nimetoa kwa kitine

nimetoa kwa kitine

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,650
Reaction score
21,014
Jamaa mmoja kwa muda mrefu alikuwa anamfukuzia binti mmoja mrembo na kila mara alikuwa anatolewa nje na yule binti kwa visingizio mbalimbali, hatimae siku moja wakati yumo kwenye taxi mitaa ya Tandale, mesej ikaingia ilikuwa inatoka kwa yule binti mrembo imeandikwa hivi, 'Kwa kweli sasa nimeamini unanipenda kweli, maana ni muda sasa umeonyesha nia ya kuwa nami bila kuchoka. Naomba uje kwangu jioni ya leo, je nikutegemee?'. Jamaa kwa furaha kubwa akajibu, "Ndiyo'. Kabla hajaminya send kibaka mmoja akaipitia ile simu kama mwewe. Jamaa akabaki kupiga kelele, 'Minya send, minya send"
 
Manesi wengine noma, jamaa alienda hospitali kumuona dokta. Akamuendea nesi aliyekuwa akipokea wageni ambao walikuwa wengi wamejazana kwenye mabenchi wanasubiri huduma; JAMAA: Samahani naomba kumuona dokta anishauri dawa, nimefanyiwa vipimo hivi hapa...akampa nesi karatasi, nesi akasoma kile kikaratasi NESI: ( Kwa sauti kubwa) He kumbe una ugonjwa wa zinaa JAMAA: (Nae kwa sauti) Ndio, dokta alinambia na wewe ugonjwa huu ulikusumbua kwa muda mrefu sana
 
MUME: Mke wangu, niwe mkweli pamoja na kuwa kwa sasa tuna watoto sita mimi bado nakupenda sana. Na hakuna kitu kitakachoweza kunifanya niache kukupenda, I love you honey. Nina swali moja tu, huyu mtoto wa nne mbona yuko tofauti na hawa wenzie sita, mkorofi, sura mbaya, shule hataki, yaani tabu tupu? Mke wangu nambie tu kama ana baba tofauti na wenzie, ukweli hautabadili mapenzi yangu kwako.
MKE🙁Huku akipiga magoti) Mume wangu najisikia vibaya naomba unisamehe ni kweli huyo mtoto baba yake ni tofauti na wenzie
MUME: (Machozi yakimlengalenga) Dah mke wangu... baba yake ni nani?
MKE: Baba yake ni wewe.​
 
DOGO 1: Mi babangu anaweza kula sufuria nzima ya ugali
DOGO 2: Mi babangu anaweza kula kuku mzima peke yake
DOGO 3: Mi baba yangu anaweza kula taa
DOGO 2: Mwongo wewe anakulaje taa?
DOGO 3: Kila siku namsikia anamwambia mama, 'ZIMA TAA TULE"​
 
Majambazi yaliingia katika nyumba moja kuiba. Mwenye nyumba akaamka na kwa ujasiri mkubwa akachukua bunduki ya kuchezea ya mwanae na kuwatisha majambazi wenyewe wakawa wapole, akawaketisha chini, na kuanza kupigia simu polisi. Wakati mzee anaita polisi huku akiwalenga majambazi kwa ile pisto ambayo wao walidhani ni ya kweli, mtoto wa mwenye nyumba akaamka;
DOGO: Baba nataka kwenda chooni
BABA: Nenda tu mi nimewakamata hawa wezi nangojea polisi waje
DOGO: Haoooo mikubwa mizima mnaogopa binduki yangu ya kuchezea......baba mkojo ukamtoka ghafla
 
1601140_724667687553159_797562362_n.jpg
 
DOGO: Mama hivi binadamu walitokea wapi?
MAMA: Kwanza kulikuweko na Adam na Hawa. Hawa ndio walikuwa wazazi wa kwanza wa binadamu, wakazaa watoto na watoto wao wakazaa ndio mpaka dunia ikajaa. (Dogo akaenda kwa baba yake)
DOGO: Baba hivi binadamu wametokea wapi?
BABA: Hapo zamani binadamu walikuwa nyani, wakabadilika taratibu na kuwa binadamu (Dogo akarudi kwa mama)
DOGO: Mama umenidanganya, baba amesema binadamu walikuwa nyani zamani
MAMA: Sijakudanganya, baba yako alikuwa anakuelezea historia ya ukoo wake
 
DOKTA: Binti we wamoto sana
BINTI: Teh teh teh kweli dokta wanaume wengi huwa wananambia hivyo
DOKTA: Acha ujinga nina maana we wa moto nadhani una homa ​
 
INBOX YA MDADA:
1. I luv u dear (JUMA).

2.Nikutoe out leo? (John)
3..Huwa inaniuma sana nikikuona na wanaume wengine (Mwambi)
4.. Sweetie usisahau trip ya Bagamoyo, unambie nikupitie wapi (MD)
5..Darling, have you seen d credit I sent u?
(Mboss 1)
6..Honey najitahidi kukamilisha taratibu za kuleta posa nakupenda sana (Evans)
7. Hilo jione kama umeshapata(Mheshimiwa 2)
8..Baby, check akaunti yako nimekuwekea kitu (Chairman)

INBOX YA MKAKA:

1..Salio lako halitoshi kukamilisha ombi lako (TIGO)
2..Ukinitumia txt nyingine namwambia rafiki yako (Jane)
3.Mwanaume gani unashindwa kutoa msaada (Patricia)
4..Unajifanya hupokei simu lakini wiki hii ni ya mwisho lipa kodi au utoke kwenye nyumba yangu(Baba mwenye nyumba)
5..Kaka nakutegemea ada (Jaki)
6..Mwanangu njaa inatuuwa usitusahau, Mungu akubariki(Mama)
7..Sijaziona siku zangu , napenda ujue hilo (Jirani House girl)
 
JIRANI: Oyaa ndugu yangu uwe unafunga pazia usiku jana nimekuona na wife wako mkiwa faraga.
JAMAA: Hahahahaha unachekesha sana, ukiitwa mbeya utakataa? we uliniona mimi jana? Jana mimi nilikuwa safarini Moro bwana, mke wangu alikuwa peke yake, acha hizooo
​
 
Akina mama wawili waliosoma pamoja walikutana sokoni baada ya salamu;
ISABELA: Jamani Adela vipi mwanao?
ADELA: Kwa kweli mwanangu kaoa mwanamke mchawi, kamloga kamuinamisha mwanangu, we fikiria, mwanamke anaamka saa 5, akiamka hapo ni kuzurula mji mzima kutumia pesa za mwanangu, mwanangu akirudi kachoka jioni, hakuti chakula, badala yake hao wanaenda kula kwenye mahoteli ya gharama, yaani we acha tu. Vipi binti yako?
ISABELA: Mtoto wangu kaolewa na mwanaume mtaratibu sana, na mpole sana, anaamka alfajiri anamtengenezea binti yangu chai anamletea chumbani, anamuachia pesa nyingi za kutumia kwenda kununua anachotaka, kila siku akirudi anampeleka kula kwenye hoteli za gharama maisha yao kwa kweli mazuri sana
 
ha ha ha ha nimecheka sana ya hyo mshikaji aliyeibiwa simu...khaaa
 
Back
Top Bottom