Nimesitisha rasmi kuchangia harusi

Safi sana mkuu, watu hawachangii wagonjwa wanaoumwa wanahitaji dawa au vipimo hata 50k haifiki lkn wanachangia harusi.

Nina ndugu na wadogo zangu huko kijijini wanasoma kayumba kwa taabu halafu nijifanye mjini doninwa kuchangia harusi??

Mimi nilishakataa kata na wife wangu nae kaniunga mkono, tunachangia vitu vya lazima kama shule, safari ya lazima, vifo, magonjwa n.k
 
Harusi nitachangia, sito changia endapo sitokuwa na pesa. Pesa ni matokeo tu.
 
Wewe ulichangiwa kwenye harusi YAKO. Je waliokuchangia wangekuwa na fikra zako ungeweza kufanya sherehe bila msaada wowote?
 
Vipi wewe wakati unaoa si ulichangiwa iweje wewe leo ukatae kuwachangia wenzio waliokuchangia? Ulitakiwa ukatae kuchangiwa then
 
Maharusi wanatangaza ndoa wakati hawana hata single cent wao akili yao wanawaza michango tu..
 
Kila mwanaume anapaswa kujipanga harusi yake iweje kwa kile alicho nacho. Kutangaza ukitegemea michango ni lawama. Watu tuna matatizo yetu na familia zetu, tufanye ya maana.
 
ukiendekeza haya mambo ni kero, juzi kuna mama kaja ana sare ya dera na mchango wa kitchen party alishaolewa miaka karibia nane sasa, walifunga ndoa bila sherehe eti leo ndiyo wanafanya harusi,
nimeona ni ujinga kuchangia vitu kama hivi.
ha hahahaha anataka avae shela
 
kinachoniudhi mimi ni watu kupanga m=bajeti kubwa kupitia mifuko ya watu ...... hivi mkienda kanisani au msikititini au serikalini mkafunga ndoa .. jioni mkakaa mahali mkala chakula kwa pamoja kila mtua akenda kwake hiyo itakuwa siyo ndoa au? tatizo tuanakazana harusi huku misingi ya ndoa hatujui ni ujinga aisee
 
Mimi sikumbuki mara ya mwisho nilichangia lini harusi. Nilishafanya maamuzi miaka mingi sana. Ndugu na marafiki wameshalijua hili hivyo hata mialiko sipati, na sioni shida maana sio lazima niende.
Nilifanya harusi ya binti yangu na sikuchangisha maana nilijikuna ninapofikia. siwezi kufanya kitu cha kifahari halafu the next day watu hamna hata chakula ndani, ni ujinga na ushamba pia.
ukioa au kuolewa jipange wewe na familia yako ambayo ni wazazi wako na ndugu zako wa kuzaliwa nao, mnaweza, lakini sio kuchangisha mpaka harusi inapita una maadui tayari wale ambao uliwalazimisha wakuchangie wakashindwa.
hii kitu iko Tanzania tu. tuchangie wagonjwa, bora hata na wanaosoma na misiba lakini harusi hapana. si lazima ufanye harusi ya mamilioni. muhimu ni ndoa ambayo haihitaji gharama kubwa.
Umefanya maamuzi mazuri, fanya vitu vya maendeleo achana na michango ya harusi haina tija
 

Kuna watu wamezaliwa kupenda shughuli, kila utumbo lazima achange na ahudhurie, mara nyingi wamama. wanaume mnatakiwa kidogo muwe wakali huko nyumbani kwa wake zenu waachane na hivi vitu ambavyo havina maendeleo. Ukiongelea harusi inaambatana na send off, reception, kitchen party, kuna bag party pia siku hizi, ujinga mtupu. Bado mke hajashika mimba akafanyiwa baby shower au uswahilini wanaita beseni... ni michango tu, hamjashona sare, tena kwenye shughuli zote hizo... excuse me... hamnipati.. pesa yangu ina mambo lukuki ya maana sio upuuzi wa harusi na michango ya kishenzi isiyokwisha.
 
Temea mate mbali mjumbe usijilaani bure maana tutakula matunda ya vinywa vyetu.
Kwani kuolewa ni harusi mkuu?

Zamani si unaenda tu kwa baba na ng'ombe, unanichukua.

Sisi ukoo wetu tuna utamaduni wa get together. So mwanaume watamuona tu bila gharama za ziada.
 
Hii michango ya harusi,kitchen party,sendoff etc..inarudsha nyuma maendeleo..mtu usipokuwa makini hauendelei.
 
Wairi wa Habari na Utamamaduni Ndg.Nape angepiga tu marufuku michango ya harusi.Tungeokoa pesa nyingi.
 
Uamuzi mzuri
mimi nilishaacha kuchangia harusi muda tu
 
Kwani kuolewa ni harusi mkuu?

Zamani si unaenda tu kwa baba na ng'ombe, unanichukua.

Sisi ukoo wetu tuna utamaduni wa get together. So mwanaume watamuona tu bila gharama za ziada.
Tamaduni hubadilika dada yangu utapata anayeamini katika sherehe maana hata za Tamaduni huwa na sherehe ndogo ambayo ndugu pia uchangia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…