Nimetokea kuchukia ndoa

Nimetokea kuchukia ndoa

Muoneshe hiyo video kaka yako alafu ataamua mwenyewe aendelee na mkewe au amuache
Japo pia kama siiamini sana story yako naona kama umetunga hivi
 
Uko sahihi kabisa mkuu
Wakati mwingine unapenda hasa! Na pia mwanamke anajifunza kupenda hata akiwa ndani ya ndoa ndiyo maana wanawake wa zanani walikuwa wakichaguliwa wachumba.

Hili tatizo limesababishwa na wanaume wenyewe wengi ingawa wameoa lakini kama hawajaoa tu wana wanawake telee,mke akishajua upendo wote hupotea wanabakia kuishi tu kulea watoto..
Wanaume muelewe pesa haiwezi kununua upendo,pamoja na kuhudumia famila kila kitu kama unamvunja moyo mkeo hutaona raha ya hiyo pesa,utabakia kusema tu nampa kila kitu lakini wapi....
Ukiona mkeo amebadilika muulize shida iko wapi mama mbona umebadilika kwa upole tu utajibiwa!
 
mkuu umekuwa mshauri wa ndoa ila inaelekea kunabaadhi ya mambo hujapata kuyafahamu kwa kina hasa hayo yahusuyo kitanda,
Mkuu sishauri mtu kuchepuka hata siku moja ila kunasababu nyingi sana ambazo zifanyazo watu kutoka nje ya ndoa bahati mbaya iliyoje nyingi zinazuilika na kuepukika, unajua mtu akiwa hafikishwi hata kama anapewa kilakitu huwa haisaidii maana unakuta huyo muuza genge anamfikisha japo hampi kitu
Pia mtu akiwa anapata karibu vyote atakavyo ndivyo hamu ya mapenzi inashika hatamu tofauti na mtu mwenye msongo wa kukosa mambo muhimu ya maisha na asiye na uhakika wa tonge lake.

Kikubwa wanandoa wajifunze kuongea pamoja tena mambo ya chumbani wazungumze kwa uwazi pasipo kuoneana aibu, yani nakuhitaji leo nikitoka kazini kwahiyo jiandae mke/mme wangu, pia ka mtu hajafika aseme pasipo kuogopa ataonekanaje, pia watu wajenge afya zao ziweze kushiriki tendo kwa ufasaha pasipo tabu na kuchoka mapema pasipo kumtosheleza mwenza, watu wakiwa na utamaduni huu itapunguza na kumaliza kabisa, matatizo ya kiafya siwezi yazungumzia sana maana yale yanakuwa nje ya uwezo wa mtu.

Tuthamini vitanda vyetu na tuwe na mapenzi kwa wenza wetu maana hata ikitokea unatatizo la kiafya ukiwa karibu na mwenza wako hata hamu ya kutoka nnje inapotea.
 
Wewe ni mgumu kuelewa au unalazimisha tu mambo?

Ndoa nyingi za sasa hivi mgogoro mkubwa ni uchepukaji,na asilimia kubwa ni wanaume kuchepuka kwao ndiyo kunapelekea wake zao nao kuchepuka,siyo kila ndoa lazima iwe hivyo...

Huyu mleta mada aseme kama anamfahamu jamaa yake vizuri,je si mchepukaji? Maana unaweza kuta mleta mada anachoshangaa kuona mwanamke anapewa kila kitu mpaka biashara halafu anachepuka,ndiyo maana nikasema wanaume muelewe mapenzi siyo pesa! Siyo sababu mtu anakula,anavaa nk then urudi home saa6 na kuendelea ingia toka kila siku ....

Hivi kwanini mwanamke akichepuka mnaumia sana? Mnajiuliza kama hamuwezi kazi,hamtutoshelezi nk, mlishawahi kujiuliza nasi tunawaza nini mkichepuka ? Tunawaza hamtupendi upendo umeshaisha,ndiyo sababu umetafuta mbadala...mnaambiana mchepuke kwa akili mke asijue,mnajua akijua hakuna ndoa tena.....hata kama utasemehewa lakini upendo hakuna tena!
Yaani unaandika upuuzi ule ule tu tangu kwenye comment yako ya kwanza, halafu unasema sijakuelewa kuna kipi cha kushundwa kuelewa hapa kwenye hizi bandiko zako? Si unazunguka pale pale tu eti mwanamke kuchepuka most likely chanzo ni mwanaume na blah... blah.

Mimi nimekujibu vizuri kabisa kama wanawake mnaona dawa ya mwanaume anayechepuka dawa ni kuchepuka na wewe basi hamfai kuolewa msikimbilie ndoa.. Endeleeni kuchakazwa tu na vijana na kulea watoto kama single parents basi.

Sasa wewe huko hapa unashupaza shingo kutetea uchepukaji wa wanawake tena kwa back up argument za kipuuuuuziiii!! Ambazo hata mtoto mdogo hazimuingii akilini.

Zipo njia sahihi za kukabiliana na mume mchepukaji lakini sio hiyo unayotetea hapa! Halafu kwanza mwanamke akishachepuka na yeye ndio inamfanya mume aache kuchepuka au?

Hivi unafahamu kwanza hata athari za uchepukaji baina ya mwanaume na mwanamke hazilingani hata kidogo?

Unajua ni kwanini jamii za kale zilizokuwa na utawala wa kifalme, mfalme alipochepuka hakuchukuliwa hatua yoyote ile lakini malikia alipochepuka alihukumiwa adhabu ya kifo mara moja?

Dada haya mawazo yako ni ya kitupa chooni
 
Lizarazu ni mgumu sana kuelewa...

Sitetei wachepukaji ila wengi wanachepuka kwa sababu hiyo, siyo kila mwanamke lazima achepuke sababu mume wake anachepuka!

Naona wewe ndiyo unatetea sasa uchepukaji kwa wanaume!

Siyo wewe uchepuke mwenzio akichepuka kosa! Kama huwezi kuheshimu ndoa yako kwa uchepukaji usioe full stop!
 
Habari wana JamiiForums

Ni ukweli usiopingika kuwa toka nijiunge na jamii forum nimekuwa siyo mchangiaji mkubwa sana kwenye masuala mazima yanayohusu mahusiano hasa kwenye upande wetu wa akina dada.

Kiupande wangu siyo mpenzi sana wa kina dada lakini nilikuwa ni mtu mwenye ndoto ya kuja kuwa na familia bora.Busara zangu na muonekano na hata tabia vimenifanya niwe mwenye kutoa ushauri kwa watu wazima na hata vijana wenzangu,hali hiyo imenipelekea jirani yangu ambae ni 40 years now,kuwa rafiki yangu na hata mshauri wake mkuu.

Ni tokea mwaka 2016 alikuwa akisumbuliwa mno na ndoa yake naweza kudiriki kusema kuwa ni mimi ndio niliyekuwa sababu ya ndoa hiyo kuendelea kutokana na ushauri nlokuwa nampa ambao ulikuwa unafanya kazi lakini mwisho wa siku wanavurugana tena.Mke wa jamaa ni mfanyabiashara na jamaa ni mfanyakazi wa benki fulani hapa Dar hivyo mkewe amefunguliwa biashara zaidi ya 3 na pia wamefanikiwa kuzaa watoto 3.

Maisha yao naweza kusema ni mazuri sababu wana uhakika wa kula wananyumba nyingi tu hapa Dar na hata magari zaidi ya ma 4 ya kutembelea,nimekuwa nikisuluhisha ugomvi wao hasa sababu ya watoto walio nao na pia mali walizonazo kwani zinaweza kuleta uadui mkubwa.

Lengo la kuyaleta haya ni baada ya siku ya leo asubuhi kwenda kumtembelea ndugu yangu na kumkuta mkewe akiwa barazani uchi wa mnyama akifanya mapenzi na muuza genge wa hapa mtaani kwetu,Hakika nilijikuta tu ninatetemeka kwa hasira nilichokifanya ni kuwapiga picha na kuondoka zangu,hivi hapa nipo tu mjini kichwa kinanizunguka ameshanipigia simu zaidi ya 100 lakini sipokei nadhani nahitaji muda wa kufikiri ili nifanye uamuzi eitha ni mpe tu ukweli mmewe au ninyamanze

Swali langu kwa akina dada ni kitu gani kinawafanya siku hizi muwe mnachepuka kiasi hiki,wakati mnapewa kila kitu ndani ya ndoa hakika mmenifanya niichukie ndoa.
vipi we umeoa, na kwanini jwe msuluhishi wao, na stori za eti wako barazani wakifanya yao we ulienda kufuata nn huko mida hiyo....... ni maswahi tu kikulacho ki nguoni
 
Lizarazu ni mgumu sana kuelewa...

Sitetei wachepukaji ila wengi wanachepuka kwa sababu hiyo, siyo kila mwanamke lazima achepuke sababu mume wake anachepuka!

Naona wewe ndiyo unatetea sasa uchepukaji kwa wanaume!

Siyo wewe uchepuke mwenzio akichepuka kosa! Kama huwezi kuheshimu ndoa yako kwa uchepukaji usioe full stop!
Ni kosa kubwa sana kwa mwanamke aliyeolewa kuchepuka, kwa jamii iliyostaharabika adhabu yake ni kifo.
 
umetukanwa wapi....we pumbafu sana...katafute kazi ya kufanya......mwanaume kamili hana tabia kama zako....eti na picha nimepiga..kapigie punyeto....iblisi wewe...wachana na ndoa za watu....
Mkuu mbona umekuwa mkali sana ndo wewe nini!
 
Coaches don't play,thats how i answer my friends when they ask me why I give relationship advice but am single.
 
Coaches don't play,thats how i answer my friends when they ask me why I give relationship advice but am single.
 
Back
Top Bottom