Nimevurugwa na nilichokiona, naombeni msaada wenu

kule masaki kulikua na mzungu mmoja anaenda kununua malaya anawapeleka kwake akifika anawaingiza chumbani wanakuta maiti ta mke wake imelala juu ya meza anawambia waifanyie masaje waipambe na maua, kuna waliokua wakifanya ivo ila kuna siku demu mmoja alivoona ile maiti alishtuka akakurupuka mle ndani kutoka nje geti limefyngwa alipiga kelele sana hadi walinzi wa nyumba za jirani wakashtuka wakaja kugonga pale mixer polisi ile kesi ilipofika obay ikazimwa inasemekana yule mzungu alikua amehifadhi maiti ya mke wake siku moja arudi nayo kwao
Hii inafana na ile ya Njiro Arusha
 
Hiyo ndoto ulimsimulia mkeo usiku huo huo au asubuhi. Ila tafsiri ya ndoto hiyo ni kuwa siku za mwisho wako utakuwa wa mateso mengi na kutengwa na watu wako wa karibu.
 
Haya mambo yanaweza kuwa na ukweli ndani yake, nakumbuka kuna kijana wa Bajaj mitaa ya Maringo Kawe kawahi pata kisa hiki.

Yeye anasema aligonga VX maeneo ya Rainbow pale Junction ya Kupanda TangiBovu na ile ya kuelekea Mbezi kwa Zena. Basi naye alinyang'anywa leseni na akaambiwa Jpili akaichukue. Vitu alivyo alivyokutana navyo jamaa anasema ni zaidi ya ushirikina tunao uona kwa movies.
 
Huyu mzee ana vituko sana aisee. Sasa kama wewe babu uko hivi hao wajukuu zako wakoje?
 
Ana kwa ana na msukule.

Siku ya sabasaba Jumanne, mida ya jioni, kama saa moja jioni nilipata ajali, kulikuwa na mvua, tulikuwa barabara ya Mwai Kibaki mitaa ya Kawe Beach, jirani na njia ya kwendea Mediterranio Hotel gari ya mbele yangu ikafunga break ghafla sana, nikaigonga kwa nyuma upande wa kulia na kuvunja taa ya BMW X5 new model.

Nikasimamisha gari na kushuka ili niangalie uharibifu.

Akashuka mzee wa makamo, kama miaka 60, anafoka, unajua gharama ya hii taa, unajua bei yake? Nikamwambia samahani. Akajibu samahani yako itanisaidia nini? Leta leseni yako.

Nikaona isiwe taabu, nikampa leseni yangu, akaenda kuifungia kwenye gari yake, akarudi na kunipa business card yake. Akasema Jumapili 12/07/2020 saa nane mchana unipigie.

Jana jumapili, saa nane kasoro robo nikampigia simu, nilikuwa mitaa ya Sinza nakula kitimoto [emoji201][emoji200][emoji241] na cocktail Konyagi na wine[emoji485].
Nikachukua simu na kumpigia jamaa, sipendi kumtaja kwa jina wala kabila lake.

Jamaa akaniamuru nichukue pikipiki fasta nimfuate nyumbani kwake Mbezi Beach.

Nikachukua bodaboda hadi Mbezi Beach mitaa ya Kwa Zena Kawawa.

Nikamjulisha kuwa mimi tayari nimefika kwa Zena, basi akanipa maelekezo ya kunifikisha hadi kwake.

Nilipofika tu getini, geti likafunguka lenyewe, mimi na bodaboda wangu tukaingia ndani.

Jamani kuna watu wanaishi high life, bonge la crib, swimming pool nzuri, bustani kali, ndege wazuri kama hauko DSM, wanacheza na kuruka huku na huko.

Tukaa kwenye viti vya bustanini, mfanyakazi akaja akamuuliza bodaboda anakunywa nini, aagize chochote bila hofu.

Akaniita kwa jina langu akaniambia nimfuate, mzee ananiita ndani.

Nikaingia ndani, sitting room kubwa, ya kisasa sana, very organized, nikakaa hapo nashangaa shangaa uzuri wa jumba lile.

Baada ya kama dakika ishirini, jamaa akaja, nikamsalimia, akanipokea kwa uchangamfu wa hali ya juu sana.

Akawa mwema sana kwangu, akanipeleka kwenye ki mini bar kilichopo hapo ndani, yeye akachukua pombe ambayo hata sijawahi kuiona inaitwa Dom prognon sina uhakika sana. Akaniambia nijihudumie, mi nikachukua Jack Daniels ndogo na kuimimina kwenye glass.
Kimya kikatawala kama kwa dakika tatu hivi.

Jamaa akavunja ukimya, akanisifia kuwa mimi ni kijana mwaminifu, angekuwa kijana mwingine asingepiga simu, wala asingehangaika na kulipa taa ya bei mbaya.

Nikaendelea kumsikiliza, kisha nikamsihi, anisamehe, anirudishie leseni yangu.

Akasema wa kunisamehe si yeye, gari sio la kwake, ila mwenye gari yupo ndani kapumzika tumsubiri.

Akilini, nikapata picha kuwa gari itakuwa ni ya mkewe, nikaanza kujiandaa kisaikolojia namna ya kukabiliana na mwanamke tajiri mwenye kiburi, jeuri na nyodo.

Zikapita kama dakika ishirini, jamaa akasema turudi sitting room.

Tukaenda, akamwita dada kisha akaagiza amuite XXXX.

Nikajiweka sawa kukabiliana na jimama la kitajiri.

Baada ya kama dakika tatu, dada akaja na li mtu linatisha, limevalishwa t shirt kubwa ina bendera ya Tanzania.

Anatisha, anachuruzika maudenda. Mtoto si mtoto, kijana si kijana, umri hautabiriki.

Nikaambiwa nimuombe msamaha, maana huyo ndiyo mwenye gari.

Nikapiga magoti, nikawa nimevurugwa aisee, naongea tu maneno mara niuite huo msukule mfalme, mara niuite boss, mara uncle, mara kaka... ili mradi najisemesha.

Msukule ule ulipiga kelele mpaka nikashtuka, ukacheka sana, basi yule jamaa akaniambia niinuke, na pia XXXX (msukule) amenisamehe na amenipenda sana, kwa hiyo kuanzia sasa mimi ni rafiki wa msukule.

Akanipa leseni yangu. Hakika nilikuwa najiona kama niko ndotoni, kwenye ndoto ya kutisha na ya kuogofya sana.

Nilikuwa naona kama muda hauendi, nilitamani upepo unichukue, unitoe ndani ya jumba lile.

Hakika nilijiona ndio siku yangu ya mwisho, nikawa nasali kimoyomoyo, nilikata tamaa ya kutoka kwenye jumba lile nikiwa hai.

Basi, jamaa akaniambia sasa naweza kuondoka kwani bodaboda amekaa nje muda mrefu.

Nikaanza kuinuka kitini ili niondoke.

Jamaa akasema sijamuaga rafiki yangu.

Akamwambia dada anipeleke nikauage ule msukule.

Nikamfuata dada, tukapiga kona, tukakuta kuna lift, akabonyeza twende juu.

Tukafika, mlango una fingerprint reader, akaweka dole gumba, akafungua mlango, akaniacha mle ndani kisha yeye akatoka.

Mle chumbani kulikuwa ni kuzuri sana, chumba kina makorokoro ya watoto, chumba kikubwa, kina vigari, Spider-Man, Ben Ten, na TV kubwa inaonyesha makatuni.

Hapo nimevurugwa, sijui nifanye nini, nimefungiwa.

Nikaogopa sana, nikaanza kuhisi labda nimeletwa pale ili nigongwe na ule msukule. Nikawa nina mawazo mengi sana, baada ya kama dakika kumi na saba, mlango ukafunguliwa, akaingia jamaa, akasema naona uko na rafiki yako. Nikajibu ndio tunaangalia katuni.

Basi, tukatoka mle chumbani, akanishusha chini.

Sebuleni akauliza kama nina mke na watoto, pia akaniuliza kama nimejenga ama nimepanga.

Nikamjibu nina mke na watoto wawili, na nimepanga.

Basi akanipa laki tatu, akasema nikanunue chakula cha watoto, akanipa laki tatu nyingine, nikalipe umeme na maji, akanipa million tatu nikalipe pango ya nyumba, laki tano ya kutengenezea gari yangu, akanipa na elfu hamsini ya kumlipa bodaboda na akanionya kwa msisitizo, hela ya bodaboda nisipunguze hata shilingi moja. Na akasema niwe naenda kila Jumapili kuongea na rafiki yangu.
Nilipotoka nje, nikamwambia bodaboda akimbize sana hadi nyumbani.

Nilipofika nikamuuliza ananidai bei gani, akasema elfu kumi na tano. Nikampa elfu hamsini, jamaa hakuamini.

Nilipofika ndani, nilipitia kulala, nikalala sana. Mida ya saa saba usiku, usingizi ukakata, nikamsimulia mama watoto kila kitu.

Kashauri hizo hela tuzifanyie maombi na tusizitumie kwani ni hela za kipepo.

Kwakweli siko vizuri, leo nimeshindwa hata kwenda kazini.

Kuumwa siumwi, uchovu, hofu, mwili kama sio wangu, breakfast imenishinda, yaani nimevurugwa mazima.
Nlishaisomaga fb miaka hyo,
 
Upande mwingine ukute huyo tajiri hana uchawi wowote... Ila ni huyu kijana kuona lile jumba. Na yale mazingira hakuyategemea kuyaona tz hii.. kuhusu yule ,, watoto wengi wa matajiri wakizaliwa vilema hasa vilema vya akili huwa wanafungiwa ndani ya geti kazi yao ni kula kucheza na kulala, wananenepeana sana, kiasi hadi wanatisha na udenda kama huyo. Huyo mtoto sio msukule sema tu ana matatizo ya akili. Usipoteze bahati ndugu yangu kujuana na matajiri ndio mwanzo wa utajiri ... Kumbuka: kaa na matajiri upate utajiri.. utaishi nyumba ya kupanga hadi lini.
Unaweza kuwa sahihi.Walemavu wengi wa akili wanadhaniwa kuwa misukule
 
Haya mambo yanaweza kuwa na ukweli ndani yake, nakumbuka kuna kijana wa Bajaj mitaa ya Maringo Kawe kawahi pata kisa hiki.

Yeye anasema aligonga VX maeneo ya Rainbow pale Junction ya Kupanda TangiBovu na ile ya kuelekea Mbezi kwa Zena. Basi naye alinyang'anywa leseni na akaambiwa Jpili akaichukue. Vitu alivyo alivyokutana navyo jamaa anasema ni zaidi ya ushirikina tunao uona kwa movies.
Hebu weka nyama za kutosha
 
Embu picha yake ..maana wabongo wakisema new model unakuta Ni ya mwaka 2005
1671637883136.png
 
Ana kwa ana na msukule.

Siku ya sabasaba Jumanne, mida ya jioni, kama saa moja jioni nilipata ajali, kulikuwa na mvua, tulikuwa barabara ya Mwai Kibaki mitaa ya Kawe Beach, jirani na njia ya kwendea Mediterranio Hotel gari ya mbele yangu ikafunga break ghafla sana, nikaigonga kwa nyuma upande wa kulia na kuvunja taa ya BMW X5 new model.

Nikasimamisha gari na kushuka ili niangalie uharibifu.

Akashuka mzee wa makamo, kama miaka 60, anafoka, unajua gharama ya hii taa, unajua bei yake? Nikamwambia samahani. Akajibu samahani yako itanisaidia nini? Leta leseni yako.

Nikaona isiwe taabu, nikampa leseni yangu, akaenda kuifungia kwenye gari yake, akarudi na kunipa business card yake. Akasema Jumapili 12/07/2020 saa nane mchana unipigie.

Jana jumapili, saa nane kasoro robo nikampigia simu, nilikuwa mitaa ya Sinza nakula kitimoto 🐽🐷🐖 na cocktail Konyagi na wine🍷.
Nikachukua simu na kumpigia jamaa, sipendi kumtaja kwa jina wala kabila lake.

Jamaa akaniamuru nichukue pikipiki fasta nimfuate nyumbani kwake Mbezi Beach.

Nikachukua bodaboda hadi Mbezi Beach mitaa ya Kwa Zena Kawawa.

Nikamjulisha kuwa mimi tayari nimefika kwa Zena, basi akanipa maelekezo ya kunifikisha hadi kwake.

Nilipofika tu getini, geti likafunguka lenyewe, mimi na bodaboda wangu tukaingia ndani.

Jamani kuna watu wanaishi high life, bonge la crib, swimming pool nzuri, bustani kali, ndege wazuri kama hauko DSM, wanacheza na kuruka huku na huko.

Tukaa kwenye viti vya bustanini, mfanyakazi akaja akamuuliza bodaboda anakunywa nini, aagize chochote bila hofu.

Akaniita kwa jina langu akaniambia nimfuate, mzee ananiita ndani.

Nikaingia ndani, sitting room kubwa, ya kisasa sana, very organized, nikakaa hapo nashangaa shangaa uzuri wa jumba lile.

Baada ya kama dakika ishirini, jamaa akaja, nikamsalimia, akanipokea kwa uchangamfu wa hali ya juu sana.

Akawa mwema sana kwangu, akanipeleka kwenye ki mini bar kilichopo hapo ndani, yeye akachukua pombe ambayo hata sijawahi kuiona inaitwa Dom prognon sina uhakika sana. Akaniambia nijihudumie, mi nikachukua Jack Daniels ndogo na kuimimina kwenye glass.
Kimya kikatawala kama kwa dakika tatu hivi.

Jamaa akavunja ukimya, akanisifia kuwa mimi ni kijana mwaminifu, angekuwa kijana mwingine asingepiga simu, wala asingehangaika na kulipa taa ya bei mbaya.

Nikaendelea kumsikiliza, kisha nikamsihi, anisamehe, anirudishie leseni yangu.

Akasema wa kunisamehe si yeye, gari sio la kwake, ila mwenye gari yupo ndani kapumzika tumsubiri.

Akilini, nikapata picha kuwa gari itakuwa ni ya mkewe, nikaanza kujiandaa kisaikolojia namna ya kukabiliana na mwanamke tajiri mwenye kiburi, jeuri na nyodo.

Zikapita kama dakika ishirini, jamaa akasema turudi sitting room.

Tukaenda, akamwita dada kisha akaagiza amuite XXXX.

Nikajiweka sawa kukabiliana na jimama la kitajiri.

Baada ya kama dakika tatu, dada akaja na li mtu linatisha, limevalishwa t shirt kubwa ina bendera ya Tanzania.

Anatisha, anachuruzika maudenda. Mtoto si mtoto, kijana si kijana, umri hautabiriki.

Nikaambiwa nimuombe msamaha, maana huyo ndiyo mwenye gari.

Nikapiga magoti, nikawa nimevurugwa aisee, naongea tu maneno mara niuite huo msukule mfalme, mara niuite boss, mara uncle, mara kaka... ili mradi najisemesha.

Msukule ule ulipiga kelele mpaka nikashtuka, ukacheka sana, basi yule jamaa akaniambia niinuke, na pia XXXX (msukule) amenisamehe na amenipenda sana, kwa hiyo kuanzia sasa mimi ni rafiki wa msukule.

Akanipa leseni yangu. Hakika nilikuwa najiona kama niko ndotoni, kwenye ndoto ya kutisha na ya kuogofya sana.

Nilikuwa naona kama muda hauendi, nilitamani upepo unichukue, unitoe ndani ya jumba lile.

Hakika nilijiona ndio siku yangu ya mwisho, nikawa nasali kimoyomoyo, nilikata tamaa ya kutoka kwenye jumba lile nikiwa hai.

Basi, jamaa akaniambia sasa naweza kuondoka kwani bodaboda amekaa nje muda mrefu.

Nikaanza kuinuka kitini ili niondoke.

Jamaa akasema sijamuaga rafiki yangu.

Akamwambia dada anipeleke nikauage ule msukule.

Nikamfuata dada, tukapiga kona, tukakuta kuna lift, akabonyeza twende juu.

Tukafika, mlango una fingerprint reader, akaweka dole gumba, akafungua mlango, akaniacha mle ndani kisha yeye akatoka.

Mle chumbani kulikuwa ni kuzuri sana, chumba kina makorokoro ya watoto, chumba kikubwa, kina vigari, Spider-Man, Ben Ten, na TV kubwa inaonyesha makatuni.

Hapo nimevurugwa, sijui nifanye nini, nimefungiwa.

Nikaogopa sana, nikaanza kuhisi labda nimeletwa pale ili nigongwe na ule msukule. Nikawa nina mawazo mengi sana, baada ya kama dakika kumi na saba, mlango ukafunguliwa, akaingia jamaa, akasema naona uko na rafiki yako. Nikajibu ndio tunaangalia katuni.

Basi, tukatoka mle chumbani, akanishusha chini.

Sebuleni akauliza kama nina mke na watoto, pia akaniuliza kama nimejenga ama nimepanga.

Nikamjibu nina mke na watoto wawili, na nimepanga.

Basi akanipa laki tatu, akasema nikanunue chakula cha watoto, akanipa laki tatu nyingine, nikalipe umeme na maji, akanipa million tatu nikalipe pango ya nyumba, laki tano ya kutengenezea gari yangu, akanipa na elfu hamsini ya kumlipa bodaboda na akanionya kwa msisitizo, hela ya bodaboda nisipunguze hata shilingi moja. Na akasema niwe naenda kila Jumapili kuongea na rafiki yangu.
Nilipotoka nje, nikamwambia bodaboda akimbize sana hadi nyumbani.

Nilipofika nikamuuliza ananidai bei gani, akasema elfu kumi na tano. Nikampa elfu hamsini, jamaa hakuamini.

Nilipofika ndani, nilipitia kulala, nikalala sana. Mida ya saa saba usiku, usingizi ukakata, nikamsimulia mama watoto kila kitu.

Kashauri hizo hela tuzifanyie maombi na tusizitumie kwani ni hela za kipepo.

Kwakweli siko vizuri, leo nimeshindwa hata kwenda kazini.

Kuumwa siumwi, uchovu, hofu, mwili kama sio wangu, breakfast imenishinda, yaani nimevurugwa mazima.
Bujibuji hii story umekopi kwa yule wa chakula kwa tajiri na vitoto vya Bugiruni.Kind of
 
Back
Top Bottom