mzee wa kasumba
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 1,439
- 2,918
Zawadi zawadi yangu, uwapi binti mweupe
Kipenzi wa roho yangu, kabinti mwenye mapepe
Na ahadi za kizungu, wacha ukweli nikupe
Leo nimewakumbuka, ma X wa kitambo
Kwakuwa mwana sanaa, nitawataja kwa beti
Yameshapita masaa, simsahau Bahati
Alojiona staa, ameolewa BABATI
Leo nimewakumbuka, ma X wa kitambo
Felista wa kiburi, leo nimekukumbuka
Nilikwisha kukariri, dakika umeshawaka
Ni binti ulo na siri, mtoto ukanibambika
Leo nimewakumbuka, ma X wa kitambo
Halima mke wa mtu, ila nilikukoleza
Kamwe hukutaka katu, kabisa kunipoteza
Ulinipa vingi vitu, kwa kule kukukojo,,,,
Leo nimewakumbuka, ma X wa kitambo
Wapi FATUMA chibonge, tipwa tipwa uteteme
Uliiruka senyenge, kisa mimi mwanaume
Kwa sasa upo Kijenge, nasikia una mume
Leo nimewakumbuka, ma X wa kitambo
Mtoto wa mchungaji, Beatha sikusahau
Tulipokuwa Kimbiji, enzi zetu za pilau
Mwisho nakujisha uji, Muhuni kapanda dau
Leo nimewakumbuka, ma X wa kitambo
Sikusahau Anita, uliye nizidi umri
Miaka kumi na sita, ila wewe ni hodari
Wanakwita mama Peter, au tena ma- Johari
Leo nimewakumbuka, ma X wa kitambo
Penzi langu liliyumba, kwako dada Mwantumu
Kisa ni zangu KASUMBA, kwakweli sikulaumu
Ulilea yangu mimba, japo kigumu ugumu
Leo nimewakumbuka, ma X wa kitambo
Maisha hubadilika, ulipo leo si jana
Leo niliwakumbuka, mademu tulonyengana
Ilishapita miaka, basi hapa natuwama
Leo nimewakumbuka, ma X wa kitambo
By: Mzee wa Kasumba
jamani mie sio mshairi, bado najifunza. NAOMBA KUKOSOLEWA (MALENGA)