Msaada bei ya kubadili kadi ya gari ununuapo kwa mtu ni kiasi gani kubadili TRA?
MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU
---Document wanazohitaji ni:
1. Mkataba wa kuuzina chombo cha moto.
2. Nakala ya kitambulisho cha mpiga kura/Leseni ya udereva/Pasi ya kusafiria au kitambulisho cha Taifa. Nakala hiyo iwe imeambatishwa na pasipoti ndogo na kuwa certified na Wakili. Hii inahusu pande zote mbili (Mnunuzi na Mnunuaji).
3. Muuzaji anapaswa kulipa 1% ya kiasi alichouza chombo cha moto.
4. Mnunuzi atalipia gharama ya kuhamisha umiliki Bank kiasi cha 50,000/- (kama ni gari) kama kama ni pikipiki atalipa 27,000/-. Pia, mnunuzi a talipia 10,000/- Bank kama gharama ya kadi.
5. Polisi unalipia 5,000/- kwa magari madogo na 10,000/- kwa magari makubwa ikiwa ni gharama ya kukagua gari.
6. Kuwe na kiapo cha Umiliki.
7. Nambari ya Mlipakodi (TIN Number).
---Motor vehicle transfer tax
Motor vehicle transfer tax is payable when a vehicle changes ownership from one person to another. Tax on transfer is payable by the transferee and Stamp Duty on the sale of asset is paid by the seller. The taxes are paid through the bank.
Transfer fees
Motor vehicle TSHS 50,000
Motor cycle TSHS 27,000
New registration card on transfer TSHS 10,000
Stamp Duty 1%
Hapo ni endapo gari hiyo au chombo hicho hakina deni lolote linalo daiwa.
Mkuu hata mimi kama wiki 2 nimetoka fanya change ya ownership ila gari hii ilikuwa ni mpya niliagiza kwa jina langu ila nilipanga liwe LA mzazi jamaa alinipunguzia kiaina kwakuwa niliambatanisha vielelezo vya kifamilia passport ya mzazi na birth certifacate yangu nikamwambia officer hapa hamna mauziano so sijajua kama kweli imefutwa au LA ila as per TRA website 1% bado ipo
View attachment 486883