Nimfanyeje huyu ndugu yangu?

Nimfanyeje huyu ndugu yangu?

Huntsman

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2012
Posts
648
Reaction score
621
Habarini za uzima wakuu.

Natumaini mko salama, naombeni ushauri wenu makini hapa. Nina ndugu zangu wawili ambao mmoja ni kaka yangu kabisa tena mtoto wa baba yangu mdogo. Huyu kaka ni mwajiriwa wa JWTZ.Nina ndugu yangu mwingine kaka yangu ambaye ni family friend.

Sasa mwaka jana huyu kaka ambaye ni family friend alichukua mkopo benk kwa kuweka dhamana ya nyumba yake nilimuomba mimi kwakuwa nilikuwa nahitaji mkopo na mimi sikuwa nakidhi vigezo kukopesheka. Alipochukua mkopo akanipatia wote na mimi nikawa narudisha kila mwezi pasipo tatizo lolote.

Sasa mwaka jana huo huo huyu ndugu yangu aliumwa sana ikapelekea yeye kusafirishwa mkoa mwingine kwenda kutibiwa hata hivyo ilinilazimu kuendelea kulipa kila mwezi rejesho la benki.Ikatoke katikati ya mwaka jana nikayumba kiuchumi ikabidi niuze moja wapo ya assets zangu ili kufidia deni la benki kwani nilipitisha mwezi bila kupeleka.

Sasa hapa ilibidi nimshirikishe huyu kaka mwajiriwa wa JWTZ ili auze ile asset na pesa aipeleke Benki kwakuwa mimi nilikuwa na safari mara kwa mara hivyo ni vigumu kutafuta wateja.

Sasa huyu kaka akapata mteja na kuuza ile asset ila pesa hakupeleka benki akatoa sababu na kuomba nimpe muda atapeleka.Kakuwa ni kaka yangu na ndugu yangu nikamkubalia na mimi nikawa nampa pesa kila mwezi arejeshe wakati bado nina deni kwake nadai.

Sababu ya kuwa nampa yeye arejeshe ni kuwa muhusika alikiwa mgojwa na alisafirishwa kulazwa mkoa mwingine na mimi kikazi ni mtu wa safari sana sasa ilikuw ni rahisi kumtumia huyu kaka kufanya deposits. Hadi hapo sikujua mchezo wowote mbaya.

Huyu ndugu mgonjwa alipona na kurud huku Dar ambapo alipochukua bank statement ikagundulika kuwa tangu aondoke pesa ilikuwa hailipwi benki kama kawaida. Na pia hivi karibuni kaka wa JWTZ kanunua plot na gari la kutembelea. Nilijulishwa na huyu kaka kuwa pesa inadaiwa na benki au nyu,ba iuzwe nikachanganyikiwa.

Nikamuuliza huyu kaka wa jeshi majibu ya dharau na kiburi na vitisho ndio ninchoambulia. Sasa hapa nipo njiapanda nawaza nikamshtaki jeshini kwakuwa nimejaribu kuita vikao vya ndugu mara mbili hahudhurii.
Nifanyeje pesa ya benki ipatikane wakuu?

Natanguliza shukrani kwenu.
 
Nenda kikosini kwake……

Mkuu huyu yuko makao makuu pale JKT mlalakuwa ila kikosi chake sikifahamu na na je huko nitapata msaada?? Nilishauriwa na baadhi ya ndugu ila sijui procedures za huko jeshini. Asante
 
Mkuu huyu yuko makao makuu pale JKT mlalakuwa ila kikosi chake sikifahamu na na je huko nitapata msaada?? Nilishauriwa na baadhi ya ndugu ila sijui procedures za huko jeshini. Asante

Anacheo gani huyo ndugu yako?
 
Huyo hata ukimfata kikosini kama kaamua kukutenda imekula kwako brother kwasababu nyinyi hamkuwa ma makubaliano yoyote kimaamdishi ni kama ww ulikuwa unampatia pesa tu akusaidie kwahio alikuwa na chaguo la kuwa muaminifu au kukurubuni!Yaani hata sijui umfanye nn ngoja nifikirie nitakuja na jibu lkn kitu kimoja nimejifunza katika maisha haya jitegemee ktk income yako usikope wala usikopeshwe hata na ndugu watu hawaaminiki kabisa yaani!
 
Kwakweli sijui cheo chake ila ni askari wa kawaida alikuwa kwenye kada ya uhasibu pale

Nenda kamshtaki, kwa mkubw wake hapo, akizngua nenda upanga na jeuri itamwisha aache kuonea raia huyo
 
Mkuu huyu yuko makao makuu pale JKT mlalakuwa ila kikosi chake sikifahamu na na je huko nitapata msaada?? Nilishauriwa na baadhi ya ndugu ila sijui procedures za huko jeshini. Asante

Nina jamaa ni mtu mkubwa pale mlalakuwa nilisoma naye uhasibu kama uko tayari tunaweza kumuuliza kuwa atakusaidia vipi. Ila kwa jinsi ninavyofahamu ukilifikisha uko unaweza kupata msaada wa haraka. Kuna jamaa mmoja aliwahi kumuuzia mjeda ploti akawa anazingua kummaliza pesa iliyobakia hata simu akawa hapokei mbona alipoenda kikosini kwao ndani ya siku mbili yule mtu alilipwa.
 
Pole sana, jeshin kuna kuheshimiana sana hasa kwa mtu aliyekuzid cheo kama yeye ni askar wa kawaida (private) hata kama ana cheo jaribu kwenda makaon kwake waeleze hali halisi wajue jinsi ya kukusaidia kibinadam maana hapo hakuna kes kama huna ushahid kama ni ishu ya kwenda kikosin kwake kuna mkuu wa nidham (RSM) akiwa ni mtu mwenye utu anaweza kukusaidia kwa kumuita na kumtaka akurudishie ama kupatikana mbadala mwingine pia ili kujua cheo chake ebhu tuambie ana elimu gan ama ana muda gan jeshin?
 
Unaweza kwenda kazini kwake lakini uwezekano wa kusaidiwa utategemea aina ya boss wake kwa sababu haya ni mambo ya kifamilia. Kwa sasa tatuta pesa za benk kwa njia yoyote ukalipe. Pia jipande kisakolojia kukabiliana na hili suala la kudhurumiwa na ndugu. Chance ya kupata hizo pesa ni ndogo sana!
 
Nenda kamshtaki, kwa mkubw wake hapo, akizngua nenda upanga na jeuri itamwisha aache kuonea raia huyo

Asante kaka nawaza hii option niifanye ikishindikana basi nitanyosha mikono lakini huyu hana hata uchungu wala hashtuki.

Funzo nimelipata na sitamuamini mtu yeyote kamwe
 
Nina jamaa ni mtu mkubwa pale mlalakuwa nilisoma naye uhasibu kama uko tayari tunaweza kumuuliza kuwa atakusaidia vipi. Ila kwa jinsi ninavyofahamu ukilifikisha uko unaweza kupata msaada wa haraka. Kuna jamaa mmoja aliwahi kumuuzia mjeda ploti akawa anazingua kummaliza pesa iliyobakia hata simu akawa hapokei mbona alipoenda kikosini kwao ndani ya siku mbili yule mtu alilipwa.

Asante mkuu nikirudi tu Dar nitaku PM unisaidie kuongea na huyo jamaa yako anisaidie maana nina uchungu sana kufanyiwa hivi.
 
Asante kaka nawaza hii option niifanye ikishindikana basi nitanyosha mikono lakini huyu hana hata uchungu wala hashtuki.

Funzo nimelipata na sitamuamini mtu yeyote kamwe

Wewe nenda kwa mkubwa wake, anaeza taka kutumia kujuana kukuzunguka, ukiona analindwa (kama jamaa waki corupt). Makao upanga ndo mwisho wake huyu, tena umwambie kuwa akizngua utamuharibia
 
Back
Top Bottom