Nimethibitisha ni kweli mke wangu kanisaliti

Nimethibitisha ni kweli mke wangu kanisaliti

Sijaoa lakini imenitouch as if nimegongewa mimi.., pole sana brother, unahitaji hekima za hali ya juu kutanzua hili. It's much better ungekuwa unajua chanzo cha yy kuacha njia kuu ungejua cha kuffixx. Mungu akutangulie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu lakini hawa watu huwa wanajikwaa kwenye vitu vya ajabu sana ni kumuomba Mungu na kuwaombea wake zetu kila siku maana kadri mnavyopendana na ibirisi anatafuta njia ya kuwavuruga.
Ushauri wangu:-
1) Usimshirikishe mtu yoyote anaekufahamu wewe wala kumfahamu mkeo iwe ni ndugu ama rafiki
2)baada ya hapo kaaa wewe pekeyako relax bila kuwa na mawazo juu ya hili jambo jitahidi sana hapa then usikilize moyo wako unasemaje juu ya jambo hili bila kushurutishwa na kitu chochote.kama moyo unakutuma kusamehe samehe na wala usiwe na kinyongo na mkeo na pia kama haukutumi kusamehe usikurupuke kuwashirikisha watu wengi jaribu kuongea na watu wa karibu pia wawe watu wazima wenye busara.
3) kama ukiamua kusamehe ongea na mkeo kwa lugha ya kirafiki sana asigombane sana na yule jamaa amuombe siku wakutane akijifanya kama anamaongezi nae ili achukue simu ya yule mtu afute picha zake alizomtumia.
4) kama umeamua kusamehe kaa na mkeo uongee nae kwa lugha nzuri akwambie sababu ya yy kufanya hivyo naamini kama ni mwanamke mwenye akili na mwelewa atakuelewa kama utaongea nae kwa ukarimu.
Ni hayo tu yangu ila kumbuka hawa wenzetu ni dhaifu sana na pia kila binadamu ni mkosaji yatupasa kumuomba sana Mungu atuepushe kila aina ya majaribu lakini pia tujitahidi kuwa wanyenyekevu,upendo,huruma na ukarimu kwa wake zetu kwani waweza kuta jamaa kampata kwa kitu kidogo sana.
Pole sana ndugu na Mungu akuongoze katika kufanya maamuzi.All the best



Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
 
It pains...inauma sana...mtu acheze na kitu kingine lakini siyo sekta ya mahusiano hasa NDOA.
MY ADVICE: TULIA kwanza uwe unajaribu kutafakari.
Pia,hiyo hoja ipotezee kwa muda ili kichwa kipoe then utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanya maamuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
'mwanamke mpumbavu huvunja nyumba yake mwenyew" na huku kuna wanaume wapumbavu kama 78% hivi!sasa nan mpumbavu kama si nyie!

mara sijui heri kukaa kwenye kona ya dari kuliko kuishi na mwanamke mwenye maneno mengi!
unafanya fauls daily unataka nisiseme! upo km mvulana wa 3rd/2nd yr!hujitambui kama umeoa!upo upo tu company za kijinga jinga tu!tukiamua kusema mnasema tuna maneno!shindweni
Ni kweli, mwanamke mpumbavu ataisambaratisha nyumba yake mwenyewe. Si kweli biblia inamlalia mwanamke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,

Huyu mwanamke nipo naye kwenye ndoa for 5yrs sasa na tuna mtoto mmoja.
Kwa kipindi chote nilichokaa naye kuna mambo mazuri ambayo ninajivunia kutoka kwake. Ni mwanamke mwenye vission.

Kwanza ananijali kwa kila hali hasa katika vipindi vigumu kimaisha pili sio mvivu ni mchapa kazi. Ni mwepesi kunisamehe hata na kuniomba msamaha kwa makosa niliyomfanya mimi.

Sasa huwa hanaga tabia za kuwa na wanaume alikuwa mwaminifu kiwango cha kutokumtilia mashaka kabisa. Nilithubutu hata kujisifu kuwa nina mke mwaminifu kwa kipindi chote.

Sasa juzi hapa nilianza kutilia mashaka nyendo zake maana kuna namna alibadilika nikaanza kumfatilia maana alikuwa hakai mbali na simu yake wakati sio kawaida yake.

Juzi kati hapa simu yake ikawa inamsumbua akanipa ni msaidie kuiset si ndio nikaingia inbox, huko nikakutana na SMS za jamaa anamtongoza wife ila wife akawa anamchomolea ila jamaa akawa anang'ang'ania japo inaonyesha jamaa anajua kuwa kaolewa maana wife alimwambia kuwa kaolewa.

Nikaona nisikae kimya nikamchana live kuhusu jamaa, akasema ni kweli jamaa anamtongoza lakini hawezi mkubalia basi nikamchimba biti mbaya na kumwambia akate mawasiliano nae.

Baada ya wiki nikahisi wife huenda bado ana mawasiliano na jamaa nikamuuliza akakataa ila moyo wangu ukawa bado una wasiwasi.

Ili kuilinda ndoa yangu na future ya mtoto wetu nikaamua kuhack WhatsApp ya wife kwa kutumia whatsapp web.

Hapo ndio nilipojuta hata kwanini nime-ihack WhatsApp yake siku ya pili tu baada ya ku ihack nikaona wana-chat live. Na wanatumiana picha, kilichoniuma zaidi ni pale wife alipokuwa anamtumia jamaa picha za nusu uchi.

Roho ilinipasuka kidogo nidondoke ukijumlisha na msg walizokuwa wanatumiana na ilikuwa kila akituma msg ikifika tu anazifuta chap na picha pia nilichofanya nikawa na screen shot mapema kabla hajafuta.

Kufika home nikamuuliza wife akakana baada ya kumzibua na kumwonyesha zile screen shot ndio akakubali.

Nilichokuja kugundua kumbe wife alishaamua kumzawadia jamaa penzi tena cha kusikitisha zaidi kuwa alimpa penzi ile siku ya pili baada ya kutoka kumuonya.

Yaani nimemkataza yeye ndio akaenda kufanya kweli. Ukiangalia wife hamna alichokosa kwangu tunaishi maisha safi anapata kila anachohitaji. Na 6×6 huwa na mkaza mpaka yeye nwenyewe anaridhika na hakuna siku nimemkaza asifike kilimanjaro na huwa ananisifugi sana sekta hiyo.

Wakuu naombeni ushauri wenu maana nimechanganyikiwa. Mpaka sasa nimeshindwa kutoa maamuzi nifanyaje.

Ninachoogopa zaidi ni itakuwaje jamaa akiamua kuzisambaza hizo picha!
Nimeogopa hata kulifikisha kwa ndugu zangu maana naona itakuwa ni fedheha.

Sina wa kunishauri marafiki zangu pia siwaamini sana hapa JamiiForums nimeona ndio kimbilio langu pekee.

Wife nilimfungulia biashara ila nimeifunga kwa muda kwanza.

Naombeni ushauri na sio matusi

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nani alikuambia mwanamke shida yake ni kukazwa hadi anaridhika? Anayewajua hawa viumbe ni Mungu pekee. Usiwawazie lolote maana hawaeleweki. Cha msingi kama mwanaume hakuna haja ya wazazi, washenga, mlikutana wawili mkatongozana mkaoana. Sijajua mlikuwa mmeweka makubaliano gani iwapo hayo yatatokea kwenye ndoa yenu. Angalia nini makubaliano yenu yanasema. Ni jambo la msingi sana kuwa na makubaliano kuwa iwapo utathibitishavpasipo shaka kwamba ameliwa nini kitokee na hakuna kusamehe. Tena huenda wakati analizwa alikuwa anakutukana wewe ni fala tu. Si unajua show za wizi
 
Na mapenzi ukishaonja tu yanakolea hasa ya wizi matamu sana, mtafute jamaa anayemfinyanga mkeo uongee naye kiume pia uwe mvumilivu usipanic, wakalishe wote na mkeo mwambie aache hiyo tabia.Kisaikolojia jamaa akijua mchezo wote unaufahamu atahisi kuwa unamuona kila mahali atakapopanga kukutana na mkeo tena ata akifanya naye mapenzi inakua ni kama Mtu anayefanya hadharani hivyo kiufupi hatarudia tena naomba ufanye hili kirafiki tu na kwa u pole kabisa mweleze kwa jinsi gani ndoa yako ni muhimu sana kwako. Ukifanya hili mbele ya mkeo nina Imani ata yeye atajihisi guilt na hatarudia tena.
 
Pole sana mkuu lakini hawa watu huwa wanajikwaa kwenye vitu vya ajabu sana ni kumuomba Mungu na kuwaombea wake zetu kila siku maana kadri mnavyopendana na ibirisi anatafuta njia ya kuwavuruga.
Ushauri wangu:-
1) Usimshirikishe mtu yoyote anaekufahamu wewe wala kumfahamu mkeo iwe ni ndugu ama rafiki
2)baada ya hapo kaaa wewe pekeyako relax bila kuwa na mawazo juu ya hili jambo jitahidi sana hapa then usikilize moyo wako unasemaje juu ya jambo hili bila kushurutishwa na kitu chochote.kama moyo unakutuma kusamehe samehe na wala usiwe na kinyongo na mkeo na pia kama haukutumi kusamehe usikurupuke kuwashirikisha watu wengi jaribu kuongea na watu wa karibu pia wawe watu wazima wenye busara.
3) kama ukiamua kusamehe ongea na mkeo kwa lugha ya kirafiki sana asigombane sana na yule jamaa amuombe siku wakutane akijifanya kama anamaongezi nae ili achukue simu ya yule mtu afute picha zake alizomtumia.
4) kama umeamua kusamehe kaa na mkeo uongee nae kwa lugha nzuri akwambie sababu ya yy kufanya hivyo naamini kama ni mwanamke mwenye akili na mwelewa atakuelewa kama utaongea nae kwa ukarimu.
Ni hayo tu yangu ila kumbuka hawa wenzetu ni dhaifu sana na pia kila binadamu ni mkosaji yatupasa kumuomba sana Mungu atuepushe kila aina ya majaribu lakini pia tujitahidi kuwa wanyenyekevu,upendo,huruma na ukarimu kwa wake zetu kwani waweza kuta jamaa kampata kwa kitu kidogo sana.
Pole sana ndugu na Mungu akuongoze katika kufanya maamuzi.All the best



Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
Hiyo namba tatu itamuongezea maumivu,atakapozungumza na jamaa ili eti wapange wakaonane ili atumie mwanya huo kufuta picha ,japo unamaanisha make amuage mmewe aende kwa jamaa ili akamrubuni acute picha unajua kuwa hizo picha zitafutwa baada ya mke wa mtoa mada kuukalia mkuyenge alafu katika ule muda wa mapumziko ya kujiandaa gemu la pili ndo huyo mke atakuwa anachezea simu ya mshikaji ndo afute picha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu kwa mke wako kuchepuka, hawa wanawake sijui kwa nini hawaridhiki??? Huenda labda ulikuwa humridhishi au jamaa alikuwa na vitu fulani vya kumshawishi zaidi ya wewe ndio maana ukazidiwa kete...

Kwa sasa hivi tulia kwanza, msamehe maisha yaendelee (japokuwa najua ni ngumu ila jitahidi tu)..Tabia ikizidi piga chini

Sent from my iPhone 5s using Tapatalk
Haridhishwi si aombe talaka nini kinamgandisha na hatoshelezwi?

Si wanasemaga msosi hata kwao upo hutoshelezwi sema uachwe sio unagawa urada wa mtu.
 
"...Ukiangalia wife hamna alichokosa kwangu tunaishi maisha safi anapata kila anachohitaji...."

Kosa kubwa sana la kifikra
 
amejitapa yupo poa sana kila idara! mtu unajikuta unapoteza nuru,unaliadaily wee mumeyupo busy namarafiki!anakuchukulia kama beki3 tena akukute umepaukaa ndo furaha zao ! atokee men wa kukupigia daily kukujulia hali,akupeleke hosp ukiugua dadekiiiiiii lazima unase
Ndiyo hapo kwa kwakweli waume wanawachukulia wake zao kivile kisa kakuoa kumbe kuna wengine wana kutamani hapo hawezi sema ukweli sio kweli ufumwe mawasiliano kisha ukamilishe si amini kitu hicho kuna something hapo kati, kila siku umechoka mapenzi yote yameishia huko nyumbani kutimiza wajibu tu si unataka basi lazima mke aumie baba avumilie tu waongee yataisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama bado unampenda na huoni kama utaweza kukaa bila yeye, kaa nalo wala usimwambie mtu hata wazazi wake ama wako.

Mueleweshe tu na jaribu kumsihi anachokifanya hakijengi.

Ukiwaambia watu unaharibu maana uliowaambia watakuwa wanaku'push kufanya maamuzi.

Mwanamke mida mingine unamfanyia kila kitu lakini anampa jamaa. Wana huruma sana hawa watu mpaka wanaboa.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] kumpa kila kitu nini hakufuata vipi alifuata penzi nawe penzi unaligawa yy afanye nini apenzi hayagawanyiki kamwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa wanawake hawa kama una hasira unaweza ukaua mtu,ndo maana vijana hawataki kuoa kabisa,yaani hivi viumbe huwa havieleweki,utakuta unampa kila kitu,lakini kaenda kwa huyo jamaa mwingine kisa tu jamaa amevaa shati zuri amependeza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu. Kuna jamaa yangu aliwahi kuniambia kuwa ukila mke wa mtu lazima na wako aje kuliwa,tena hata liwa tu bali ataliwa hadi wewe ujue. Sasa isiwe ni hii theory imekutokea.

Ila pole sana ,najua hali yako kwa sasa. Muombe Mungu akupe njia.
 
Dah pole sn... yaani hata sina cha kukushauri yaani nimeumia kama ni mm vile... Hapo ujitahidi uwe imara tu mkuu maana..

Iphone 5
 
Back
Top Bottom