Nimeumizwa na tukio hili

Nimeumizwa na tukio hili

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
42,566
Reaction score
105,395
Salam kwenu wana jamvi.

Mtanivumilia kwa urefu wa habari hii.

Niliwahi kuwa kwenye mahusiano na mdada ambae alikua na mtoto mmoja, huku nami nilikuwa na watoto wawili (mapacha). Wakati wote wa mahusiano wetu tulikubaliana kuwapeleka watoto wetu wakasome kwenye shule moja na niliamua kua namlipia ada pia kama wanangu.

Na wakati wote wa mahusiano yetu tulikua tukiishi mbali mbali nikimaanisha kila mmoja akiwa nyumbani kwake.

Shida ilikuja baada ya kuhisi ninachepuka na mdada mwingine hali iliopelekea kutofautiana na kuvunja mahusiano yetu kabisa. Baada ya muda x-wangu alipata mc
humba na pasipo kuchelewa jamaa akamuoa na maisha yakaendelea.

Matatizo yalianza pale mume wa x-wangu alipogundua kua namlipia ada mtoto wa mke wake na kipindi cha likizo ya watoto waliporudi toka shule, yule mtoto wa x-wangu aligoma kwenda kwa mama yake na alikatalia kubaki nyumbani kwangu kwakua walikua tayari wamezoeana na watoto wangu, huku wakimuita dada kwani alikua amewazidi umri.

Hali hii ilianza kuleta mgogoro kwenye ndoa ya x- wangu hadi kupelekea yule jamaa kuanza kutoa maneno ya vitisho kwangu. Na wakati haya yakitokea kuhusu migogoro mimi sikuwepo Tanzania, zaidi nilikua nikipata taarifa kutoka kwa watu wa karibu.

Niliona isiwe tabu, nikaamua nimtext x- wangu kwamba nikirudi likizo nitamtoa mtoto wake shuleni na nitamrudisha kwake maana sihitaji wema uniponze.

Kipindi niliporudi likizo nilifanya taratibu zote na nikamfuata mtoto shuleni na nikaenda kumkabidhi kwa wazazi wa x, mbele ya mjumbe, x na mumewe na wazazi wa x. Pia niliomba tukabidhiane kwenye maandishi kwa sababu ya kujiweka upande salama.

Cha kushangaza mtoto yule (binti) alilia sana na huku aking'ang'ania kwamba nisimuache, hakika mtoto yule alilia hadi wote tukajiskia huzuni kubwa. Ilibidi nimdanganye mtoto kwamba nitamfuata baada ya kuwasalimia bibi na babu yake.

Siku ya tatu sasa imepita, naambiwa binti (mtoto) yule amefariki dunia kwa kujirusha kwenye kisima cha maji.

HAKIKA NIMEUMIZWA SANA NA TUKIO HILI
 
ushiboy

Duh pole sana mpendwa kwa yaliyokukuta. Kitu kimoja usijilaumu kwa haikuwa sababu ni wewe , kama hayo mema uliyoyafanya kwa marehemu Mtoto yule , hakika Mungu hatokuacha. Hebu naomba uombe mungu akupe Amani moyoni ili , uondokane na na mzigo uliojiweka nao moyoni ambao unaweza kukutia dhambini. My dear tafuta nafasi moyoni mwako ujisamehe na kuamini haikuwa wewe ndio chanzo chs yule Mtoto kufariki. Mungu akutie nguvu katika kipindi hichi kigumu . Asante !
 
Last edited by a moderator:
Dah pole sana!! Mitihani katika dunia tumeumbiwa wanadam!! Hakika wema hauozi na nakusifu sana kwa moyo wako kumlea mtoto wa mtu kama wako had akakupenda kias hicho n.ngumu sana dunia hii ya sasa. Bas mungu hulipa kila tulifanyalo hapa hapa duniani na utalipwa kwa njia yoyote ile malipo ya wema wako. Hiv ina mana huyo mwanamke alishindwa kumconvice mumewe kua hakuna mapenz bali n.mtoto tu umejitolea kumlea??? Wanawake wengine bana...kitendo cha mtoto kulia na kukutaka mbele za macho yao tayar ilikua n prove kua unamlea vizur....mungu amueke pema pepon malaika huyo!!
 
Duh! Pole sana mkuu. Lakini dhamira yako inakuweka huru na lawama zote hizo. Kimsingi wewe huna kosa lolote. Wakujilaumu zaidi ni huyo mume wa X wako
 
Dah pole sana!! Mitihani katika dunia tumeumbiwa wanadam!! Hakika wema hauozi na nakusifu sana kwa moyo wako kumlea mtoto wa mtu kama wako had akakupenda kias hicho n.ngumu sana dunia hii ya sasa. Bas mungu hulipa kila tulifanyalo hapa hapa duniani na utalipwa kwa njia yoyote ile malipo ya wema wako. Hiv ina mana huyo mwanamke alishindwa kumconvice mumewe kua hakuna mapenz bali n.mtoto tu umejitolea kumlea??? Wanawake wengine bana...kitendo cha mtoto kulia na kukutaka mbele za macho yao tayar ilikua n prove kua unamlea vizur....mungu amueke pema pepon malaika huyo!!

Nahisi walikua na migogoro ya hapa na pale kuhusiana na swala zima la mtoto (marehem)
Pia kunakipinda niliwahi kupata taarifa kwamba jamaa alikua akimtuhumu mkewe kwamba haiwezekani asomeshewe mtoto bure, pengine alihisi kuna kitu au mahusiano yanaendelea
 
Duh pole sana mpendwa kwa yaliyokukuta. Kitu kimoja usijilaumu kwa haikuwa sababu ni wewe , kama hayo mema uliyoyafanya kwa marehemu Mtoto yule , hakika Mungu hatokuacha. Hebu naomba uombe mungu akupe Amani moyoni ili , uondokane na na mzigo uliojiweka nao moyoni ambao unaweza kukutia dhambini. My dear tafuta nafasi moyoni mwako ujisamehe na kuamini haikuwa wewe ndio chanzo chs yule Mtoto kufariki. Mungu akutie nguvu katika kipindi hichi kigumu . Asante !

Amen....
Lakini nawaza hapa, nini nitawaeleza watoto wangu kuhusu kifo cha dada yao!?
 
Nahisi walikua na migogoro ya hapa na pale kuhusiana na swala zima la mtoto (marehem)
Pia kunakipinda niliwahi kupata taarifa kwamba jamaa alikua akimtuhumu mkewe kwamba haiwezekani asomeshewe mtoto bure, pengine alihisi kuna kitu au mahusiano yanaendelea

Asee kwa kitendo alichofanya huyo mtoto huyo mumewe atajutia maisha yake yote maana yeye ndo source
 
haya mambo ya x-ni sawa na sakata la ESIKROOOO....

YOHANA 2:13-17 "..wivu wa nyumba yako hakika utanila".....Eeeee mola tusameheee kwa hili
 
Dah pole sana ushiboy Hakika nimesikitika na nimeumia sana kiukweli wewe huna lolote la kujibu mbele za mungu (tambua hili ili uwe huru) kwa kuwa hukufanya hivyo kwa matakwa yako.Hongera kwani wenye roho km yako ni 1/100.
 
Last edited by a moderator:
pole sana mkuu! laiti usingechepuka yote haya yasingetokea!ungeendelea kuwa na mama yake hivyo huyo mwanaume asingemuoa mama yake! kuhusu huyo mume kuja juu kwa mtoto kulipiwa ada na wewe ex wa mke wake,alikuwa sahihi kabisa.
 
funguka mkuu.., alikuhisi au ULICHEPUKA?na kama ndivyo...,mhh pole bos...LIMEKUGANDA....you are guilty till is proved otherwise....MCHEPUKO noma baki NJIA KUU..
 
Back
Top Bottom