Nimetoka kusuluhisha ugomvi mkubwa wa Mdogo wangu na mke wake

Mirungi huaribu sana nguvu za uume, wakati mwingine ktk hii dunia si kila kitu ni cha faida na chakuigwa.

Ona sasa Mke mwema kabisa anakosa Mume sahihi na kuachwa njia panda.

Mungu ni mwema sana kuniepusha na ulevi wowote wa sigara, bangi, kokein, shisha, pombe, pornography na uzinzi wa Wanawake na hata hii mitandao ya kijamii.
Pombe muhimu acha ubwege
 
Kuna rafiki yangu aliolewa na msomali tabia ni Kama za huyo dogo

Wametengana kwa shari sana mwaka jana

Kumbe veve haifai aisee
Veve tatizo lake kubwa ni gharama tu. Yenyewe inauzwa bei ghali na pia inahitaji machanjio. Yani ukishanunua hujamaliza kuna vitu vingine lazima ununue ili vikuwezeshe kuchanja.

Kuhusu suala la kupunguza uwezo wa 6x6 nimesikia pia japo kuna wengine wanasema sio kweli.
 
Alijua kuoa ni kuja kupikiwa tu, akasahau kuwa akishiba anatakiwa apige show ya kibabe sio kulala kama nyau aliyeshiba maziwa
 
Mmeondoka bila kutatua tatizo lililowaleta! Mlitakiwa dogo mumpeleke hospitali ya serikali kwenye tiba ya mateja.
Pia kaka ungebaki nyumbani pao kumhamasisha dogo arudishe hamu asikiapo chaga za kitanda zikilia ukimgegeda shemeji yako, tiba hii ingemponya haraka sana kuliko maombezi.
hakuna hosptikali ya mateja ni sober apelekwe pia acha dharau jina teja suo zuri sema waraibu ! endelea kuita mateja mpk siku mtu wakaribu akitumbikia huko ndo utajua
 
Maisha haya nimeshuhudia Tanga, vijana wameharibika sana na hizo mirungi...

Mtu anakwambia hana hamu ya mwanamke kabisa....

Nina jamaa yangu sasa ni marehem, alishindwa kuacha hizo mambo, mwishoe alikuja kufa kwa wizi baada ya kukosa ela ya mirungi na kuanza kuiba...

Walimuua pale kwa Michi...
Rest in peace
 
Back
Top Bottom