Nimesitisha kumuombea Rais

Nimesitisha kumuombea Rais

Ni vizr kama unajijua wewe ni shetan so endelea na endeleeni na ushetan wenu wa kudhurumu Haki za watu wake na Mengne kwa kisingzio cha Mamlaka, but Mjue Mungu hadhihakiwi, soon Hasira ya Mungu Mtaiyona na mmesha anza Iyona, then Kuhusu Israel sijasema mim bali ni Neno lake Mwenyewe!
Utasubiri sana..haki IPI imedhurumiwa..nchi ilikosa mwenyewe mliila hadi basi..sasa kaja mzalendo mnajifanya...pu..Mb...avu Zenu....na mnanikela sana watu wa aina hii...mbona wapinzani mwenyewe wametulia...nyie sisiemu wapiga dili ndo mnashupalia utadhani mmeibiwa...this time mtakoma haibiwi MTU hapa..na maombi tuna endelea kumuombea jembe letu ,...Kiongozi mzalendo..mpenda Taifa letu...HAPA KAZI TU...
 
Nani anauhakika kua ni kweli kwamba ulikua ukimuombea? Yaani kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo jinsi tunavyozidi kuwafahamu ukawa halisi! Ni sifuri tu!
Ukiwafahamu UKAWA utawafanya nini.
 
Utasubiri sana..haki IPI imedhurumiwa..nchi ilikosa mwenyewe mliila hadi basi..sasa kaja mzalendo mnajifanya...pu..Mb...avu Zenu....na mnanikela sana watu wa aina hii...mbona wapinzani mwenyewe wametulia...nyie sisiemu wapiga dili ndo mnashupalia utadhani mmeibiwa...this time mtakoma haibiwi MTU hapa..na maombi tuna endelea kumuombea jembe letu ,...Kiongozi mzalendo..mpenda Taifa letu...HAPA KAZI TU...
Punguza mapovu hata kama una point inaweza isionekane.
 
Yeye mwenyewe siku hizi hasemi tumwombee
 
Mkuu nakeleka sana napoona watu mnaandika kwa hisia za matumbo yenu...hadi nashidwa kujizuia..nashukuru kama umeziona point..
Punguza mapovu hata kama una point inaweza isionekane.
 
Utasubiri sana..haki IPI imedhurumiwa..nchi ilikosa mwenyewe mliila hadi basi..sasa kaja mzalendo mnajifanya...pu..Mb...avu Zenu....na mnanikela sana watu wa aina hii...mbona wapinzani mwenyewe wametulia...nyie sisiemu wapiga dili ndo mnashupalia utadhani mmeibiwa...this time mtakoma haibiwi MTU hapa..na maombi tuna endelea kumuombea jembe letu ,...Kiongozi mzalendo..mpenda Taifa letu...HAPA KAZI TU...
Mzalendo ni Nyerere ambae alijenga Nyumba kibao kwa kodi zetu, alafu Huyo mzalendo akaja kuziuza na kuzigawa ovyo ovyo, then nakushaur uzidishe hayo maombi yako kwa siku mara mia ili viwanda vije kutoka kwa mungu wenu ambae husikiliza na hujibu kwa kumpa mema mtu batili, ubarkiwe sana, Mwisho mm sijawai kuwa chama cha majambazi,au maccm naomba unitake radhi
 
Mungu alishakasirika kwa kauli yake ya kuahidi kugeuza binadamu wenzake (kuwapeleka kwa) mashetani ili hali Mungu anashusha manabii ili binadamu wamtambue na wamuepuke shetani.Infact kiongozi unapaswa kuwa mfano wa kumuamini na kumtegemea Mungu na kuongoza watu kwa busara na hekima bila ya kuwabagua tofauti na mtazamo wake wa kibinafsi(Anapambana na wapinzani kudhoofisha ili arudi tena 2020)Na nina wasiwasi kwamba ni mtumiaji mzuri wa tiba mbadala
 
Alipochaguliwa tu alitusihi Watanzania wote bila kujali itikadi zetu, makabila yetu na dini zetu tumwombee, kwa kile alichosema alichokikuta kule kilihitaji maombi.

Kweli kama Mtanzania nilianza maombi ya nguvu, nilitenga siku moja ya mwezi kufunga kwa ajili yake nikijua kazi aliyonayo ni ngumu na ya hatari.
Pamoja na kufanya hivyo, leo takriban mwaka unakwisha bila kuona faida ya maombi yangu. Maisha ndiyo yamezidi kuwa magumu afadhali ya mwaka jana.

Katika maombi yangu nilitegemea atakuwa rais wa wanyonge kama alivyoahidi.
Nilitegemea atakuwa rais wa vyama vyote, dini zote na makabila yote kama alivyoahidi. Nilitegemea rais atakuja kuwapata mikopo wanafunzi wote kama alivyoahidi.

Nilitegemea maombi yangu yatambadili na kutawala kwa haki kwa kufuata utawala wa sheria, rule of law. Nimesubiri ahadi yake ya ajira kwa vijana kama alivyoahidi, matokeo yake kaajiri vijana kwa kuangalia ukada na mbaya zaidi kaajiri vijana wenye ukakasi mbele ya jamii.

Matokeo ya maombi yangu ni kusitishwa kwa ajira, kunyanyaswa kwa watumishi wa umma kwa kisingizio cha kuhakiki wafanyakazi hewa.
Maombi yangu yamesababisha wafanyabiashara kunyanyaswa kwa kuongezewa kodi zisizo na ulazima.

Nilitegemea madawa yataongezeka mahospitalini, matokeo yake hata dawa ya chanjo kwa watoto imekosekana. Naona kama maombi yangu yanazidisha ugumu wa maisha kwa wananchi. Kwanini basi niendelee kuomba?

Kama mwaka jana niliishi vizuri, watoto walisoma bila kumwombea rais aliyekuwepo, ajira zilikuwepo wafanyakazi walipanda madaraja bila kumwombea rais aliyekuwepo, wanafunzi walipata mikopo tena wote bila kumwombea rais aliyekuwepo, kuna sababu gani basi kuendelea kumwombea aliyepo?

Nimestisha maombi.

Ni uamuzi wangu sijashinikizwa na mtu.

Quinine.
1.Ulishiriki kumpigia kampeni/kumnadi
2.Ulishiriki kumchagua
3.Shiriki kumuombea
4.Shiriki kuisoma namba
 
Mie ndio kwanza naanza maombi rasmi. Nchi inahitaji maombi yetu wote.

unamjua unayemuombea?au umekurupuka tu?mungu aache kusaidia watu Syria hukooo akusaidie mtanzania kwa makosa tuliyojitakia 2015 October
 
1.Ulishiriki kumpigia kampeni/kumnadi
2.Ulishiriki kumchagua
3.Shiriki kumuombea
4.Shiriki kuisoma namba
Hata kama nilishiriki kumnadi, anayofanya leo siyo yale aliyoahidi wakati wa kampeni.
 
"mjomba rudi mjomba, huku wanao wanalia lia,tangu umkabidhi familia anko huyu yaani hatujawahi kula hata wali wala kuku, ni mwendo wa dagaa/bamia na ugali siku nyingine tunapiga ndefu"
 
Goli la Juventus limekataliwa imeniuma sana
 
Sijui ni dini gani hiyo usichopata kile ulichokuwa unaomba katika maombi unaacha kuomba!
Dini ya Kujitambua hiyo. Badala ya kupoteza muda kufanya maombi, ni bora kuchakarika au angalau kuchagua viongozi ambao sio "chaguo la Mungu", (tafsiri magamba).
 
Wapo watu wanaodai wamechoka kuniombea, wewe choka tu, mimi nasonga mbere.
 
Back
Top Bottom