Nimezimiwa simu

C

coco bella

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2016
Messages
319
Points
500
C

coco bella

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2016
319 500
Kama nilivyokuja na uzi wangu wa kuomba wenyeji kwenye baadhi ya mikoa, nashukuru nimetoka Mtwara ahsante kwa mwenyeji wangu kwa ukarimu wako, juzi wakati nipo Mtwara nikapata mwenyeji wa Dodoma lakini mwenyeji huyu maongezi yake ilikuwa anataka tu nimletee vitu kama Nguo sijui viatu halafu anataja vitu vya bei, nikamjibu mbona hata Dodoma vipo?

Yeye akajua fika mimi nitabeba hivyo vitu leo nimepanda gari kuelekea Dodoma tumewasiliana vizuri nimefika njia panda ya Gairo ananiuliza umenibebea vitu nikamwambia sijabeba, jamani kanitolea maneno ya shombo na kuniambia utajijua mwenyewe tafuta mwenyeji mwingine. Nimejaribu kumpigia simu hapokei na kwa sasa ameizima kabisa!!! Labda nikuambie ulichofanya ni utoto mkubwa Kama ulitaka wa kumchuna kwangu umenoa Dodoma ndogo sana hii siwezi kupotea.
 

Forum statistics

Threads 1,324,981
Members 508,911
Posts 32,179,402
Top