Nimesoma taarifa ya TCU kusitisha udahili kwa vyuo kadhaa

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Anaandika Abdul Nondo.

Nimesoma taarifa ya Tume ya vyuo vikuu inayohusu kuzuia vyuo kadhaa kuendelea kutoa Elimu na vingine kusitishiwa udahili na kuwekwa chini ya uwangalizi. Ni kweli usiopingika vipo vyuo vingi vilivyokuwa vinatoa Elimu kwa kukeuka taratibu hongereni sana Tume ya vyuo vikuu (TCU).

Ilia kinachoshangaza ni tume kutoa maagizo hayo ikioneshwa kutokujali hata kidogo juu ya hatma ya wanafunzi na kuishia kusema wanafunzi wake wahamishwe.

Na ikamaliza bila hata kujibu maswali Muhimu ya msingi.

1.hamjatuambia kwanini mmeshusha Rungu kwa vyuo ambavyo tayari vimedahili wanafunzi 2018/2019.

>Je,wanafunzi hawa na wenyewe watahamishiwa vyuo vingine au waanze kuomba upya?

Na kama kuhamishiwa vyuo vingine wanaamishwa na nani ikiwa wamedahiliwa na chuo wapo katika Database ya chuo ?

Na kama wanahamishwa na chuo hiko,chuo wanamamlaka yapi ? ,na kama wanahamishwa na Tume ya vyuo vikuu wana hamishwa kwa utaratibu upi ?

Je ,wanafunzi waliodahiliwa katika vyuo hivyo mwaka huu 2018/2019 bado hawajasajiliwa chuoni hapo watahamishwa kwa njia ipi?

Tume ya vyuo vikuu itawadahili na kuwagawanya katika vyuo vingine ? ,hayo mamla TCU wanayatoa wapi ,mamlaka hayo kwa sasa yapo chini ya chuo husika .

Kama wanafunzi hao watahamishwa vyuo vingine ,kwa njia yeyote tuu itakayotumika ,Je mnajuaje kama chuo mlichomuhamishia kwake sio chuo apendacho na kozi aipendayo haipo katika chuo hiko ,anasaidiwaje huyu.?

Au wanafunzi hawa waliodahiliwa 2018 katika vyuo hivyo ,watapewa nafasi nyingine ya kuomba chuo anachotaka ,anapewaje nafasi tena ikiwa tayari mfumo limpa Code ya kuhakiki akahakiki chuo hiko ambachokimefungwa ,Je ,anasaidiwaje kuomba chuo kingine ikiwa mfumo ukipewa CODE na kuthibitisha haukuruhusu tena kuomba chuo?

Je ,kama mtawaruhusu kuomba kwa njia yeyote ! ,je hawaoni kama watakosa vyuo sababu udahili unaoendelea unaelekea mwisho sababu awamu ya tatu tayari inafunguliwa leo ya udahili ,je kuna kipaumbele chochote watapewa? .

Sababu kuna wanafunzi wengi tangu awamu ya kwanza ya udahili, na ya pili hawajapata vyuo ,wengine hawajapata hata code ,wengine wapo wapo tuu hawajui hatma yao ! Ndio maana nauliza kuna kipaumbele chochote mmewapa hawa wanafunzi.

Sababu hii sio kosa lao kuanza kusumbuka kuhusu vyuo bali ni kosa la TCU kusubiri hadi udahili na wanafunzi kudahiliwa ndio waje kufanya kuzuia walishundwa kuzuia kabla ya mchakato wa udahili kuanza?

Naendelea kuuliza wanafahamu kama future ya wanafunzi hawa imeharibiwa TCU bila kujali?

Hivi wanajua kuwa tayari bodi ya Mikopo ilikuwa hata imetenga fedha za mkopo kwa baadhi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga katika vyuo hivyo 2018/2019 ?

Wanafahamu kuwa sasa bodi ya Mikopo wana kata majina yao hao wanafunzi waliodahiliwa katika vyuo hivyo sababu tuu BODI hawatoi mkopo kwa mwanafunzi asiyeeleweka amedahiliwa chuo gani.

Wanafahamu kuwa bodi ya Mikopo haitasubiri kujua mwanafunzi hawa watahamishwa chuo gani na lini ili wapewe mkopo? Kwa wanaoendelea mkopo wao utasitishwa na watapewa kwa Chuo watakachopelekwa, je vipi kwa ambao wamedahiliwa tuu na hawajasajiliwa chuo hapo? Ni wazi mkopo wao utaondolewa !

Na uhakika kwa sarakasi hadi kuisha ,na hawa wanafunzi kupata vyuo tayari bodi ya Mikopo itakuwa imefunga dirisha na mwanafunzi hawa hata kama watapata chuo mkopo kwao itakuwa too late !! Na wengi hatma yao itaanza kuyumba hapo .


Swali la mwisho !

Kwanini TUME YA VYUO VIKUU izuie vyuo hivi baada ya udahili wa 2018 na sio kabla ya udahili ili wanafunzi wasiombe kwa vyuo hivi ,waombe vyuo vingine kuepusha usumbufu unaojitokeza sasa.


TSNP inaandaa taarifa na mawazo mbadala wa kipi kifanyike ,natumai changamoto hii itapata ufumbuzi.

Suala lingine ni Hao Bodi ya mikopo waliotoa majina ya waliokosea.

Sasa kama bodi hawana fedha ni bora kuweka wazi kuliko kuviziana kwa kutafutiana makosa yasio kuwepo .

Cheti kimehakikiwa RITA ,mnasema hakija hakikiwa?

Mtu ameweka taarifa zote za mdhamini wake mnasema hajaweka ?

Mtu ameambatanisha hati ya mahakma kuwa mzazi wake amemtelekeza na uthibitisho kutoka kwa serikali za mitaa ,hamtaki mnataka barua ya kifo cha mzazi ,hawa watoto waonewe huruma !

Mbaya zaidi hakuna utaratibu maalumu wanafunzi hawa wafanye nini sasa ! Bodi mpo kimya mnahesabu siku tuu za kufunga mchakato .

Na hili TSNP inajadili itatoa mapendekezo yake kwa Bodi .


Wengine ni hao NACTE yaani ,tabu juu ya Tabu hadi sasa kuna wanafunzi hawajapewe AVN (award verification number) ,kumekuwa na kutupiana mpira chuo kinasema tayari tumepeleka matokeo NACTE ,tatizo lipo NACTE ,NACTE nawao wanasema tatizo lipo chuo hawajaleta matokeo yako ya diploma na certificate, chuo tumepeleka tayari matokeo yote !

Haya ni matatizo makubwa yaliyopo katika mifumo ya Elimu katika vyuo vyetu nchini kuna haja taasisi hizi kukaa chini na kuanza kutafakari njia bora zaidi ya kuhudumia wanafunzi.


Abdul Nondo.
 
Kuna changamoto katika mifumo ya udahili na uombaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ipo haja mifumo hii kufanyiwa tathmini
 
Ukiangalia vizuri unaona kabisa ama huu mchakato wanaoendesha hawana utaalamu wa kutosha au bado kuna upungufu wa vipengele vinavyowaongoza.Bado mwezi 1 vyuo vifungue halafu mnafuta udahili ambao watu wameomba miez 2 ilopita
 
Back
Top Bottom