Nimeumizwa sana na utangazaji wa Chanel Ten. Kama CCM mmeinunua wafukuzeni watangazaji wasio na weledi

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Ninaomba nikiri kuwa nina matatzo katika uandishi wangu ila naomba ujumbe uwafikie wote. Mimi ni mfatiliaji mzuri sana wa habari nchini mwetu na hata za nje ya nchi hii, ni kwa maslahi yangu.

Siku ya jana niliumia jinsi kituo cha habari cha Channel Ten walivyotangaza habari ya kuungua kwa Soko la Samunge mkoani Arusha.

Hivi kweli ni nini ilikuwa habari pale? Kuungua kwa soko na kuteketea kwa mali nyingi za wajasiriamali, au mjasiriamali aliyekufa ghafla baada ya kuunguliwa na maduka yake mawili?

Kwa kifupi habari hii ililipotiwa vizuri na ITV kwenye habari zake za saa mbili kwa kuanza na kifo cha mfanyabiashara aliyekufa kwa sababu ya mshtuko.

Nitoe rai kwa CCM. Kama mmenunua kituo hicho ni bora kufukuza waandishi wa habari wa namna hii hapo ni kosa la mhariri, mwandishi pia, na msomaji wa habari (kasuku) wachukuliwe hatua.

Sifi leo ikifika kesho ntakuwa tayari kufa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bahati nzuri niliangalia taarifa zote jana.Chanel Ten walikuwa detailed kuliko ITV.
Wewe utakuwa na shida binafsi
 
Back
Top Bottom