Maisha pesa
JF-Expert Member
- Nov 6, 2015
- 681
- 632
Kuna denti wa chuo fulani jijini Dar (jina kapuni) tulikutana wakati anaenda chuo na mimi naenda kazini nikampa lift hadi chuoni kwao nikachukua namba ya simu tukawa tunawasiliana.
Siku ya nane nane nikaona nimtafute tukapanga tukutane maeneo fulani Sinza. Sasa bana akaja na kijiji yuko na wenzie 4 na yeye wa 5 halafu naskia wenzao wawili wako njiani wanakuja eti wanawapitia waende beach.
Huku wakiwa na nyuso za furaha kama fisi anayejiandaa kumnyonya mbuzi damu na mimi nikaanza kunyongonyea lakini ujasiri ukanijia ikabidi nisimame kama mwanaume nikawaambia usawa huu wa Magu kila mtu anywe soda moja moja halafu tukaogelee beach.
Aisee sura zao zilibadilika ghafla wakawa kimya nikabaki mimi nawapigia stori za Magu alivyobana, maisha tight, tunashindia mikate maofisini baada ya hapo wakaanza kuondoka kwa mafungu hata denti mwenyewe akaniaga anaondoka na rafiki yake wanaenda kumsalimia mjomba wake. Hadi leo hii siku ya tatu hapokei simu yangu.
Sent using Jamii Forums mobile app