Nakupa pole kwa msala ulioupata. Nakushauri kama una uhakika kuwa kweli humpendi huyo mwanamke mwache, utakuja kumtesa bure mtoto wa watu. Ila usije ukaja ukamsumbua hapo baadae maana baadhi ya nyie wanaume hamueleweki. Ntakupa kisa kilichonipata mimi katika maisha yangu.
Nilizaa mtoto na mwanamume niliyekuwa kwenye mahusiano nae kwa muda wa miaka sita. Kiukweli ile mimba ilikua ni bahati mbaya sikupanga kuzaa, nilipomwleza mwenzangu alikuja juu na akataka mimba itolewe na akadai kuwa hanipendi.Sikuwa tayari kuua kiumbe kisichokua na hatia, nililea mimba yangu kwa masimango na mateso makali toka kwake, baada ya kujifungua aliondoka akaniacha nikiwa na mtoto wa wiki tatu tangu azaliwe. Niliumia sana moyoni lakini nikajipa moyo nikalea mwanangu. Alipofika huko alikoenda alikutana na mwanamke mwingne na wakaharakisha kufunga ndoa, nadhani alifanya haraka ili kunikomoa na kunionyesha ni jinsi gani hanipendi.Baada ya miezi kama mitano ya ndoa yake tulionana kwan nilipangiwa kufanya kazi karibu na eneo alilokua akifanyia kazi yeye. Huwez amini akaanza kunisumbua akiniambia kuwa eti ananipenda tena baada ya kuniona nimenawili. Na mpaka kesho anaendelea kunisumbua kuwa anananihitaji, sasa sijui huko aliokenda amekutana na kitu gani mpka atamani kurudi huku kwangu.
Kiufupi baadhi ya wanaume huwa hawajui wanataka nini katika maisha yao, TSN unaweza ukamuacha huyo mzazi mwenzio na ukaenda kuoa mwanamke mwingne , mwisho wa siku unaweza jikuta unarudi kwa huyu huyu uliyesema humpendi. KUWA MAKINI NA MAAMUZI YAKO. TAFAKARI MARA MBILIMBILI KABLA HUJAAMUA KUFANYA JAMBO.