Nimewakamata wezi wa ajira mtandaoni!

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,101
6,027
Baada ya kuapply tangazo lao la kazi huko Uranium Songea,fasta wakanipigia simu wakadai wapo kwenye mchakato wa kuita watu kwenye interview lakini tutangulize kwanza laki 2 kwa M-PESA, nikawakubalia...nikaja hapa jamvini kuhoji uhalali wa hii kampuni kwa kiasi kikubwa hivyo kabla hata hatuajiriwa. Nikachukua mawazo yote ya wanaJF, nikatengeneza maswali yangu kadhaa naomba uyajibu.

Halafu nikampandia hewani yule jamaa aliyejitambulisha kama Ishe Mboma, simu ikaitaaaa weeee, hadi ikakatika haikupokelewa. Baada ya kama dakika 5simu yangu ikaaza kuita, kucheki yule jamaa ananipigia. Nikapokea!!

Maongezi yakaanza kama ifuatavyo: Nilianza kumwambia kwamba nina fedha mkononi na nipo dukani Mpesa tayari kuzituma, ila nina mawali matatu tu naomba uyajibu kabla sijatuma.

Swali la kwanza nilimuuliza, Je hiyo ni kampuni au ni Recruitment Agent(RA)? Akanijibu yeye ni HR wa ndani ya kampuni na sio RA.
Nikamuuliza huo mgodi unaochimba Uranium upo wapi? Akanijibu upo songea na mpaka kijiji akanitajia...Nikamuuliza Wewe mwenyewe na hiyo kampuni mpo wapi(nikajua wapo dar)..akanijibu wapo Songea mjini 2 km kutoka pale mjini.
Nikamwambia kama upo Songea basi na mie nipo hapohapo Songea unaonaje tukionana halafu nikakukabidhi mzigo ana kwa ana....!!


Hapo jamaa aliniachia vumbi baya!! Akaniambia ''This thing is very confidential and we are not allowed to have personal meeting'' Nikamwambia NIMEKUKAMATA MWIZI MKUBWA WEWE. AKAKATA SIMU.

SO TUWENI MAKINI JAMANI NA HAWA JAMAA WANAOTOA KAZI HALAFU WANATAKA FEDHA KWANZA, BILA KUJA HAPA JF NISINGEPATA MAWAZO YA KUULIZA STRONG QESTION YULE BWANA,MANAKE ALISHANIBAMBA.
 
ungetoa na namba zao za simu kabisa ili watu wengine wkipigiwa simu wajue kuwa huyo anayepiga ni tapeli

Nadhani umewasahau matapeli,huwa wanakuwa na line tofauti tofauti kibao hiyo waliyompigia jamaa wanaweza hata wasiitumie tena kwa siku za usoni
 
warerere!!!!yaani imekula kwake angejipatia fuba ki ulaini na usawa wenyewe huu wa kulenga kwa manati.asante kwa kutufahamisha hili.
 
hahaha ulimshika pababaya akamua kukimbia .. Safi sana

Agh nilimshika nyeti...manake kuna muda nilimwambia kwanini asinipe hiyo akira halafu tufanye arrangement mshahara wangu wa kwanza nikamkatia kiasi anachotaka...akakataa!! Nikaona huyu jmaa ni magumashi!!
 
Jamani kazi tunayo sasa hivi tunaotafuta kazi inabidi tuwe makini sana mi mwenyewe imenikuta ivyoivyo hapa arusha baada ya kumpigia jamaa akarusha nikamshtukia ni jambawazi.But iwish ningenkamata live ili tuwakomeshe.
 
weka namba ya simu hapa tuone amejiandikisha kwa jina gani mpesa. kwa mfano, kama ni namba ya voda ukawa huna salio kwenye m-pesa fuata maelekezo yote kama vile unatuma pesa hadi mwisho, meseji utakayopata itakuambia huna salio la kutosha kumtumia so and so salio lako ni 0, au kama una salio, tuma salio ambalo ni zaidi ya kiwango ulichonacho, mfano kama una laki 2, tuma laki 4, utapata jina lake alilojiandikisha na unaweza kulileta hapa JF tukamsaka.

Jina la laini amejiandikisha CURTIS IBINZA

Unaweza kumcheki facebook kama alitumia jina lake sahihi.
 
weka namba ya simu hapa tuone amejiandikisha kwa jina gani mpesa. kwa mfano, kama ni namba ya voda ukawa huna salio kwenye m-pesa fuata maelekezo yote kama vile unatuma pesa hadi mwisho, meseji utakayopata itakuambia huna salio la kutosha kumtumia so and so salio lako ni 0, au kama una salio, tuma salio ambalo ni zaidi ya kiwango ulichonacho, mfano kama una laki 2, tuma laki 4, utapata jina lake alilojiandikisha na unaweza kulileta hapa JF tukamsaka.

Wazo zuri, nimejaribu mwenyewe kutuma imeniletea jina la CURTIS IBINZA.....Ila yeye alinitajia anaitwa ISHE MBOMA....Kazi kwelikweli hapa bongo
 
Anaweza kutafutwa kwenye Facebook au hata kujaribu ku google hilo jina pia,
Safi sana ulimshika pabaya
 
kukomesha watu kama hawa, kwa nn usimripoti polisi, hoping watamshughulikia au watamtoa upepo- vyote ni adhabu tosha !!
....Interesting katumia jina la Mboma, kumbuka huyu m-meremeta ana miradi ya machimbo... mmmmhh !! Hapa kuna pazuri pa kuanzia...
 
Hongera sana hiyo ndiyo dawa yao hawa wezi.......... umefanya jambo la maana sana ndugu yangu
Keep it up
 
hongera, watu wanalizwa sana, tunashukuru kwa kutujulisha tutakuwa makini na hizo nafasi za kazi hewa.
 
Back
Top Bottom