Nimeumizwa sana na Dr. Slaa

Nimeumizwa sana na Dr. Slaa

Joined
Jul 29, 2015
Posts
22
Reaction score
16
Taarifa niliyoisikia kutoka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA kuwa wameridhia Katibu Mkuu wetu Dr Slaa, kupumzika kwa mda usio julikana.

Kiukweli nimeumizwa na kusikitishwa kwa uamuzi huo wa Dr Slaa hasa nikikumbuka taabu na mateso aliyoyapata katika kukikuza na kukisimamia leo anaamua kuacha kwa namna alivyo amua kufanya.

Naomba nitumie fursa hii kumuomba Mh😀r Slaa fikiri mara nne ni maumivu makali kiasi gani utakuwa umeyasababisha kwa watanzania wenzako na hasa tunao kuunga mkono na kutambua umuhimu wako na mchango wako ndani ya chama cha CHADEMA na UKAWA kwa ujumla tafadhari nakuomba rejea kambini kwa masilahi ya chama na Taifa.
 
Taarifa niliyoisikia kutoka kwa Mwenyekiti wa Chadema kuwa wamelidhia KATIBU mkuu wetu Dr Slaa, kupumnzika kwa mda usio Julikana. Kiukweli nimeumizwa na kusikitishwa kwa uamuzi huo wa Dr Slaa hasa nikikumbuka taabu na mateso aliyo yapata ktk kukikuza na kukisimamia leo anaamua kuacha kwa namna alivyo amua kufanya.... Naomba nitumie fursa hii kumuomba mh😀r Slaa fikiri mara nne ni maumivu makali kiasi gani utakuwa umeyasababisha kwa watanzania wenzako na hasa tunao kuunga mkono na kutambua umhimu wako na mchango wako ndani ya chama cha CHADEMA na ukawa kwa ujumla tafadhari nakuomba lejea kambini kwa masirahi ya chama na Taifa.

ANGALIZO KWA DR SLAA NA LOWASA
Kabla sijaanza kuelezea lolote napenda kumukumbusha Slaa ambaye ana taalum ya upadri.
Katika kitabu cha matendo ya Mitume kuna ushahidi kwa Sauli alikuwa muuaji na tena alikuwa anauwa mitume lakini alipata padiliko la kweli na kujiunga na mitume wengine.

Wakati Sauli anafanya hivyo Mitume wengine walianza kumunyanyapaa na kumuogopa lakini katika bibilia , imethibitishwa kwamba hadi leo Paulo (aliyekuwa Sauli) ndiye aliyefanya kazi kuliko Mitume wote.

Bila shaka kuna watu ndani ya Chadema na hata nje ya chadema wanataka kujenga hoja ya kumunyanyapa LOWASA ati ni Fisadi , hata mimi niliingia mtego huu lakini napenda kuhojhi yafuatayo:
(1)Lowasa amehama CCM na kwa hatua hiyo ameingamiza nafsi yake kwa kiwango Kikubwa.
(2)Lowasa yupo tayari kutumia Pesa yake na mali yake kubomoa CCM
(3)LOWASA anahasira kali na CCM na miungu watu ndani ya CCM
(4)LOWASA kama waziri Mkuu mstafu ametake risk ya Kifo kiasi kwamba anataka kupiga CCM kwa Nyaraka zito za Siri ambazo Slaa hawezi kuzielezea
(5) Lowasa anajua mikakati ya Wizi wa Kura ndani ya CCM kwa miakazaidi ya 40
(6) Ndani ya CCM hawakutarajia wala hawakuwahi kupanga kuwa mtu kama Lowasa ambaye amewshijka nafasi nyeti kama waziri mkuu anaweza kuasi serikali kiasi hiki
Huu uasi unatisha na haujawahi kutokea, na hata pale ulipojaribu kutokea wahusika hawakubaki hai
(7)Kwa sasa CCM wanahaha sana juu ya Lowasa kuchukua form. Mikakati ya CCM iliielekeza Nguvu kumshambulia Slaa lakini Mungu amebadili Plan ghafla na kumuleta Lowasa amabaye hawajajipanga nan i Pigo kubwa
(8)Kwa sasa Uasi uliojitokeza CCM ni vigumu kujua nani yupo kwa nani
Angalia mtandao wa Lowasa ndani ya CCM unatisha na umetulia Kimia.
Mtandao huu jumlisha nguvu ya Umma ni lazima CCM ibaki kama KANU
MAONI KWA SLAA.
(1)Wakati unagombea urais ulikuwa na Rozi Kamili ukamwacha na kumuoa Josephine
Rozi Kamili alikubali ujio wa Josephine lakini leo Josephine huyo amekuwa kikwazo kwa maamuzi yako.
(2)Mambo ya Chama huwezi kumuhusisha Mwanamke, huo ni udhaifu mkubwa na kama kweli unamsikiliza mwanamke basi ujue hutapata nafsi ya kurudi kwenye jamii na wakakuamini na kukupa heshima kama walivyokupa.
Mke ni mshauri wake kwa mambo yote lakini kikao kama kamati kuu kinapopitisha maamuzi harafu mkeo anapinga maana yake mke huyo hafai kuwa First Lady na hata wewe hufai kuwa Kiongozi
MAONI KWA LOWASA
(1)Umeitwa Mwizi kwa siku nyingi sana na hata mimi nimekuita hivyo , sasa huu ni wakati wa wewe kutuambia mwizi halisi ni nani na utoe Ushahidi
(2) Zipo taarifa kwamba CCM wanapanga kukata jina lako kwenyenye tume ya uchaguzi hivyo nakusihii usikate tama .Muombe Mungu .Hii ni safari ya ushindi na si matumaini tena
(3)Usiogope kushambulia Ikulu kwa kuwa Mussa alikaa Ikulu ya Farao na kulelewa hapo lakini Mungu alimupa kazi ya kumuangamiza Farao.
Hivyo Lowasa umepewa kazi ya Kuingamiza CCM hivyo fanya kweli ujue kwamba Slaa hajui haya.
 
Kwa kweli pamoja na ujio wa mwamba wa kaskazini, kuleta amsha amsha, Lowassa hakutakiwa kupewa nafasi ya juu kiuongozi. kwanza hajakijenga chama. Yeye alitakiwa kuandamana na MTU ambaye angeteuliwa kugombea urais kwenye mikutano yote ya campaign.

Kwa kweli Dr upo sahihi sana kwa maamuzi yako. Naomba tuheshimu maamuzi yake.
 
Kwani hata Dr. Slaa angesimamishwa kugombea urais kupitia ukawa angeshinda? Mm nahakika asingeshinda. Nguvu alionayo Lowasa na uwingi wa wafuasi wake ni dhahiri atashinda.Dr Slaa angeungana na wapambanaji wengine kuing'oa ccm.maana nia ni kuiondoa ccm madarakani
 
Hili la Dr. Slaa hebu tuwe na subira, alichokifanya mwenyekiti ni kumruhusu apate muda wa kutafakari na kurudi katika hali yake ya kawaida ya kiharakati.. najua na nafahamu kuwa tutakuwa naye katika kampeni za kumnadi mgombea wa ukawa.. ni suala la muda tu!! Tuwe na moyo mkuu makamanda..
 
Inaskitisha na inanisononesha kwa uamuzi wako dr slaa.Hata kama umeingia kinyongo hukupaswa kuamua katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi,naomba urudi tuendelee kuiokoa nchi hii
 
Inaskitisha na inanisononesha kwa uamuzi wako dr slaa.Hata kama umeingia kinyongo hukupaswa kuamua katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi,naomba urudi tuendelee kuiokoa nchi hii

If wishes were horses Mkuu
 
Kwani hata Dr. Slaa angesimamishwa kugombea urais kupitia ukawa angeshinda? Mm nahakika asingeshinda. Nguvu alionayo Lowasa na uwingi wa wafuasi wake ni dhahiri atashinda.Dr Slaa angeungana na wapambanaji wengine kuing'oa ccm.maana nia ni kuiondoa ccm madarakani


Kwa kweli Dr. Slaa angeshindwa urais lakini sio kama Lowassa atakavyoshindwa, kwa mbinu yeyote, chafu, atakayotumia!
 
Siipendi cdm. Lkn msimamo wa dk Slaa taukumbuka daima. Huyu mtu ana sifa zote, msomi, mkongwe na mweledi wa siasa. Anajipambanua kwa kuchukia wahujumu uchumi/mafisadi. Sioni muujiza wowote wa kumkutanisha na Lowasa. Slaa hana bei ila ana principal anazoishi nazo. Utu wake uko kwenye ukweli wake. Namshauri aende CCM, CCM wamemsikia wamemwelewa na wameanza kazi ya kuwafyeka mafisadi. Slaa anajua ufisadi ni hulka, haupo ktk maandiko ya vyama. Kwa hiyo, mtu anahama na hulka na anaachana na makatazo ya maandiko!!!
 
Tawashangaa CCM kama hawatomfuata Slaa kumshawishi arudi ccm kusaidia chama kusafisha mafisadi. Slaa ni mtu muhimu sana, ccm inatakiwa isilale hadi impate dk Slaa, mpambanaji wa kweli wa mafisadi.
 
Tawashangaa CCM kama hawatomfuata Slaa kumshawishi arudi ccm kusaidia chama kusafisha mafisadi. Slaa ni mtu muhimu sana, ccm inatakiwa isilale hadi impate dk Slaa, mpambanaji wa kweli wa mafisadi.

Umenena vyema
 
Kwa kweli pamoja na ujio wa mwamba wa kaskazini, kuleta amsha amsha, Lowassa hakutakiwa kupewa nafasi ya juu kiuongozi. kwanza hajakijenga chama. Yeye alitakiwa kuandamana na MTU ambaye angeteuliwa kugombea urais kwenye mikutano yote ya campaign.

Kwa kweli Dr upo sahihi sana kwa maamuzi yako. Naomba tuheshimu maamuzi yake.

hiyo ndio ilikuwa hoja ya Slaa lkn akaambiwa yeye sio altimatum na kama hataki aondoke Chamani-dharau na dhihaka
 
Back
Top Bottom