Nimfanye nini huyu office-mate?

Nimfanye nini huyu office-mate?

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,374
Reaction score
38,248
Wana - JF nawasalimu sana!

Mwenzenu nina mtihani! Hapa ofini kwangu ni na bidada mmoja (ni mrembo wa haja tu, anatoka ule mkoa karibu na Dodoma na wadada wa mkoa huo wana ile sifa kama ya ule mkoa wa kanda ile isiotakiwa kutoa Mkulu). Ni mfanyakazi mwenzangu, tuliajiriwa mwezi mmoja, tumeishi kwa miaka mi3 kama kaka na dada, huku tukiheshimiana sana! Kama mnavyojua ofisi za serikali, huwa tunashirikiana sana katika mambo mengi sana ya kiofisi kuanzia kushare stories mpaka kupeana ushauri, asipokuwepo nafanya kazi zake, nisipokuwepo anafanya kazi zangu! Tunashirikiana ktk NIDO, majani ya chai, maji ya kunywa, vitafunio - hivi huwa tunapewa na ofisi, mpaka nauli!

Katika lunch pia hivo hivo, nina hela namuagizia lunch box, na yy akiwa nazo hivo hivo! Yaani tumekuwa dada na kaka wapenzi mpk ofisi zingine wanatuonea wivu! Wakati ofisi zingine wanashindana umbea na majungu, sisi kwetu ni kupendana na kujaliana! wakati mwingine majungu yakiwazidia wenzetu huwa wanakuja ofisini kwetu kupata relief!

Mimi nimeoa na yeye ameolewa! Mwenzangu ndoa yake ina mtihani, hawajabahatika kupata mtoto! Bahati mbaya ni kuwa, bi dada umri umeenda! Mimi amenizidi 2 years! Mimi kwa upande wangu mungu amenijaalia watoto wawili! Mwanzoni kabla sijamsoma, ilikuwa rahisi mimi kumueleza ama kupiga story kuhusu watoto, reference kwa wanangu! Kumbe mwenzangu moyoni alikuwa anaumia sana! ktk story zote tunazopiga, hizi za watoto hazipendi! zinamchoma! Baada ya kujua na mimi nimeacha kumuelezea lolote lile kuhusu watoto wangu! Hata kama naenda hospital kupeleka mtoto, basi yeye nitamuambia naenda k'koo ama posta, ili tu nisimuumize!

Sasa balaa ni hili hapa! Kaja na mpya!
Alianza kwa kuntumia video ya PILAU whatsapp! kwa kuwa ni mtu ambae uhusiano wetu haukuwai kufikia ktk kutumiana vitu km hivo, nikashtuka! nikahisi kakosea wa kumtumia! mimi sikumjibu bali nikai-delete fasta kabla mama nanii hajaiona! nikasubiri sms yake ama call ya apology! kimyaaaa! Baada ya siku kama 3, akanambia samahani ile video haikuwa yako, nilikosea kukutumia, nikamuambia sawa ila kuwa makini!

Hapo kabla alikuwa ni mpenzi wa sketi ndefu na blauz za kuficha matiti, siku hz ni mwendo wa vimini na blauz za manyonyo nje! Mbona nakoma mwenzenu!Siamini kama ananivalia mimi ama mwengine, lkn kazi ninayo! Na pia kesi za kuitwa nikamsaidie kitu ktk computer yake sk hz zimekuwa kibao, hasa za kumwelekeza program mbali mbali, tena wkt mwingine anakuja kwangu kuniinamia nimuelekeze, nakomaje! manyonyo yote, tiiii kwangu!

Likaja la kuonyeshwa chachandu! mimi sijui kama tangu zamani anavaa ama ameanza kuvaa siku hz, na kama anavaa siku hz, ananivalia mimi ama mr wake, mm sijui! ila kila siku naonyeshwa chachandu, lazima nionyeshwe chachandu, kama si asubuhi basi mchana! na anajua style nzuri za kunionyesha chachandu zake! tena anajua kuchagua, zinamkaa vzr kweli kiunoni! (bahati mbaya hajui kama mimi ni ugonjwa wng, hii bidhaa mimi huwa naumwa nikiiona! daah kila m'me na madhaifu yake jamani)

Yote kwa yote mimi si mfuasi wa michepuko! Na bado tunaheshiana sana, japo nimeshaanza juhudi za kupunguza mapenzi ya udada-ukaka ili huko mbele yasije yakawa mazito! Shida yangu wanaJF, naomba mnisaidie njia sahihi ya kumuomba kama ananitega, basi mimi hapana, siko huko! anionee huruma, coz mateso ninayopata, kila siku nakuwa wa kwanza kusepa ofisini na wa mwisho kuingia, na hii inanipunguzia ufanisi kazini! Nambieni nitumie njia gani ili nimrekebishe na turudi ktk undugu wetu kama zamani, nia yangu ujumbe umfikie japo naogopa mashushu ya bimdada! Msaada jamani!
 
Kemea hilo pepo kwasauti mbele yake. Nena mpaka kwa lugha na umshike kichwa chake kwa nguvu ukiwa unasali kwa nguvu zote.
Onyo: Kama ofisini kwenu kuna camera usijaribu. Utawavunja mbavu IT.
Pole kwa majaribu.
 
wana - jf nawasalimu sana!

huwa tunashirikiana sana katika mambo mengi sana ya kiofisi kuanzia kushare stories mpaka kupeana ushauri, asipokuwepo nafanya kazi zake, nisipokuwepo anafanya kazi zangu! Msaada jamani!

dont ever let someones wife to talk to you that much..because from a shoulder to cry on will soon be a d**k to ride on
 
Uwe mwanaumme; kama huna nia ya KUCHEPUKA mwambie ukweli kuwa Dada kidogo unanikwanza kwa nyendo zako.....Heri uwe mkweli (hata kama itamuuma) ili roho yako iwe na amani.
 
Mwambie kwamba hizo nguo fupi hazimpendezi na ukiona kakuonesha chachandu, mwambie pandisha skirt kiuno kinaonekana..... lazima ataacha ila mwambie kama masihara masihara hiv ila ujumbe utamfikia.
 
Kemea hilo pepo kwasauti mbele yake. Nena mpaka kwa lugha na umshike kichwa chake kwa nguvu ukiwa unasali kwa nguvu zote.
Onyo: Kama ofisini kwenu kuna camera usijaribu. Utawavunja mbavu IT.
Pole kwa majaribu.

Hamna camera, na mimi mwenywe ushanivunja mbavu Mkuu!
 
Mwambie aende kwa TB Joshua akaombewe. Stress hizo.....

huyo TB hana kaz nyingine za kufanya???kuna mambo mbona yapo ndani ya uwezo wetu wadau,tatizo nini???sasa mwanaume anashindwaje ku-handle hii ishu???,kama ni muislam mpe vipande vya aya za mwenyezimungu ili avae kwa kujistiri,kama mkristo mpe mistari yake ,kuliko kuja kulialia hapa,gharamaza kwenda kwa Joshua angemnunulia nepi mwanae
 
Kamshitaki kwa bosi wako..
Serikali imepiga marufuku kwa watumishi wake kuvaa nguo fupi....

Nadhan kama suala la nidham ya mavazi inafuatiliwa hapo ofisin kwenu...
Ataonywa.....



Pengine na ww unakodolea macho kodo kodo.......

Umeshatengwa....
 
Mwambie kwamba hizo nguo fupi hazimpendezi na ukiona kakuonesha chachandu, mwambie pandisha skirt kiuno kinaonekana..... lazima ataacha ila mwambie kama masihara masihara hiv ila ujumbe utamfikia.

Huwa anasifiwa akapendeza ghorofa zima, masekretari huwa wanamsifia sana! mimi ntaanzia wapi kumwambia hujapendeza! hili la masihara naliweza!
 
Kamshitaki kwa bosi wako..
Serikali imepiga marufuku kwa watumishi wake kuvaa nguo fupi....

Nadhan kama suala la nidham ya mavazi inafuatiliwa hapo ofisin kwenu...
Ataonywa.....



Pengine na ww unakodolea macho kodo kodo.......

Umeshatengwa....

Huwa nakodoa macho kwenye chachandu tu!
 
me nazani mpotezee tu, jifanye huoni wala hujali mwenyewe atakuja kujiona mjinga ataacha, ila ukimwambia unaweza kuharibu akakutafutia visa au akakugeuzia kibao ofisi ukaiona chungu
 
mimi huwa naamini kitu kimoja kwamba katika mahusiano mamuzi ya aina a uhusiano hayatilii maanani ushauri unaopewa! ww ndo unayeweza kuamua uhusiano wa aina gani ue nao na huyo mdada!
 
kwa kuwa yeye ndo amekuwa wa kwanza kubadilika na wewe badilika tu akiingia ofisini kwako nuna,uonekane huna furaha na kutomjali akikuuliza mweleze unavyojisikia vibaya juu ya uvaaji wake......ogopa sana mke wa mtu ni hatari sana.

 
Back
Top Bottom