Nimfanyaje huyu dada? Yamenikuta leo asbh

mkuu usikute kuna mahali umetuficha!..manake haiingii akilini afyonze wkt mtu ata akujui..mmh?
 
Haya sasa ni mazito jamani! Mwanamke hana haya huyo! Duh. Potezea mbali.
 
Kwani kukataa kupanda gari lako kakupunguzia nini zaidi ya usumbufu? Lakini kaka inaonyesha kuna utani fulani fulani ambao umeshawahi kuufanya mwenzako akajua ni serious.

Take care
 
mkuu ina maana baada ya salamu, hakukuwa na maongezi mengine ndani ya gari na huyo binti wa njiani ?
Its so strange afyonye bila ya sababu.

Mkuu huyo mdada ana matatizo tu kichwani.Kwa sababu hata kama huwa wanamaongezi mengine ya kimahusiano bado hakutakiwa kuji behave vile kwani hakujua yule aliyemkuta ndani ya gari ni nani na kwa nini yuko pale.
 
Achananae huyo,sisi tunawaita ngedere magari mademu wa dizaini hiyo,yaani yeye akimuona mtu ana gari tu,bila kujua ni dereva au la kwake anataka kumletea mahaba,tena sasa hivi hata kama hautumii AC,ukimuona kwa mbali mfungie vioo,alafu huwezi kujua unaweza kuta huwa anajibanza sehemu akikuona unatokeza tuu ndio nae anajitia barabarani!!!ngedere magari
 
Mbona mkuu HP hiyo kesi imeisha toka pale alipozira na kukataa kupanda gari!...au nini unataka zaidi ya hilo?kama lifti ulitoa kwa huruma yako,mpewaji sasa haitaji wewe unatafuta kitu gani kingine?....au mkuu kuna kitu zaidi ya lifti ambacho unaona utapoteza kutokana na hilo tukio?.....yeye kapotezea then wewe potezea zaidi yake....hakuna kesi hapo kiongozi.

Mkuu hapo umemaliza,kama akiendelea kutafuta majibu mengine atakuwa alitangaza nia.
 
Wanachangia mafuta au?bac kama ni bure kuna namna alikuwa anakulipa pesa zako za mafuta ndo mana alipomkuta dada mpya wa lift alimynd kinoma kwa7bu yeye analipaga kidizain.uongo man wang sema 2 ukwel 2kushaur
 
wewe lift unawapa wanawake tu???
au wanaume huwaonagi wakihangaika na tabu ya usafiri,...??
pole nadhani ulitaka kutumia gari yako kama chambo cha kupatia wanawake.....na ukawapata kweli.....
kifupi,usimpe huyo dada lift tena ukimuona uchune atajifunza kusonya watu asiowajua,uchune kabisaaa kama hujamuona kwanza una mtu mwingine wa kupiga naye stori kwenye gari (jirani) incase boredom ndio inakusumbua....
and second,jifunze kutokana na hii experience ya kusonywa kuwa OPEN,huyu dada wa pili asije akapata bichwa kwa kuona mwenzie 'kaachia ngazi' hivyo kumpa false hopes yeye kawa 'promoted' mwambie wazi kilichotokea na unafanya hivyo kama msaada tu na si vinginevyo...ili na yeye asipate matumaini ya kukuzoa...
mwisho OA uwe unampe lift mkeo tu.......ukionyesha udhaifu kuna wanawake ni mapapa yapo kuwinda tu shaurilo....

Aiseeee kumbe wanawake ni mapapa! Wanafaa kwa mchuzi eti eenh?
 
Ushauri wa bure. Achana naye atakuletea balaa kama angekuwa mkeo je? Kwa nini akasirike naye ulikuwa unamsaidia tu unless katika mazungumzo yenu katika siku mbili tatu ulizompa msaada wa usafiri ulitamka kitu ambacho kilijenga matumaini kwake!!

Nimeipenda hii advise.. Hebu m-PM mshikaj kwa msisitizo
 
binafsi nimekuelewa mkuu.pengine hujawahi kumpenda huyu dada ila alijiaminisha kuwa hueda one day YES.....kwa kifupi achana nae na usimpe lift tena ....wakati anafunga mlango na kusonya ndo alikuwa anajimaliza........kaa nae mbali...hakuongezi humuongezi.....wema usizidi uwezo mkuu......

umenena pia
 
Mbona mkuu HP hiyo kesi imeisha toka pale alipozira na kukataa kupanda gari!...au nini unataka zaidi ya hilo?kama lifti ulitoa kwa huruma yako,mpewaji sasa haitaji wewe unatafuta kitu gani kingine?....au mkuu kuna kitu zaidi ya lifti ambacho unaona utapoteza kutokana na hilo tukio?.....yeye kapotezea then wewe potezea zaidi yake....hakuna kesi hapo kiongozi.

Kwa hayo mkuu nadhan kakuelewa na cc wengine tumeuchukua... Mkuu don umesomea guidence and counselling nn?
 
Yaani hapo hakuna hata lakujiuliza kama amepotezea hiyo wala hamna kesi ingawa kwa tabia aliyoonyesha atakiwi kupewa lift tena, wewe endelea kumpa lift jirani hata wezi wakija nyumbani atapiga kelele.
Labda huyo msichana anabifu na jirani
 
Back
Top Bottom