Nimevamiwa na kunguni

Nimevamiwa na Jeshi la kunguni naomba msaada nimejaribu dawa mbalimbali za kunguni bila mafanikio tafadhali naomba msaada ili niweze kupambana na jeshi hilo!!.
Hiyo ni dalili ya umaskini hata kama haujafika ila ni dalili kuwa unaenda huko.
 
Hall 1 UDSM BLOCK G mwisho wa maelezo.
Kuna siku wakati nakaribia kuodoka nikasema ngoja nipumzike kidogo. ile kushituka nina kunguni kama 200 wengine watoto. nikajisemea leo nitapanda daladala ya nani!
Wale jamaa , ni nomer
Ni wapole , ila balaa lao , sio la kitoto
 
mokiti vipi?
 
Nimevamiwa na Jeshi la kunguni naomba msaada nimejaribu dawa mbalimbali za kunguni bila mafanikio tafadhali naomba msaada ili niweze kupambana na jeshi hilo!!.
Kazi unayo , watakunyoosha mpaka uombe po ,damn ,I hate those creatures more than anything , Mungu sijui kwanini aliumba hao wanaharamu , walinitesa sana shule ya sekondari bweni washenzi hao
 
Nakupa solution ya kumaliza kabisa tatizo funga geto hilo kwa miezi 3 hadi 5. Ondoka sahau kabisa kama una geto ukirudi hapo broh hautakuta kunguni hata mmoja. Utafanya usafi utaanza upya.

Hii solution ili nisaidia sana. Siasahau nilimkaribisha jamaa yangu geto akaniletea hawa wadudu hii ilikua ndio njia yangu ya mwisho kabisa. Nilifanikiwa kwa 100%
 
Kuna basi flani (***) la Mbeya - Mwanza, ikifika mida ya usiku mnasafiri linaibuka jeshi la viroboto+kunguni, basi utasikia tu abiria wanajipiga makofi ya miguuni, migongoni..
 
UDSM huwa wanafunga chuo mwezi wa 7 katikati na wanafungua oktoba mwishoni kabisa tena first year, mkifika mnawakuta kunguni wamewamiss.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…