Nimrod Mkono, bado huna mpango wa kuachia Ubunge?

Nimrod Mkono, bado huna mpango wa kuachia Ubunge?

mhilisila

Member
Joined
Jun 3, 2014
Posts
25
Reaction score
3
Huu ni mwaka Wa uchaguzi,mbwembwe na tambo
Kwa wanasiasa walioko madarakani haziishi kama alivyowahi kusema nimrod mkono mbunge Wa musoma vijijini kwamba hana mpango Wa kuachia madaraka hajaona MTU Wa kumwachia na atakuwa king'ang'anizi kama Mugabe, Je mheshimiwa kwa barabara hizi una sifa za kuendelea kuwepo?
 
Attachments

  • 1430581177327.jpg
    1430581177327.jpg
    41.4 KB · Views: 478
Hata mpigi magoe kumara kilungure barabara ziko hovyo je hiyo ni sababu tosha ya kumwambia mnyika aachie jimbo la ubungo!!!?
 
dah! hamna jema nyie! mbona aliyowafanyia ni mengi! ambayo ni dalili kuwa hata yaliyobaki akipewa muda atafanya! Bila shaka tayari kuna mtu anataka jimbo...sasa kawakusanya msiojitambua kawapa vijihela vya viroba..mnaanza kuwayawaya! HOPELESS! halafu mkifanikiwa kumtoa, akaja mnayemtaka, then akawa mzigo mtaanza kuchonga tena! Hebu nikuulize swali....ni kwa sababu gani unataka Mkono atoke?
 
Wazee hata mkimtetea babu haponi mwaka huu na sidhani kama mnalifahamu vizuri jimbo LA musoma vijijini.
Sikatai kafanya mambo mengi katika awamu ya kwanza na ya pili lakini hii ya tatu utadhani jimbo halikuwa na mbunge. Mnaotetea kwamba aendelee naomba mrejee matokea ya uchaguzi Wa serikali za mitaa, mfano nendani kata ya Buswahili mtapata
Majibu yeye na chama chake wana hali gani.
 
Mwenye namba ya huyu ndugu anitumie
I mean his mobile phone number. Kwa pm please.
 
Hata mpigi magoe kumara kilungure barabara ziko hovyo je hiyo ni sababu tosha ya kumwambia mnyika aachie jimbo la ubungo!!!?

Hongera kwa kuwa mmoja wa wanaotumia akili yako ipasavyo
 
dah! hamna jema nyie! mbona aliyowafanyia ni mengi! ambayo ni dalili kuwa hata yaliyobaki akipewa muda atafanya! Bila shaka tayari kuna mtu anataka jimbo...sasa kawakusanya msiojitambua kawapa vijihela vya viroba..mnaanza kuwayawaya! HOPELESS! halafu mkifanikiwa kumtoa, akaja mnayemtaka, then akawa mzigo mtaanza kuchonga tena! Hebu nikuulize swali....ni kwa sababu gani unataka Mkono atoke?

Tumemchoka tu,kwani yeye amekatia leseni ya kuliongoza hilo jimbo maisha yake yote?
 
Wazee hata mkimtetea babu haponi mwaka huu na sidhani kama mnalifahamu vizuri jimbo LA musoma vijijini.
Sikatai kafanya mambo mengi katika awamu ya kwanza na ya pili lakini hii ya tatu utadhani jimbo halikuwa na mbunge. Mnaotetea kwamba aendelee naomba mrejee matokea ya uchaguzi Wa serikali za mitaa, mfano nendani kata ya Buswahili mtapata
Majibu yeye na chama chake wana hali gani.

Mkuu tupatie angalau ka picha ili tuende sawa
 
Kazi ya Mbunge ni Kujenga barabara? Nimrod Mkono anakusanya kodi toka lini? Mkiambiwa muende shule mkajielimishe Zaidi mnaishia kunywa viroba tu .... Vijana wa FISADI Muhongo mnakera kweli kweli ...
 
Tumemchoka tu,kwani yeye amekatia leseni ya kuliongoza hilo jimbo maisha yake yote?

oh, kama ni hivyo poa! i thought issue ni kuwa hawajibiki jimboni, ndo maana nikashangaa! maana kazi anapiga fresh
 
Mkono ana umri nafikili ni over 55 yrs,amesha invest vya kutosha na bado anataka kuendelea kung'ang'ania hilo jimbo,nimuda muafaka awaachie vijana wapo wengi ambao hawana kazi ya kujipatia hata mkate wa kila siku bila kujali kama huyo atakaye chukua hilo jimbo anatoka chama gani,iwe ccm au upinzani.
 
Kama mmemchoka msimpigie kura. Lakini kuna watu watampigia kura na akishinda ndo hivyo tena. Ataendelea kuwa mbunge. Suala la kwamba aachie ngazi halipo kama yeye anataka kuendelea. Kama nilivyosema hapo awali mwenye ubavu wa kupambana naye ajitokeze tu akapambane naye. Akishinda basi atakuwa mbunge wa jimbo la Butiama.
 
Back
Top Bottom