Nimewahi kuwa changudoa, nimjulishe?

Nimewahi kuwa changudoa, nimjulishe?

Marytina

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
9,738
Reaction score
8,005
Changudoa home Arusha, baba Mngoni, mama Mchagga

Ilikuwa hivi; baba na mjomba waliwekwa Korokoroni kwa kesi ya ujambazi tukiishi na kusoma Arusha. Mimi na wadogo zangu wawili kuna siku ghafla kama saa nne mama akaja shuleni (day skuli) akatuchukua (wawili, mdogo alikuwa hasomi) bila kupitia nyumbani tukaelekea Tanga tukakaa hotelini for two weeks then tukaelekea Kenya Nakuru ambapo mama alinunua nyumba na gari tukaanza maisha bila ya baba na mjomba.

Wote watatu tukapelekwa boarding skuli Nairobi-Kenya, mama akarejea Nakuru. Miaka minne baadae mama akakamatwa akarejeshwa Arusha kuunganishwa kwenye kesi. Mimi ndiye nlikuwa mtoto wa kwanza na wote hatukuwa tumejua kama mama kakamatwa mpaka tuliporudi nyumbani likizo.

Majirani walitushangaa na kuanza kutuuliza alipo mama. Kwa msaada tukavunja mlango, gari ilikuwepo, kuna chumba ilikuwa inafungiwa. Niliwaambia wadogo zangu mama kaenda kumsalimu mjomba atarejea. Nikaanza misele Nakuru mjini na kiboyfriend changu. Siku moja akaja mama fulani nilipokuwa nimepaki kigari mjini akajitambulisha ni Mtanzania mmarangu na aliongea kichagga nikazuga simsikii.

Akaniambia amenitambua kwa kuwa anaifahamu gari ya mama na anajua mama na nimefanana na mama. Akanieleza kuhusu mjomba, baba na akaniambia mama alikuwa gerezani Arusha kwa kesi. Akanitaka niiuze gari na nyumba fasta kabla havijakamatwa.

Akaniambia nisiwe narudi rudi kukaa muda mrefu pale nyumbani mpaka atakapoachiwa mama. Nilikuwa form three-Nairobi, four days baadae niliuza gari, nyumba ikagoma kwa kuwa collateral ya mkopo alichukua mama benki. Nikawaamuru Madogo tuondoke tuwahi kurudi shuleni mama anatusubiri Nairobi.

With time hata mwaka haukuisha hela ikakata nikashawishiwa na a classmate Elizabeth-Mkenya mkamba wa Nairobi. Tukaanza kujiuza likizo and life ikasonga na nikawa nawalipia wadogo na mimi ada. Nilijiuza mpaka nikasoma chuo na wadogo wakaingia sekondari.

Thanks God mama aliachiwa baada ya miaka mitatu. Kuna wakati tuligombana sana na wadogo zangu wakiamini mama amenipa access ya akaunti zake za benki na natumia hela nyingi kivyangu huku nikiwapa wao kidogo.

Tatizo: Kwa sasa tupo Arusha. nina boyfriend mmasai na kila wakati wa semina kanisani mchungaji husema ni bora wapenzi wachumba muwekane wazi kuhusu maisha yenu hata ya nyuma ili isiwagharimu baadae. Naogopa sana kumwambia jamaa kuwa niliwahi kuwa changudoa.

NOTE: Kuna wadada wa Kenya ambao nilijiuza nao wamehamia Arusha na hawana kazi za maana.

Nlilazimika kuhama kanisa ambalo mimi nlikuwa kiongozi wa vijana baada ya baadhi yao kuanza kusali pale kanisani uamuzi ambao BF na mchungaji wanaushangaa mpaka leo. Kwa sasa nasali kikanisa kidogo nje ya mji kwa kuwaogopa washirika uchangudoa wenzangu wa Nairobi... Nateseka sana kuwaza.

Ufafanuzi: Natumiwa PM nyingi zikitaka ufafanuzi. Hii stori ni 5% ya maisha yangu na inaeleza namna nilivyoanza na kuacha uchangudoa tu. Stori haielezi maisha ya mama wala mjomba, namna walivyokamatwa na nini hasa walichokuwa wakifanya, namna mama alivyotoroka na baadae kukamatwa. Haielezi namna tulivyosafiri toka ARUSHA-TANGA-NAKURU KENYA.
 
it wasnt your will kua changudoa hustle za maisha zilikufanya uwe vile na hata hvyo hyo kaz ilikufanya ufike hapo ulipo sasa? naamin hata wadogo zako hawajui hilo kutokana na maelezo yako. kwa ushaur anza kuongea na familia yako ukifanikiwa hapo ukaongee na mchumba wako!

am proud of what you did si kwa kua changudoa ila kwa umr wako kuweza kusimamia wadogo zako na wewe kusoma mpaka chuo kikuu
 
Ukisema ukweli tu umeula wa chuyaaa,maana hata yeye kuna aliyoyafanya lakim hatakuambiaa kila mtu siri yakee we baki na yako watanzania kwenye ukweli bado hatujajifunza

tatizo nimekuwa mtu wa dini na sipendi kuendelea kuwa muongo kama mama alivyonidanganya
pia kuna waschana wawili wakenya wanaishi hapa ARUSHA na tulifahamiana KENYA kwenye hotel
 
tatizo nimekuwa mtu wa dini na sipendi kuendelea kuwa muongo kama mama alivyonidanganya
pia kuna waschana wawili wakenya wanaishi hapa ARUSHA na tulifahamiana KENYA kwenye hotel

my dear kua muazi kwake kama ulipangiwa awe ndo mumeo atakua bila mashaka hakuna kitu kizuri kama kua mkweli wa nafsi kamwe haikusuti kua makini usijejuta baadae
 
Usijaribu kumwambia utakuwa umejiharibia. Maana yatafuata maswali mengi sana ni bora ukakaa kimya
sikuwahi kufanya kinyume na maumbile
pia kuna wadada wakenya wako hapa AR wanaweza kuvujisha hii siri ikawa msala zaidi sjui hata nianzie wapi..
 
Nani atakubali kuoa changu, bora ukae kimya sio kila kitu ni cha kuweka wazi hapa duniani.
what if i keep it down as posibo ila akajajua baadae kupitia kwa wadada wakenya ambao wako hapa AR?
 
it wasnt your will kua changudoa hustle za maisha zilikufanya uwe vile na hata hvyo hyo kaz ilikufanya ufike hapo ulipo sasa? naamin hata wadogo zako hawajui hilo kutokana na maelezo yako. kwa ushaur anza kuongea na familia yako ukifanikiwa hapo ukaongee na mchumba wako!

am proud of what you did si kwa kua changudoa ila kwa umr wako kuweza kusimamia wadogo zako na wewe kusoma mpaka chuo kikuu
so...if ur proud of me niwe mkweli kwa jamaa na kikiwaka utanipigia chepuo kwako au kwa mshikaji wako anioe?
 
home arusha,baba mngoni ,mama mchagga

...NAOGOPA SANA KUMWAMBIA JAMAA KUWA NLIWAHI KUWA CHANGUDOA

Vp na T.G. iligongwagongwa kidogoo
Na utamu wake Vp bado waukumbuka?

Je? unatamani siku moja tena u...T.G.gike
 
tatizo nimekuwa mtu wa dini na sipendi kuendelea kuwa muongo kama mama alivyonidanganya
pia kuna waschana wawili wakenya wanaishi hapa ARUSHA na tulifahamiana KENYA kwenye hotel

Hayo yalishapita ushaomba msamaha kwa muumba wako,kwa wanaume w kibongo ukimuambia ukweli siku mkikosana ndio silaha ya kukuumiza wewe utaambiwa ndio maana ulikua changudoa ,mwambie sasa utayaona tunayokuambia
 
my dear wanasema ukweli humueka mtu huru why usingemueleza toka kitambo? ila hata ukificha tambua hakuna siri chini ya jua
unazidi kuniumiza
hata wadogo zangu hawajui kama nlikuwa najiuza NAIROBI wakati wa LIKIZO....so i do believe hata mchumba wangu anaweza asijue hii siri maisha yake yote.Only my mama anajua hata baba na mjomba wahajui
 
my dear kua muazi kwake kama ulipangiwa awe ndo mumeo atakua bila mashaka hakuna kitu kizuri kama kua mkweli wa nafsi kamwe haikusuti kua makini usijejuta baadae

mmh hivi kaka yako akikueleza kuhusu kutaka kumuoa former changudoa hutamkosoa???
nina kazi nina kijiIST ila nawaza sana itakuwaje ikibumburuka
 
sikuwahi kufanya kinyume na maumbile
pia kuna wadada wakenya wako hapa AR wanaweza kuvujisha hii siri ikawa msala zaidi sjui hata nianzie wapi..

Ndio uwe mbali nao wataanzaje kumuambia mumeo hayo mambo ,kua mbali usiwe na mazoea nao,ukiwaweka karibu lazima watakuharibia maana mtaweza gombana siri ikatokaa
 
MMghhhhhhh ngoja nitafakari kwanza, sio kila mara kweli inakuweka huru
ila pia dini zetu hazitaki uongo na kuna uongo unatesa sana maisha yoote
hapa naogopaga hata kwenda kwenye baadhi ya sherehe maana kuna wadada wakenya hapa ARUSHA wanaweza kuniharibia
 
so...if ur proud of me niwe mkweli kwa jamaa na kikiwaka utanipigia chepuo kwako au kwa mshikaji wako anioe?

read between the lines am proud of what you did as a sisiter to your siblings. and looks like what you want is only marriage you dnt care the consequences anyway utajisikiaje pale ushaolewa halaf anakuja kujua kuhusu hyo tabia yako na akakuacha cz ya hilo swala? ipi ni aibu kubwa kwako?
anyway mi kwangu ukija ntakutreat kama ambavyo walikutreat
 
Back
Top Bottom