NIMR yagundua dawa ya UKIMWI, Tezi dume

NIMR yagundua dawa ya UKIMWI, Tezi dume

Kama dawa yenyewe haijawa tayari kuna uharaka gani kipindihiki?.Hayo si ndio mambo ya Samunge tena?
 
Watu wanataka kila siku habari za ACT na CHADEMA mambo mengine hawataki kweli hii ni sheeeedaaa
 
Kila kukiwa na mambo yabayogusa taifa hawakosi kuja na mbinu kuwaondoa watu kwenye mjadala,sasahivi tupo kwenye swala la daftari lawapiga kula na uchaguzi mkuu,au ni kick kwa kuwa hiyo kazi imeshindikana tusahau?
Kuhusu dawa ya tezi dume imeonyesha uwezo mkubwa na naamini watatupa takwimu.
 
HONGERA nyingi NIMR,Mwele na team yako yote.

Ila msisahau HAKI MILIKI la sivyo zitarudia kwa majina mengine.
 
Kumbe ukimwi unatibika?
Ndiyo maana wakati mwinyingine wana sayansi wanaogopa waandishi wa habari!!
Nina imani kubwa kuwa maelezo waliyopewa sio kusema inatibu ila waandishi wa habari wameweka hivyo ili wauze gazeti.
Ili ueleze ya kuwa dawa inatibu kuna taratibu zinatakiwa zifanyike na kama ingekuwa ni kweli ingekuwa ni WORLD BREAKING NEWS!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Wametengeneza dawa ya ukimwi (AIDS) ambapo kabisa kuna uwezekano wa mtu kuweza kuishi akifika stage hizo.

Au wametengenza dawa ya kuweza kudhibiti virusi vya ukimwi kutopelekea kupata gonjwa la ukwimi.

Dawa ina tibu nini hasa na inafanya kazi vipi mbona maelezo ya habari yanaancha maswali kuliko majibu ina uwezo wa ku-repair CD4 cells inazuia nguvu za HIV kuweza badilika na kuvidhibit surely kuna medical reporters kwenye haya magezeti maana huu ni uandishi kanjanja kupindukia.
 
Inatibu UKIMWI huuhuu unaoua ndugu zetu au kuna UKIMWI mwingine
 
hivi huyu dada yake na le mutuz kweli??

mbona yeye akili nyingi while le mutuz akili ndogo
 
NIMRI imeshirkishwa kimataifa kufanya utafiti dawa ya ukimwi. Si yake. Acheni siasa

Hii ilikuwa habari ya kuuza magazeti ya leo na pengine wamepata mgao kutokana na mauzo ya leo. Huo uwezo wa ugunduzi wa juu hivyo bado hawajawa nao na wala hauwezi kuaminika na kukubalika hata hapa nchini tu mbali ya mataifa makubwa yenye maabara makubwa na wataalam waliobobea katika chunguzi. Madawa ya mimea ya kuua wadudu yanachakachuliwa kila leo na wakulima wanakosa mavuno na Nimr wapo leo waje na ugunduzi wa dawa ya ukimwi? Mafrof. vyuo vikuu vinavyoheshimika dunia nzima vipara hadi vimeota vipele hawajagundua dawa wakati kila kitu wanacho hadi misaada ya nchi tajiri leo hii Nimr iseme wanasubiri kuiingiza dawa sokoni. Hizi ni njozi kama za babu wa Loliondo.
 
Super geneus kowero. Sound intel
 
Back
Top Bottom