Nimfuate au nikomae tu?

Nimfuate au nikomae tu?

Iko hivi, juzi alikuja mpnz wangu kuja kuishi, (tuna mtoto) baada ya kukaa kijijini kwa kipindi fulani nikaomba kwa wazazi wake aje tusaidiane baadhi ya mambo, (nataka kumsapoti kwa issues za kibiashara walau aweze kujipatia kipato, maana hatuijui kesho)

Sasa ameingia jijini kama siku 4 zilizopita, Jana majira ya saa tatu usiku nikapigiwa simu mke wa jamaa yangu kwamba jamaa ana hali mbaya mno, tunaweza kumpoteza kwa jinsi alivyo!

Nikamwambia mgeni wangu hiyo situation na kumuomba anisubiri nitarudi, akagoma "Hamna kwenda" nikajaribu kumuelewesha akagoma, kwa hisia kwamba aliyenipigia simu ni mwanamke hivyo hiyo habari ya rafiki yangu ni uzushi, nikaona isiwe tabu, nikaondoka!

Nimefika kwa jamaa nakuta hajitambui na anatoka povu mdomoni, (sijui alikula kitu gani) maana baada ya kufika hospital ikaonyesha amekula sumu, sijui aina gani huko, wamehangaika naye bahati nzuri akanusurika!

Mpaka majira ya saa kumi asubuhi ndo nimeingia home, nikakuta bibie amelala! Nikajipumzisha kidogo then nikaamka kwenda job.

Nikiwa job bibie akanitumia msg, ukirudi haunikuti, haiwezekani unaniacha ndani unakwenda kulala na mwanamke aliyekupigia simu!

Sikujibu, nimerudi home nakuta mabegi yake hayapo, na yeye anamalizia kumuandaa mtoto aondoke, nimejaribu kuongea naye lakini hajanielewa kabisa akaondoka zake!

Mida hii nimemuandikia kuwa alikuja jijini kwa ajili yangu,wazazi wake wanajua yupo na mimi hivyo namtaka nyumbani haraka, akanijibu kama namtaka nyumbani basi niende nikamfuate! Nikumuuliza yupo wapi ananiambia nimtafute mpaka nimpate...khaaaaaaa!

Nimeshikwa na hasira kweli kweli, nimfuate au nimpotezee tu, kinachoniuma ni kwamba yupo na mtoto mdogo, hivi wanawake wengine mkoje??? Huyu ananisumbua asubuhi hivi, ntawaza habari ya kumuoa kweli? Na hata nikifosi ndoa na mtu wa hivi, hiyo ndoa itadumu kweli???
View attachment 2361829
Mwandike sms " Kwa kuwa hukutaka kunisikiliza ili ujue ukweli,sioni haja ya kukutafuta,maisha mema"

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Kazi kweli kweli maamuzi ya mwisho unayo wewe mwenyewe sikilizia moyo wako.
 
kwakweli kuna watu hawajielewi,sasa mtu wa hivyo utawezaje kumuoa ikiwa yuko hivyo bila ndoa?
 
Iko hivi, juzi alikuja mpnz wangu kuja kuishi, (tuna mtoto) baada ya kukaa kijijini kwa kipindi fulani nikaomba kwa wazazi wake aje tusaidiane baadhi ya mambo, (nataka kumsapoti kwa issues za kibiashara walau aweze kujipatia kipato, maana hatuijui kesho)

Sasa ameingia jijini kama siku 4 zilizopita, Jana majira ya saa tatu usiku nikapigiwa simu mke wa jamaa yangu kwamba jamaa ana hali mbaya mno, tunaweza kumpoteza kwa jinsi alivyo!

Nikamwambia mgeni wangu hiyo situation na kumuomba anisubiri nitarudi, akagoma "Hamna kwenda" nikajaribu kumuelewesha akagoma, kwa hisia kwamba aliyenipigia simu ni mwanamke hivyo hiyo habari ya rafiki yangu ni uzushi, nikaona isiwe tabu, nikaondoka!

Nimefika kwa jamaa nakuta hajitambui na anatoka povu mdomoni, (sijui alikula kitu gani) maana baada ya kufika hospital ikaonyesha amekula sumu, sijui aina gani huko, wamehangaika naye bahati nzuri akanusurika!

Mpaka majira ya saa kumi asubuhi ndo nimeingia home, nikakuta bibie amelala! Nikajipumzisha kidogo then nikaamka kwenda job.

Nikiwa job bibie akanitumia msg, ukirudi haunikuti, haiwezekani unaniacha ndani unakwenda kulala na mwanamke aliyekupigia simu!

Sikujibu, nimerudi home nakuta mabegi yake hayapo, na yeye anamalizia kumuandaa mtoto aondoke, nimejaribu kuongea naye lakini hajanielewa kabisa akaondoka zake!

Mida hii nimemuandikia kuwa alikuja jijini kwa ajili yangu,wazazi wake wanajua yupo na mimi hivyo namtaka nyumbani haraka, akanijibu kama namtaka nyumbani basi niende nikamfuate! Nikumuuliza yupo wapi ananiambia nimtafute mpaka nimpate...khaaaaaaa!

Nimeshikwa na hasira kweli kweli, nimfuate au nimpotezee tu, kinachoniuma ni kwamba yupo na mtoto mdogo, hivi wanawake wengine mkoje??? Huyu ananisumbua asubuhi hivi, ntawaza habari ya kumuoa kweli? Na hata nikifosi ndoa na mtu wa hivi, hiyo ndoa itadumu kweli???
View attachment 2361829
Baada ya kuona hakuamini ungemwambia muende wote akajionee kisha angerudi nyumbani baadae. Inaweza kuwa ni kutojiamini sababu hamjakaa pamoja muda mrefu anaamini ulishakuwa na demu mjini. Mtafute ni mama wa mwanao..
 
Hiyo demokrasia kwangu haipo, yaani usiku nianze kusumbua mtoto wangu kwa sababu ya wivu tu?

Hapanaaa
 
Baada ya kuona sijamfuata wala sijatetereka anakuja kihivi...nataka kumwambia ili nimpokee aje na huyo alikwenda kuishi kwake siku zote hizi...

Sitaki ujinga kabisa, bronken instanbul...

Screenshot_20220923-151244~2.jpg
 
"Hivi wanawske wengine mkoje"
Mkuu hii sentensi inabidi utuombe radhi, maana hata sisi wenye jinsia "ME" unetuweka kwenye jinsia "KE". Mimi sikubaliani nayo labda wenzangu., hapo kwenye " MKOJE" ungeweka "WAKOJE"

Ushauri, hiyo pisi yako kali piga chini, unasema amekaa kijijini muda mrefu so alikuwa anatafuta namna ya kuingia mjini tayari umeshamrahisia ndio maana anakwambie umtafute. Wajulishe wazazi wake kolichotokea then fuata yako.
 
Pole sana, mambo yake muachie mwenyewe, akimalizana nayo atarudi...
 
Back
Top Bottom