Nimeupenda huu ujumbe, usome utakujenga sana

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,525
Tai ni ndege pekee mwenye uwezo wa kuishi miaka 70. Lakini kabla ya kufika umri huo lazima afanye maamuzi magumu, yanayomuumiza na kumchukua muda mrefu.

Akifikia umri wa miaka 40, makucha yake magumu na makali yanakosa uwezo wa kunyakua chakula, mdomo wake uliochongoka unapinda, mabawa yake yanakuwa mazito na kunata kwenye kifua chake hivyo kumfanya kuwa mzito kuruka na kuwa mwenye kasi ndogo.

Katika hali hiyo ndege huyo hubakiwa na maamuzi mawili; aidha akubali kufa au afanye mabadiliko katika mwili wake ili aendelee kuishi miaka 30 iliyobakia. Akichagua kufanya mabadiliko kwenye mwili wake humchukua siku 150 sawa na miezi 5, hivyo huenda katika kilele cha mlima mrefu na kujificha katika pango ambapo watu na wanyama wengine wanaoweza kumzuru hawafiki.

Ndipo huanza kujivua kucha, midomo na mbawa zake zilizozeeka huku akisikilizia maumivu makali, baada ya mabadiliko hayo hurudi katika hali yake ya mwanzo ya kuweza kuruka kwa kasi na kupata chakula chake kizuri (fresh meat).

Bado siku chache sasa ili tumalize mwaka, hivyo lazima ufanye mabadiliko makubwa sana katika maisha yako, ujivue baadhi ya tabia ambazo zimeleta Ukakasi katika maendeleo yako ya 2019 japo zingine ni ngumu kuziacha na pengine zitakusababishia Maumivu lakini "no pain no gain" lazima ujivue baadhi ya Marafiki wasiolekea unakoelekea, jivue Uvivu, jivue Uongo, jivue Mahusiano yasiyo na Amani, jivue Ulevi, jivue kulala sana, jivue Uasherati, jivue kuahirisha ahirisha Mipango yako, na mengine yanayofanana na hayo.

Ikiwa Tai anafanya maamuzi ya kubadilika akiwa na miaka 40, hata wewe bado hujachelewa. Fanya mabadiliko sasa, ingia Mwaka 2020 ukiwa na Tabia mpya na Mtazamo Mpya kwa ajili ya kuanza safari yako mpya ya maisha.

MUNGU Akubariki Sana katika Maamuzi yaliyo sahihi

FB_IMG_1576046465218.jpeg
 
Akili yako huwa yaipuuzi sanaa aya za mwisho hujaona hayo maamuzi au unapenda attention za kipuuzi
Mbona panic sasa au ulikua unataka watu fulani waje kuchangia mawazo fulani amabayo wewe umeyajenga kichwani.?
Usipende tufanane..maishani mwangu kinachonitofautusha na wenzangu ni kujitofautisha na watu. Nafanya vitu kwa jinsi yangu mimi nipendavy ilimradi kiwe sahihi. Kwa mawazo maneno na matendo sifanani na mtu..
Endelea kutaka watu wachangie vitu fulani uvitakavyo sio vitu tofauti ili ujifunze mambo tofauti
 
"Fanya mabadiliko sasa, ingia Mwaka 2020 ukiwa na Tabia mpya na Mtazamo Mpya kwa ajili ya kuanza safari yako mpya ya maisha." Kuanza upya au kuendeleza ulipoishia.

 
Asante sana ushauri mzuri,hasa kuhusu kujivua kuhusiana na hawa wadudu,kwa nini nakwama?
Tendo ama kitu kinachokufurahisha wewe unaita 'wadudu'! Kwanini usitumie neno 'sukari', kisha ukaendelea na hayo mabadiliko kimyakimya kama kweli unataka kujitwist?
 
Naona mtiririko wa zile message ndeeeeefu za kufungia mwaka zimeshaanza
Zipo tu kwenye 'seva', mtu anayekutumia, kazi yake ni ku 'clik' na ukimwambia arudie maneno hayo kuyaandika bila ya kutazamia wala hawezi, maana hajayawaza yeye.

Kwa kuwa msg hizo huwa ninaelewa kuwa ni 'copy', huwa sijihangaishi kuzisoma hata ziwe zimetoka kwa rafiki nnayemheshimu.
 
Back
Top Bottom