KERO Nimeuza gari Mwaka mmoja uliopita na kubadili jina lakini umiliki haujabadilika kwenye mfumo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nimebadilisha jina la gari langu kwenda kwa jina la mtu aliyenunua usafiri huo kutoka kwangu tangu tarehe 23/01/2023 lakini mpaka leo (Februari 2024) mabadiliko hayo ya jina yanasomeka kwenye kadi pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pekee.
cheti.jpg
Upande wa Polisi (traffic side) jina lililobadilishwa halisomi, Wanausalama wakitumia ile mashine ya kuonesha taarifa ya muhusika wa gari inaonesha gari fulani (Plate Number) halidaiwi, kwenye umiliki inasomeka TRANOCON, aina ya gari TRANOCON.

Nimeuliza Askari Polisi nini hasa changamoto ya hali hiyo wanasema mifumo haingiliani.

Nimeenda TRA kuuliza tatizo ni nini wanasema mfumo ndio shida kwa hiyo itachelewa kusoma, ninachojiuliza huo mfumo gani haueleweki.

Tunaomba hili jambo litatuliwe haraka iwezekanavyo kwani linatunyima kufanya biashara na wateja wanaopenda kuhakiki usajili wa vyombo vyao Polisi.
 
Back
Top Bottom