Ukiona mtu anamlinganisha mzungu na mwafrika ujue uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana.
Dunia ni ya Mungu , vitu ni vya mzungu.
Mapaka karne hii waafrika hatuna mfumo wetu wa Elimu na hatuwezi kuwa na mfumo wetu wa Elimu.
Mpaka karne hii tunaamini kuwa Elimu ni ile inayopatikana kwa Lugha za wenzetu hasa kingereza.
Naangaliaga tu kule hospitalini palivyo na mashine na vifaa vingi vya kufanya oparationi na kugundua kuwa kama sio mzungu bado tungekuwa tuna wapoteza wakina mama wengi wakati wa kujifungua.
Baadhi ya mila bado wanaume na wanawake wanafanyiwa tohara kinyama kwa kukatwa bila ganzi tena kwa vifaa duni sana na mazingira yasiyo na majengo au usafi wa kutosha. Zamani tohara zilipoteza sana maisha ya watu kwa sababu tu ya upuuzi wa mila zinazobaki katika zama za ujima bila kubadilika na kufanyika kwa ufanisi.
Mila za mzungu zinabadilika kwa kasi kutokana na teknolojia yao pia kukua kwa kasi.
Mpaka leo watu wanalima kwa jembe la mkono wenzetu wamesha hama huko miaka mingi sana.
Huwezi kuendelea kwa kasi kama una viongozi wanaowajengea fikra za kuishi maisha magumu na kazi ngumu. Ni lazima pawe na watawala wanaohamasisha mbinu za kurahisha maisha . Bado tunagombana kwa sababu ya kutofautiana namna ya kufikiri. Wenzetu huko walishapita zamani sana.
Amini amini amini nakuambia Leo hii mzungu akigoma kuja Afrika kuangalia wanayama basi wanyama wetu watakuwa hawana faida yoyote huko porini zaidi ya kuwinda digidigi kwa ajili ya kitoweo.
Leo hii wazungu wakigoma kununua madini yetu basi yatakuwa hayana maana yoyote zaidi ya kuyayeyusha na kutengenezea hereni na pete mikononi.
Kinachomtofautisha binadamu na wanyama wengine ni teknolojia. Kama binadamu wote tungekosa teknolojia basi tungekuwa ni kama wanyama wa porini mana tulikua tumeshaasi na kupoteza hata ule uwezo wa kujikinga au nguvu zetu za asili kama uchawi na mazingaumbwe.
Mungu alimtumia mzungu na Mwarabu kurejesha ubinadamu duniani kwa kuleta teknojia ili watu wawe tofauti na wanyama.
Watu waishi kwenye nyumba na sio mapango.
Watu wavae nguo na sio majani.
Watu wapeane taarifa kupitia maandishi.
Watu wapate Elimu ili wajaze "empty minds". Bila elimu mtu anakua kama kipofu.
Mpaka leo tuna maprofessor chungu nzima lakini hawana majibu ya matatizo yetu mana uprofessor wao ni livuli cha uproffessor wa mzungu. Naam ni kivuli mana vyote vilivyoko kichwani ni ndoto za mzungu. Kuanza kufikiri mpaka kutenda ni mzungu tupu. Hakuna profesa wala mwanafunzi wake.
Ukiacha kumfuata mzungu kiteknolojia basi unajiingiza kwenye ushenzi mana utakua huna cha kujivunia pia. Mfano leo hii tukapiga marufuku :-Dini za kiislam na kikristo,matumizi ya simu, matumizi ya tv, matumizi ya namba za kwarabu na mrumi, matumizi ya computer,matumizi ya robot, matumizi ya viwanda na mashine za kushonea nguo ,matumizi ya ndege, matumizi ya mifumo ya kijeshi na kiuslama yanayotokana na mafunzo ya kizungu.
Matumizi ya saa na majira ,matumizi ya dawa na madaktari waliosoma elimu za kizungu,matumizi ya nguo zinazotokana na teknolojia ya mzungu, taarifa za hali ya hewa zinazopatikana kutokana na teknolojia ya mzungu, uvaaji wa miwani inayotokana na teknolojia ya mzungu, matumizi ya dawa za meno, Kuweka meno na viungo bandia . Nadhani tutakua hatuna tofauti na wale jamaa wa hifadhi za Udzungwa au hifadhi ya Tarangire.
Mzungu ni mzungu na mwafrika. Hawakutokea kwa bahati mbaya.
Hata ndege wa porini wanatofautiana kiuwezo na kiutendaji. Kunguru hawezi kujenga kiota kinachofanana na manyuwai japo wote ni ndege.