Nimevunja kibubu muda huu, siamini nilichokikuta ndani

Nimevunja kibubu muda huu, siamini nilichokikuta ndani

aise

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2018
Posts
8,621
Reaction score
24,164
Dah, yaani hapa wakuu natamani kucheka wakati ni jambo la hovyo limetokea.

Siku ya tarehe 3 mwezi huu, ni juzi tu hapo niliamua kununua kibubu na nikaanza kuweka visenti vyangu ninavyopata kazini, kazini nalipwa kwa kila siku, nikaona hela nayolipwa kwa siku ni nyingi na nikajiapiza kuwa nitakuwa nakula walau robo ya kipato na nyingine nitadumbukiza kwenye kibubu.

Kwakuwa ilikuwa tayari ni usiku na nimeshatumia hela niliyolipwa siku hiyo, nikaamua kukizindua kibubu changu kwa kuweka vijisenti vilivyobaki kwenye matumizi, nikaweka 3,400/=
Tarehe 4. 7,000/=
Tarehe 5. 12,000/=
Tarehe 6. 10,000/=
Tarehe 7 nikaweka chenchi chenchi kama za elfu 3.
Tarehe 8 nikaweka 20,000/=

Sasa kwakuwa huwa nasikia stori nyingi kuhusu vibubu, ikabidi nifanye ziara ya kushtukiza kwenye kibubu changu, nikivunje kibubu nione hesabu zangu kama ziko sawa au vipi.

Haha! Kama mchezo wa kuigiza tu wakuu, yaani Hapa nimekuta 23,000 mpaka siamini nachokiona.

Chenchi zote zipo, kasoro zile noti tu.

Mlaaniwe wauza vibubu
 
Kibubu unatengeneza mwenyewe sio kununua au njia rahisi hifadhi kwenye simu halafu hamishia account yako ya bank every single day, then utajikuta umeweka akiba nyingi sana...
Mkuu hizo njia za benki mara kwenye simu nazifahamu, tatizo natumia laini za "janja janja fc"
sina kitambulisho (nida? Etc)
Labda sina ufahamu sana katika hili.
 
Hivi vibubu mnawezaje?

Mi ni mtaalamu wa kujiibia mwenyewe kwa kutumia kitu chenye ncha nachomoa tunoti.

Afu zikiwa hazitoki tena natikisa mpaka chenchi zote ziishe.

Ila mwisho wa mwaka ndo nitavunja kabisa sijawahi kujua huwa nategemea kukuta nini 🤣🤣
 
Hapa nimekaa kwenye sakafu nafikiria na usiku huu plus baridi hili natamani niende nikachukue kitimoto lost ya hii hela yote iliyobaki niondoe mikosi!
Pole Sana mwanangu, kajipooze na chochote, lakini vp umejaribu kuangalia mazingira unayoishi hakuna mtu mwingne ambae anaweza kuzichomoa? Mpaka ukaamini moja kwa moja Ni mambo ya utamaduni?
 
Back
Top Bottom