Nimetoa boko wakuu

Nimetoa boko wakuu

Kazi na Dawa
Poleni sana na janga linalowakumba TZ kitalaamu likiitwa changamoto ya upumuiji.

Katika pitapita zangu kwenye majukwaa pendwa MMU na CHIT CHAT ili kutumiza yale yote anayonituma ibilisi nikakutana na ID moja ya mlimbwendwe, malikia, mremboo mmoja hatarii sana(ukiwa legendary na mkali wa hizi kazi unaweza kuisoma id na kuijua hii kazi ya maana au hii kazi ni ya kiwango cha kawaida).

Baada ya kuvutiwa na mwandiko wa bidada na kujiridhisha kua hii ni chombo ya fundi nikazama pm kwa kasi ya ajabu mnoo, baada ya kuchat chat kidogo nikataka kukihamisha chombo sasa kutoka kwenye server za melo nikipeleke kwenye server za Mark Zuckerberg.

Kumbe mrembo ananichora tu ni ex wangu wa humu kwa id nyingine wakuuu, halafu id zote ni za mda mrefu wala huwezi kizisuspect pamoja na mimi kua ni mtu mwenye intelejensia kali kwenye jamuhuri ya serekali ya watu wa mmu na chit chat, baada ya kujiridhisha na vichat chat kadhaa nikaomba contact nashanga ujumbe unarudi.

"Namba zangu za nini tena wakati unazo?" Mara paap inakuja nyingine "wee umalaya utakuua mimi M"
Baharia nikaumbuka pale lakini kama mnavyojua malegendary huwa hatushindwi nikareact fasta.

"Nilihisi ni wewe lakini nilitaka kujiaminisha let us pretend kama hatujawahi kukutana, naomba nikutoe out for dinner leo mrembo" baada ya dk kadhaa likarudi jibu

"Call me"

Na kiporo kikapashwa motoo...... mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom