidi, kuna taarifa kuwa kiongozi huyo aliyekuwa Katibu wa UWT tayari amehamishia Wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

  Inadaiwa kwamba ‘kosa’ alilofanya Katibu hiyo ni hatua yake ya kukiri kwamba simu hizo ni za Mkono alipohojiwa Takukuru.

  Inasemekana kwamba simu nyingi zilimwagwa kwa wajumbe walioshiriki hivi karibuni kwenye kikao cha Baraza la UWT la Wilaya ya Musoma Vijijini kilichofanyika katika ofisi za CCM za wilaya hiyo.

  Walifafanua kuwa wilaya hiyo ina kata 27 ambapo kila kata iliwakilishwa na mwenyekiti, katibu na mjumbe, ambapo kila mmoja alipata simu.

  Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Mkono alisema simu alizotoa ni ahadi yake ya muda mrefu kwa wapiga kura wake na kwamba angewanunulia simu ili ziwasaidie katika mawasiliano.

  Alisema kuwa amemwaga simu hizo (zaidi 800), hususan kwa wajumbe wa nyumba kumi kwa kufuata utaratibu uliowekwa na viongozi wa CCM kwa kuzikabidhi kwenye chama.

  “Hiyo ni ofa kwa wapiga kura wangu na sasa zinaweza kusaidia pia katika kutuma ujumbe wa kuchangia chama chao. Hata wakitoa ki-thumni kinafika sehemu husika,” alisema Mkono.

  Alisema kuwa ni haki yake kukichangia chama na kwamba alichofanya ni mchango wake kwa CCM na wala sio rushwa kama ambavyo baadhi ya watu wanadai.

  “Huo ndio utaratibu tulioambiwa sisi wabunge na viongozi wa CCM kwamba vitu vinatolewa kwa utaratibu unaoeleweka kwa kukabidhi ndani ya chama na kisha chenyewe ndicho kinagawa. Hivyo ndivyo nilifanya na si kumpa mtu mmoja mmoja,” alifafanua.

  Katika sakata la kadi feki, makada kadhaa wa CCM wilayani Simanjiro wako matatani baada kubainika kusambazwa katika wilaya hiyo.

  Habari kutoka wilayani Simanjiro zinasema kuwa idadi kubwa ya kadi feki zimesambazwa katika kata kadhaa na kwamba lengo lake ni kuwanufaisha baadhi ya watu wanaotaka kugombea nafasi za ubunge na udiwani.

  Baada ya kubainika kuwa kuna kadi feki zilizosambazwa, kikao cha Halmashauri Kuu ya wilaya ya Simanjiro kiliketi Juni 28, ambapo pamoja na kujadili hali ya kisiasa, pia kilijadili suala la kumwagwa kwa kadi feki za CCM.

  Viongozi wa CCM wa wilaya hiyo, wameithibitishia Nipashe kufanyika kwa kikao hicho kujadili suala la kadi feki na hatua zilizochukuliwa.

  Katibu wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Jamilah Mujungu, alisema kuwa zaidi ya kadi 1,000 zisizo halali zilibainika kuingizwa katika kata sita kati ya kata 15 za wilaya hiyo.

  Mujungu alisema baada ya kuzigundua walianza kuchukua hatua kuhakikisha zinasimamishwa na kuzikamata zilizokuwa zimeshasambazwa.

  Alisema kuwa hatua nyingine ni kuwasimamisha watendaji waliobainika kuhusika katika njama hizo kwa kuzipokea na kuzisajili katika daftari la orodha ya majina ya wanachama ambao mwaka huu ndio watakaowapigia wagombea udiwani na ubunge kura za maoni.

  Aliwataja watendaji waliosimamishwa kuwa ni Katibu wa Kata ya Kitwai, James Lesile, Katibu wa Kata ya Rufulemiti, Daniel Mbalakai na Katibu Mwenezi wa Kata ya Terrat, Isaac Abraham.

  Aidha, alisema kuwa chama kimemvua uongozi Katibu wa Tawi la Terrat, Simvu Elija, na kwamba wote wamechukuliwa hatua hiyo kwa tuhuma mbalimbali ya ukiukaji wa maadili katika mchakato wa kuelekea katika uchaguzi mkuu.

  Mujungu alidai kuwa Lesile alipokea kadi feki na kuzisaini pamoja na kuzipiga muhuri halali wa chama hivyo kuingilia jukumu la katibu wa tawi.

  Alisema tuhuma zinazomkabili ni kupokea kadi feki na kuzihalalisha, kutekeleza majukumu yasiyo yake na kuhujumu daftari la orodha ya wanachama.

  Kwa upande wa Mbalakai, Mujungu alidai aligonga muhuri kadi ambazo si halali, eneo lake kuwa na kadi nyingi feki pamoja na kuzigonga mhuri wa kata kinyume cha utaratibu.

  Kuhusu Abraham, alidai amekosa maadili kwa kuchonga muhuri wa katibu mwenezi ambao aliufanyia kazi katika vikao vya maamuzi ambayo yameathiri shughuli za chama.

  Kuhusu Elija, Mujungu alidai kuwa amefutwa kazi baada ya kubainika kubadilisha majina yaliyokuwa yamepitishwa na vikao vya CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka jana na kwamba baada ya uchaguzi huo, aliwatumia viongozi aliowaingiza kufanya maamuzi kadhaa ya kukipaka chama matope.

  Alisema maamuzi ya kuwasimamisha watendaji watatu yalipendekezwa na Kamati ya Siasa na kuridhiwa na Halmashauri ya Wilaya na kwamba uamuzi wa kumvua uongozi Elija ulifanywa na Halmashauri ya Wilaya.

  “Pia Halmashauri ya Wilaya imeagiza hatua kali ziendelee kuchukuliwa dhidi ya kiongozi, mtendaji na mwanachama atakayekiuka maadili ya chama,” alisema.

  Katika hatua nyingine, CCM Kata ya Kivukoni mkoani Dar es Salaam, kimelalamikiwa kwa kuandikisha wanachama wapya kwa hila lengo likiwa ni kukipatia ushindi mnono katika chaguzi mbalimbali zijazo ukiwemo wa madiwani ambao baadaye watamchagua Meya wa Jiji.

  Hali hiyo imesababisha baadhi ya wananchi wakiwemo wanachama wa chama hicho kuweka pingamizi kwa baadhi ya wananchi waliojiandikisha wakidai kuwa si wakazi wa eneo hilo hivyo wamekosa sifa za kujiandikisha eneo hilo.

  Chama hicho kinashutumiwa kuandikisha wanachama kutoka vyuo vya Usimamizi wa Fedha (IFM), Mwalimu Nyerere na Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni jijini Dar es Salaam.

  Wanaotaka kuweka pingamizi walidai kuwa baadhi ya wananchi waliojiandikisha kwenye kata hiyo si wakazi wake hivyo wanataka kujua uhalali wa wao kujiandikisha kwenye eneo hilo.

  Katika moja ya nyaraka za CCM ambayo Nipashe inayo, inaonyesha kuwa wanachama wengi wameandikishwa uanachama siku moja jambo ambalo linatia shaka kuhusu uhalali huo wa uanachama.

  Waraka huo unaonyesha zaidi ya wanachama 300 wa CCM wa Kata hiyo walijiandikisha kuomba uanachama siku moja ya tarehe 01/01/2010, wengine zaidi ya 50 walijiandikisha tarehe 25/1/2010.

  Barua iliyoandikwa na kada mmoja wa CCM Tawi la Kivukoni kwenda kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Yusuf Makamba, inasema anahujumiwa na baadhi ya watendaji.

  Alidai kuwa anashangazwa kuhusishwa na kufutwa kwa majina ya wanachama halisi kwenye kadi zao na kuandikwa majina ya watu wengine kwenye kadi hizo kitu ambacho alisema hakimhusu.

  Alisema matatizo hayo yameleta mgawanyiko mkubwa miongoni mwa wanachama na viongozi wa ngazi za matawi, kata, wilaya na mkoa kwa ujumla kwani imefikia mahali wanaletwa watu kutoka maeneo mengine kama Gongo la Mboto na kujiandikisha katika daftari la kudumu la waopiga kura.

  “Tujiulize watu hawa wametoka huko walikotoka wakaacha kujiandikisha huko na kuja kujiandikisha katika Kata ya Kivukoni ni kwa ajili ya maslahi ya nani? Kwani hali hii ndiyo imeleta mgogoro katika matawi yetu kwa kuletewa wanachama mamluki tuwaingize kwenye matawi yetu,” alisema.

  Alisema hali hiyo inaweza kuvuruga zoezi zima la kura za maoni kuelekea katika kuwapata wagombea wa CCM hasa katika kata nyeti kama Kivukoni ambayo Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete anaishi.

  Ofisa Mtendaji Kata ya Kivukoni, Harold Uisso, alisema ni kweli kuna watu walikwenda kuweka pingamizi kwa baadhi ya wananchi waliojiandikisha, lakini walikosa sifa za kuweka pingamizi hilo.

  Alisema aliwaelekeza watu hao kuleta vitambulisho vyao vya kupigia kura na waeleze sababu za kuweka pingamizi hilo, lakini hawakufanya hivyo hadi kufikia jana.

  “Kuna masharti matano ya kutimiza mtu anayetaka kuweka pingamizi moja ikiwa ni kuwa na kitambulisho cha kupigia kura na aelezea alijiandikisha wapi na lini, amtaje mtu anayemwekea pingamizi kisha atoe sababu za kuweka pingamizi wale waliokuja hawakuwa na sifa hizo wakaenda hawajarudi,” alisema Uisso.

  Aidha, alisema watu wakishaweka pingamizi ofisi yake inakagua kuangalia ukweli wa pingamizi lililowekwa na baada ya hapo ndipo hatua zaidi zinachukuliwa.

  Alithibitisha kusikia maneno ya watu kujiandikisha katika kata hiyo wakati si wakazi wa eneo hilo, lakini alisema hajui ukweli wa malalamiko ya wananchi hao hadi uchunguzi utakapofanyika.

  Kwa upande wake, Katibu wa UVCCM wa kata hiyo, Bakari Itariel, alisema hawana takwimu sahihi za wanachama wa CCM kwa kata hiyo kwa kuwa uhakiki bado unaendelea.

  Alisema takwimu sahihi zitapatikana baada ya kazi ya kuhakiki wanachama litakalomalizika Julai 15, mwaka huu kwa kuwa kuna wanachama wengi wamehama na wengine wapya wamejiunga na chama hicho.


  Imeandikwa na Joseph Mwendapole na Sabato Kasika

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Naaam
  goma limepata mchezaji
  bado hayajafikia mahala pake haya masuala haya
   
 3. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyu anatakiwa awe KEKO !Mabillioni feki toka BoT bado yananuka.
   
 4. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  huyu ni fisadi tangu enzi za miaka ya 60...
   
 5. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  CCM / Takukuru hawana ubavu wa kumfanya chochote - the guy has power!
   
 6. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  I support you CCM hawaweai kumfanya chochote
   
 7. bona

  bona JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  huyu jamaa hamna mtu wa kumfanya kitu nchi ii, iyo chamber yake ya law duniani ipo kwenye chati, hata iyo kesi, ataimaliza kiulaini kwani sidhan serikali kama ina wakili wa kumpelekesha uyu jamaa mahakamani!
   
 8. M

  MJM JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  haya yote yana mwisho. .................chonya of chilonwa me.
   
 9. M

  MJM JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Lakini hawa CCM wana nini na sisi Wadanganyika? Hivi hatuwezi kujiunga pamoja tukaomba na kufunga ili Wadanganyika wabadili fikra zao kuhusu watu hawa. Tatizo nani amfunge paka kengele. kwa sasa naona waelewa wengi hawataki kusikia "....MIJITU HII....."- J.K. Nyerere aliita watu waaina hii hivyo.

  Hata kama kura yangu haitoshi nasema No kwa CCM. Hata kama influence yangu ni ndogo nitaitumia kusema No. kwa CCM. Tanzania bila CCM ina maendeleo makubwa kuliko sasa ambapo naona illusions.
   
 10. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Pole sana TAKUKURU - TA(CHICKEN)RU:

  Hamna uwezo wa "kulegeza kamba za viatu vya NM" abadan
   
 11. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kwanini asimwage mapesa hayo kwa wale vijana wa vyuo vikuu waliondanganywa na chama chake..
  Hakuna atakayerudisha nyumbani kwa kukosa ada..?
  Ukamwage simu huko vijijini sijui hata umeme wa kuchaji sijui wanao..let alone hela za vocha...
   
 12. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Well said, for CCM money is power you can buy all rulers.
   
 13. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
   
 14. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sasa hakuona muda mwingine wa kutimiza ahadi mpk muda huu karibu na uchaguzi??? that is Rushwa atraight away.....I wish tungeapata kiongozi dikteta mpanda maslahi ya watu wengi.....kama ni kisheria itakua ngumu sana kumtia hatiani huyu ******'nyaji.....as said b4, yote yana mwisho.....leo wanakubali simu but ipo siku watakaa na watamkataa na watampiga.....sijajua ni lini hii siku....but naamini kuwa ipo na haiko mbali
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,521
  Likes Received: 81,905
  Trophy Points: 280
  Hata mimi ndiyo nashangaa. Kachota mabilioni chungu nzima pale BoT, lakini TAKUKURU hawakumgusa kabisa sasa kamwaga simu chache tu wanajifanya wanatenda kazi zao. Ni usanii tu kuelekea October 31, 2010 hawana jipya TAKUKURU.
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyu mjamaa ni black version ya yule wa kidosi!
   
 17. T

  Tajiri Mtoto Senior Member

  #17
  Jul 3, 2010
  Joined: Feb 12, 2009
  Messages: 131
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  I believe there is a thin line btn "rushwa" na "genuine michango". Ni mazingira gani yanayomtofautisha aliyetowa simu kama zawadi na the same simu iliyotolewa kama rushwa; je ni swala la timing? Kwamba ikitolewa kabla ya uchaguzi ni rushwa na ikitolewa baada ya uchaguzi ni zawadi??? Sheria zetu zimekaaje??
   
 18. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Who is TAKUKURU Money talks 'I have got power' says Mkono
   
 19. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2010
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kama hiyo ya prof. Mkono sio rushwa, basi wengine hatuelewi maana halisi ya neno rushwa.

  CCM wawe tayari kuwatosa wote wanaotoa rushwa mbalimbali bila ya kujali umaarufu wao, vinginevyo sheria ya gharama za uchaguzi itakuwa haina maana yoyote. Hapa mwanzoni inabidi chama na serikali wawe wakali kweli kweli ili kuipa meno hiyo sheria. Wananchi wengi bado wanaona ni utani tu na hata wakiambiwa hairuhisiwi kupewa posho, wengi wanachukia. Lakini wakiona baadhi ya watu maarufu wamenyimwa nafasi ya kugombea ubunge shauri ya kutoa posho au zawadi, hata wananchi wenyewe wataanza kuogopa.

  Inasemekana mpaka sasa CCM imepeleka majina zaidi ya 60 ya wagombea ubunge huko TAKUKURU kwa uchunguzi. Inasemekana kuna baadhi ya wabunge wa sasa na wagombea wapya wenye majina makubwa kwenye jamii. Wacha tuone nini kitatokea na ndio wananchi watajua kama kweli chama kiko serious kwenye hii issue.
   
 20. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  "Money Power Respect"-The L.O.X 1998
   
Loading...