Nimetafakari, nimeamua kujiunga na CHADEMA.

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Nimechukua muda mrefu kutafakari na kupata uamuzi ambao
Nimeridhika kuwa sahihi kwa kuhamia CHADEMA.

KWANINI CHADEMA?
Kitaalamu unapata majibu mafupi ambayo hayamchoshi yeyote
NIA YA DHATI YA KILE WANACHOZUNGUMZA, msimamo Na umakini.
Hapa nataka nifafanue kidogo, Kama ni kuzungumza hata CCM
Huzungumza kama si kubwabwaja lakini hawana nia ya dhati ya Kile
wanachozungumza badala yake imekuwa ni kinyume chake Hapa sitak
i kwenda mbali, hebu chukua mfano wa kauli hii Dr, Profesa Jakaya
Mrisho Kikwete “Maisha bora kwa kila Mtanzania” Kauli hii imekuwa
kinyume kabisa tena kwa 200%, Wanachokifanya sasa ni chetu chao
chao chao. Ni wakati Huu ambao ninashuhudia bei ya mchele
ikifika 3000 tsh na Unga tsh 1200 bila kusahau kiberiti ambacho sasa
ni 100tsh WAPI NINAKOTOKA? Toka mwaka 1998 nilikuwa ndani ya chama
cha wananchi CUF Nimeamua kuachana na chama hiki sababu kuu ikiwa ni
kukosa Nguvu na watu wenye nia ya dhati. Kuna wachache wana nia
ya dhati lakini chama kimekosa umakini Kwa kushindwa kutambua mapandikizi
ya CCM ambayo yamekuwa Mwiba ndani ya chama.

DHANA YA UDINI.
Kile kinachoitwa wagawe uwatawale ndicho kilichonichelewesha Kujiunga
na Chama hiki makini. CCM wamefanikiwa sana katika Mbinu hii kwa kuwatumia
baadhi ya viongozi wa dini ambao wamekuwa Wakikipigia Debe chama hicho
kwa kutamka wazi kuwa CHADEMA Ni chama chenye msimamo wa kidini.
Sipendi kuwataja wote lakini nafahamu wazi kuwa kuna viongozi wa Dini
ambao wanatumiwa na chama Tawala huku wakiuza utu kwa kwa Vitu kama
Gari, nyumba n.k Sitoizungumzia bakwata kwa sababu hakuna asiyefahamu kuwa
bakwata Ni CCM kwa 100% Hapa naomba nitoe mfano wa Shekhe mmoja ambaye
alikuwa katika msikiti Wa mtoro anajulikana kwa jina la Khalifa Hamisi
(amefukuzwa kwa bakora Na waumini wenye Jazba) Huyu amewahi kusimama
kwenye mimmbari kumpinga waziwazi ndugu Augostino Lyatonga Mrema wakati
ule akiwa na nguvu ndani ya NCCR- MAGEUZI. Kaifanya kazi hii na kueneza propaganda
mzito kiasi cha Waislamu wengi kumchukia Mrema wakati huo.

NASAHA ZANGU KWA WAISLAMU.
Nina mengi ya kuzungumza lakini naomba nifupishe kwa kutoa nasaha Kwa ndugu
zangu waislamu kuwa wakati sasa umefika kwa sisi kuachana Na propaganda na
unafiki wa CCM na kujiunga na CHADEMA ili Kuking’oa chama hicho ambacho
hakiwaumizi WANACHADEMA tu Bali Watanzania wote kwa ujumla. Maisha magumu
Tuunganishe nguvu na WANACHADEMA tuling’oe Genge hili la MAFISADI.
 
Pole sana kwa uamuzi wako, maana
.
"UKIJIUNGA NA CHADEMA, UNAKUWA UMEPUNGUKIWA NA AKILI".
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
kaka wewe ni mtu mkubwa sana sema watu wengi hapa JF wanaweza wakawa hawakuji ..karibu sana kijana nakumhbuka walivyokuletea zengwe kwenye mbio za ubunge bora umehama karibu sana
 
CHADEMA inasemaje kuhusu kuweka mikataba ya kiserikali hususan na makampuni makubwa ya kigeni wazi kwa wananchi wote?
 
Nimechukua muda mrefu kutafakari na kupata uamuzi ambao
Nimeridhika kuwa sahihi kwa kuhamia CHADEMA.

KWANINI CHADEMA?
Kitaalamu unapata majibu mafupi ambayo hayamchoshi yeyote
NIA YA DHATI YA KILE WANACHOZUNGUMZA, msimamo Na umakini.
Hapa nataka nifafanue kidogo, Kama ni kuzungumza hata CCM
Huzungumza kama si kubwabwaja lakini hawana nia ya dhati ya Kile
wanachozungumza badala yake imekuwa ni kinyume chake Hapa sitak
i kwenda mbali, hebu chukua mfano wa kauli hii Dr, Profesa Jakaya
Mrisho Kikwete “Maisha bora kwa kila Mtanzania” Kauli hii imekuwa
kinyume kabisa tena kwa 200%, Wanachokifanya sasa ni chetu chao
chao chao. Ni wakati Huu ambao ninashuhudia bei ya mchele
ikifika 3000 tsh na Unga tsh 1200 bila kusahau kiberiti ambacho sasa
ni 100tsh WAPI NINAKOTOKA? Toka mwaka 1998 nilikuwa ndani ya chama
cha wananchi CUF Nimeamua kuachana na chama hiki sababu kuu ikiwa ni
kukosa Nguvu na watu wenye nia ya dhati. Kuna wachache wana nia
ya dhati lakini chama kimekosa umakini Kwa kushindwa kutambua mapandikizi
ya CCM ambayo yamekuwa Mwiba ndani ya chama.

DHANA YA UDINI.
Kile kinachoitwa wagawe uwatawale ndicho kilichonichelewesha Kujiunga
na Chama hiki makini. CCM wamefanikiwa sana katika Mbinu hii kwa kuwatumia
baadhi ya viongozi wa dini ambao wamekuwa Wakikipigia Debe chama hicho
kwa kutamka wazi kuwa CHADEMA Ni chama chenye msimamo wa kidini.
Sipendi kuwataja wote lakini nafahamu wazi kuwa kuna viongozi wa Dini
ambao wanatumiwa na chama Tawala huku wakiuza utu kwa kwa Vitu kama
Gari, nyumba n.k Sitoizungumzia bakwata kwa sababu hakuna asiyefahamu kuwa
bakwata Ni CCM kwa 100% Hapa naomba nitoe mfano wa Shekhe mmoja ambaye
alikuwa katika msikiti Wa mtoro anajulikana kwa jina la Khalifa Hamisi
(amefukuzwa kwa bakora Na waumini wenye Jazba) Huyu amewahi kusimama
kwenye mimmbari kumpinga waziwazi ndugu Augostino Lyatonga Mrema wakati
ule akiwa na nguvu ndani ya NCCR- MAGEUZI. Kaifanya kazi hii na kueneza propaganda
mzito kiasi cha Waislamu wengi kumchukia Mrema wakati huo.

NASAHA ZANGU KWA WAISLAMU.
Nina mengi ya kuzungumza lakini naomba nifupishe kwa kutoa nasaha Kwa ndugu
zangu waislamu kuwa wakati sasa umefika kwa sisi kuachana Na propaganda na
unafiki wa CCM na kujiunga na CHADEMA ili Kuking’oa chama hicho ambacho
hakiwaumizi WANACHADEMA tu Bali Watanzania wote kwa ujumla. Maisha magumu
Tuunganishe nguvu na WANACHADEMA tuling’oe Genge hili la MAFISADI.

karibu.
 
Nyumbani husema hivi 'hata wa mwisho naye ni mtoto' ...karibu sana,na wengine hata kesho wazidi kuja,hamjachelewa.
 
M4C naona inafanya kazi, karibu sana. VUA GAMBA VAA GWANDA.
 
Nanyi mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru. Usifiche ujio wako katika harakati za ukombozi unazoziamini. Jitaje wewe ni nani kama alivojitaja Kamanda James Milya.
 
Back
Top Bottom