Nimezimiwa simu

Nimezimiwa simu

coco bella

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2016
Posts
305
Reaction score
315
Kama nilivyokuja na uzi wangu wa kuomba wenyeji kwenye baadhi ya mikoa, nashukuru nimetoka Mtwara ahsante kwa mwenyeji wangu kwa ukarimu wako, juzi wakati nipo Mtwara nikapata mwenyeji wa Dodoma lakini mwenyeji huyu maongezi yake ilikuwa anataka tu nimletee vitu kama Nguo sijui viatu halafu anataja vitu vya bei, nikamjibu mbona hata Dodoma vipo?

Yeye akajua fika mimi nitabeba hivyo vitu leo nimepanda gari kuelekea Dodoma tumewasiliana vizuri nimefika njia panda ya Gairo ananiuliza umenibebea vitu nikamwambia sijabeba, jamani kanitolea maneno ya shombo na kuniambia utajijua mwenyewe tafuta mwenyeji mwingine. Nimejaribu kumpigia simu hapokei na kwa sasa ameizima kabisa!!! Labda nikuambie ulichofanya ni utoto mkubwa Kama ulitaka wa kumchuna kwangu umenoa Dodoma ndogo sana hii siwezi kupotea.
 
kwa hiyo jamaa wa mtwara kajilia siku hizo zote au? Haya mambo haya
 
Mimi sikumlazimisha mtu awe mwenyeji wangu naomba nieleweke
 
Duh pole ila bado upo Tanzania nawala haupo Burundi so sheria nizilezile mkuu naulipotoka
 
Back
Top Bottom