Mhhh ngoja nikumbuke
Wengine waliishia pale pale std seven wakaja kuwa mafundi magari au carpenter
Mmoja ni dr kwa sasa ana maisha yake na familia yake
Mwingine was my friend yuko African Court of human and peoples right wengine ni wafanyabiashara japo hawakuendelea na shule
Duh ni great moment sana unapokutana na mtu mliyemaliza nae la saba
mmm nimekumbuka mbali sana.Sisi tulifaulu wawili tu kati ya 65.Mimi nikaenda sec wa pili mdada akaenda wakati huo ualimu grade B..Enzi hizo usafiri kwa train na mabasi ya TRC natunatumia warrant..na tunapewa masurufu ya njiani wewe...Basi bwana
Long tym man!
Hahaaaa! Tulifaulu 3 kati ya 44, wawili waliishia form four, mmoja anafanya PhD sasa hivi, wengine wana wajukuu, kuna lidada limoja lilikuwa libabe ile mbaya, sasa hivi lina wajukuu watatu! Choka mbaya, nyumba inataka kumuangukia huko kijijini,.....pamoja na ubabe wake wakati ule, sijisikii vibaya kuwasaidia wajukuu zake ili wasiishie alikoishia bibi yao.
baada ya form four karibu wote wako kijijini wanne tu waliendelea na shule, na mie ndio neema imefunguka kwa sasa nipo chuo, ...naomba Mungu anipe moyo wa ujasiri nisome nifaulu... ukifikiria ni ngumu kuamini, maisha magumu sana ndugu yangu
Huu uzi umenikumbusha mbali sana...mie ninajua walipo wawili kati ya darasa zima tuliomaliza nao std 7 enzi hizo.
Inauma sana kuona kuna wengin wamepoteza mwelekeo siku nyingi zilizopita.
mimi huwa nafarijika ninapowaona wale waliokuwa hawana akili but wamefaulu maisha....
Kuna rafiki yangu namkumbuka sana nilimaliza nae la 7, sijui alipo. Natamani siku moja tuonane tena.
I'm honoured by your compliment.
Thanks to my new "name" here,the old one was not me,it forced me to
wear the character of the name hahaha.