puker
JF-Expert Member
- Nov 22, 2018
- 1,054
- 2,179
Habar za muda huu wadau wote wa JF.
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada. Hakuna asiefahamu janga linaloendelea kipindi hichi duniani kote, juu ya ugonjwa huu hatar wa Corona" unaoambukizwa na virusi vijulikanavyo kama COVID 19.
Sasa katika kupambana na virusi vya ugonjwa huu, zipo hatua kadhaa tunazoshauriwa kuzichukua ili kuepuka maambukizi, ikiwemo kunawa maji na vitakatisha mikono maarufu kama Handsanitezer lakini pia kuvaa mask (barakoa) pale unapokuwa katika mikusanyiko...hususani sisi tuishio Dsm barakoa imekuwa kama sheria (siyombaya) kufuatia na tamko kutoka kwa Mh. Mkuu wa Mkoa Poul Makonda.
Sasa binafsi baada ya kuanza kuvaa hizi mask (barakoa) naona kunatatizo lingine limejitokeza katika mwili wangu hali ya kuwa sikuwa na hili tatizo hapo kabla. Nina kama siku ya nne (4) leo...sihisi harufu kabisa katika pua zangu.
Na sina kabisa mafua hata dalili za mafua pengine labda ingeweza kuwa chanzo cha tatizo kama ilivyozoeleka. Sasa lengo kuja hapa kitaaalamu imeakaaje, maana ni hatari sana kama litakuwa ni tatizo la kudumu.
Nimehisi tatizo limesababishwa na kuvaa barakoa kwa sababu mara tu nilipoanza kutumia nimeahisi kuhisi tofauti hiyo.
Naombeni ushauri ndugu zangu.
Natanguliza shukrani.
Sent using Jamii Forums mobile app