Nimeupenda ukauzu wa Dr. Maghufuli

Nimeupenda ukauzu wa Dr. Maghufuli

Hivi unadhani kwenye kununua kivuko cha billioni 8 mtu kama waziri akila cha juu atakula ngapi? Hujiulizi? Huyo mzee wako unayempenda Luwasa, amesababisha nchi hii kulipa Richmond bilioni 63 kila mwezi hulioni. Unakomaa na kivuko ambacho saaaana kama kuna ganji itakuwa bil. 1 na mlolongo wa mgawo.
Tatizo hapa huyu Luwasa ni jizi, jizi, jizi balaaaa!!!

Dada Yangu, Mwizi ni mwizi hata kama kaiba pencil.Huyu Lowasa kasema kuwa mwizi wa Pesa za Richmond ni JAKAYA MRISHO KIKWETE, Je yeye magufuri kasemaje kuhusu hiyo Pesa ya kivuko na ile ya nyumbani za serikali???.
 
Kivuko feki chakavu cha mwaka 1978... kanunua bil 8 za Tshs... alafu inaenda Bangamoyo masaa 3... inapakia watu 300 imeshakufaa...!!!

Bahressa kanunua kivuko cha watu 500, kipya cha mwaka 2014, kwa Bil 6 za tshs... na inaenda Zanzibar kwa Lisaa 1:30 tu... JIULIZE SASA...!!!

ASANTE #JAY ONE

Hizo kashifa za kuokoteza tu. Lowasa alishatabiriwa na Hayati Shabaan Roberts katika riwaya ya kusadikika. Katika riwaya huyo yumo mhusika anaitwa MAJIVUNO huyu alikuwa Waziri Mkuu wa nchi hyo kama lowasa. Majivuno alikuwa hataki kukosolewa kama lowasa. Mwenye uchu wa madaraka kama lowasa. Alikuwa na nywele nyeupe kama lowasa,na pia akitaraji kuwa Siku moja atakuwa rais, kama lowasa. Habari njema ni kwamba Majivuno hakufanikiwa kuwa rais, kama lowasa.
 
Wana JF Hola!!

Tumlizoea, kwenye chaguzi nyingi, wagombea kuambatana na wenza wao, kwenye campaign, hii hali imezusha maswali kibao, hasa kwa marafiki zangu wa UKAWA, wamediriki hadi kunitania wakisema Magufuli hana mke, hatutaki Rais bachelor, lakini niliwajibu kuwa ana mke na watoto, ikumbukwe magufuli sio mtu wa kujivuna, Mungu amsaidie, pia anajua anachofanya ni kwa manufaa ya taifa, hata watoto wake wanasoma shule hizi hizi za St Kayumba, hivyo sio mtu wa kujiweka matawi ya juu, Magufuli ana hofu ya mungu kama hutaki kajinyonge. Dkt. Magufuli ni mmoja ya mawaziri wanaoogopwa sana kwa misimamo hata na Rais mwenyewe kwa jambo analoliamini analifanya kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu.

Amemuekeza Kanali Kinana kuwa moja hatapenda kuiona familia yake ikishiriki katika kampeni za urais kwani sitaki familia yangu kujihusisha au kujinasibisha na urais wa nchi.

Nataka nikapambane kufuta hili lililojengeka kwa watoto wa vigogo kubebwa kwenye nafasi za uongozi hata ajira na kuwaacha watoto wa watanzania maskini wakiwa mitaani eti kwa sababu hawana wa kuwashika mikono haki ya Mungu hili nitapambana nalo ili chama hiki kiwe cha wote na nchi hii iwe ya wote.

Hivyo mke wangu naomba aachwe akafundishe,wanangu waendelee na mambo yao na hata ndugu zangu. Jukumu lao kubwa ni kuniombea kwa Mungu ili nikawatumikie watanzania kwa moyo wa dhati bila kiburi na majivuno.

#hapakazitu.

Angekuwa ana hofu ya Mungu (JEHOVA) kusingekuwa na MWENGE kwenye jina lake. Mwenge ni symbolism ya shetani asilimia 100%. Unapoweka mwenge as your symbol maana yake upo kinyume na unampinga Mungu (JEHOVA).
 
Dada Yangu, Mwizi ni mwizi hata kama kaiba pencil.Huyu Lowasa kasema kuwa mwizi wa Pesa za Richmond ni JAKAYA MRISHO KIKWETE, Je yeye magufuri kasemaje kuhusu hiyo Pesa ya kivuko na ile ya nyumbani za serikali???.

Usiwe muongo kama lowasa! Ni wapi na lini Lowasa alimtaja JK kuwa ndo .husika? Alkchosema ni kuwa Richmond yalikuwa maahiza ya mkuu wake. Watu wakamuuliza, kwa nafasi ya uwaziri Mkuu, wakubwa wa kazi ni makamu wa rais na raisi, lowasa sema ni nani kati ya hao? Lowasa kimya hadi kesho. Lowasa ni mwizi hata Nyerere anajua.
 
Babu Lowassa kaambatana na mke na watu kibao kana kwamba anatàka kuwa rais wa familia ama wa marafiki ..simply, Magufuri is the best, he knows the work and how to go about it.
 
Wacha tusubiri tuone hapo mbele maamuzi ya watanzania na mazuio ya goli la mkono
 
Huyu ndo aina ya uongoz tuliokuwa tunawahitaji leo mtu mmoja alikuwa mshabik wa kutupwa wa mamvi kanifuata kaniambia kura yake kwa magufuli kwa sababu ana msimamo mzalendo na ni mtu asiyependa makuu ila sasa hv anapiga kelele za lowasa kwa sababu wameandikwa majina ya kupewa hela na 4u mvt ikikaribia uchaguz
 
Angekuwa ana hofu ya Mungu (JEHOVA) kusingekuwa na MWENGE kwenye jina lake. Mwenge ni symbolism ya shetani asilimia 100%. Unapoweka mwenge as your symbol maana yake upo kinyume na unampinga Mungu (JEHOVA).

Hivi wewe kumbe ni kilaza kiasi hicho? Kwa hiyo mwenge wa uhuru ni ushtani? Kwa hiyo serikali yetu ni ya kishrtani? Acha umbumbu wewe, hapa ni magufuli tu.
#hapakazitu
#mabadiliko peleka mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa
 
Mke wa magufuli ni mwalimu na kwa ratiba ya shule kipindi hiki kuna majukumu mengi na mazito MF. Mtihani wa class 7. So kumzungusha mfanyakazi wa serikali kwenye kampeni inakuwa kukiuka sheria za kazi yeke. Magufuli yuko very right. Nenda baba nenda Baba Mungu akutangulie. Binafsi ninakuombea sana. Nina imani Tanzania ya Magufuli itakuwa Tanzania ya kukumbukwa kwa mazuri mengi.
Mwisho kabisa ninakuomba utakapofika ikulu usinisahau. Baba usitisahau pia watanzania kwa ujumla
 
Back
Top Bottom