Nimetafakari, nimeamua kujiunga na CHADEMA.

Nimetafakari, nimeamua kujiunga na CHADEMA.

Hongera sana, wengine tunasubiri chama chetu TEA PARTY (rightist) of Tanzania kitakapozaliwa. Sisi wengine ni local rightist wa Tanzania ambao tunaamini Tanzania itakombolewa pale tu wazawa wa Tanzania watakapokuwa na uwezo wa kuwaajiri wazawa wenzao. Tunaamini kamwe binadamu wote hatuwezi kuwa sawa, lazima kuwepo na tabaka lenye kuongoza. Tabaka hili halipatikani kwa ufisadi bali kwa vipaji na juhudi binafsi za mtu kama vile akina Mark Zuckerberg, Bill Gates, Ndesamburo, e.t.c. Tunahitaji akina Bill Gates wa kibongo. Wengine hatuamini sera za kugawana umaskini za CHADEMA ambazo kamwe haziwezi kuikomboa Tanzania. Sera za kugawana umaskini zilishatumiwa sana na CCM tangu uhuru mpaka miaka ya 90'S na sasa wamebaki hawajui hata wanakokwenda.
Wasalimie sana CHADEMA, ila swali moja napenda kukuuliza kuwa unatarajia kuwa kundi lipi kati ya haya... Kundi la mlengo wa kulia (rightist) ambalo waumini wake wakubwa ni Mh Mbowe, Ndesapesa, Owenya etc au utakuwa kundi na mlengo wa kati (centrist) ambalo muumini wake mkubwa ni ZZK etc, au kundi la mlengo wa kushoto (leftist) ambalo linasadikika kuongozwa na jembe lao lenyewe DR W. Slaa, Tundu Lissu, Mnyika etc?.
Ukionana nao kawaeleze kuwa Tanzania ya sasa tunahitaji itikadi za vyama, utaratibu wa kuwa na vyama vyenye wanachama wenye itikadi mbalimbali kama kundi la watu wanaofukuza mwizi ulishapitwa na wakati. Huu ndio utaratibu CCM wanaufanya na CHADEMA wanaiga kila kitu, no wonder mara utasikia sijui Ole Miria leo yuko CCM mara kesho yuko CDM, mara Lowassa atahamia CDM na kelele kibao zunazisikia. Isije ikawa na wewe hayo yote uliyoandika kuhusu CHADEMA yahatotoki moyoni mwako bali malengo yako ni kutegeshea 2015 kama kama sera za kugawana umaskini zitashika hatamu ili nawe japo hata damu ya sungura wa Tanzania ikirukie pale atakapokuwa anachinjwa
 
Haya mambo ya kuwa mwanachama wa chama fulani ni upuuzi mtupu. Kama huhitaji kuwa kiongozi hakuna haja ya kujiunga na chama chochote.

Tuachane na ushabiki wa vyama maana huu unawanufaisha wachache na familia zao ambao huhodhi madaraka kwa muda mrefu. Pigania nchi na sio chama. Chama kitakachokuwa na uongozi au mgombea mzuri ndio cha kupigia kura na sio kushabikia kelele za msimu.

Kama CHADEMA watasimamisha kiongozi mzuri kuliko CCM, NCCR, CUF n.k., then tuwape support, lakini tusijilazimishe kuwa mashabiki wa chama na kuweka madarakani watu wasiofaa japo kuwa tunao uwezo wa kupiga kura bila kufungamana na chama chochote. Mungu ibariki nchi yetu.
 
Pole sana kwa uamuzi wako, maana
.
"UKIJIUNGA NA CHADEMA, UNAKUWA UMEPUNGUKIWA NA AKILI".
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
pole sana mkuu

afadhali anayepungukiwa na akili kwani at least alikua nazo kuliko wewe uliye na zero from day 1
 
Back
Top Bottom