Nimesitisha kumuombea Rais

Nimesitisha kumuombea Rais

Mamba wa Mungu unamfananisha na Magufuli?

Kwa hiyo unasubiri siku ya tatu afufuke? Endelea kuomba.
Yani kwa kua ni uhulu wa mawazo na maamuzi!!!! Jamaa we acha kuomba sepa.sisi tunaomba
 
Hata usipomuombea wewe,wengi tunaompenda mungu anapokea maombi yetu
Nyie muombeeni mbowe azidi kutafuna ruzuku
Wewe ndiye unayempenda Mungu?Utawezaje kumpenda Mungu na kushuhudia uongo?mbona una chuki na Mbowe?Mungu gani unayempenda wewe?Kama ni Mungu wa Wakristo hayuko hivyo wala usijidanganye!
 
Alipochaguliwa tu alitusihi Watanzania wote bila kujali itikadi zetu, makabila yetu na dini zetu tumwombee, kwa kile alichosema alichokikuta kule kilihitaji maombi.

Kweli kama Mtanzania nilianza maombi ya nguvu, nilitenga siku moja ya mwezi kufunga kwa ajili yake nikijua kazi aliyonayo ni ngumu na ya hatari.
Pamoja na kufanya hivyo, leo takriban mwaka unakwisha bila kuona faida ya maombi yangu. Maisha ndiyo yamezidi kuwa magumu afadhali ya mwaka jana.

Katika maombi yangu nilitegemea atakuwa rais wa wanyonge kama alivyoahidi.
Nilitegemea atakuwa rais wa vyama vyote, dini zote na makabila yote kama alivyoahidi. Nilitegemea rais atakuja kuwapata mikopo wanafunzi wote kama alivyoahidi.

Nilitegemea maombi yangu yatambadili na kutawala kwa haki kwa kufuata utawala wa sheria, rule of law. Nimesubiri ahadi yake ya ajira kwa vijana kama alivyoahidi, matokeo yake kaajiri vijana kwa kuangalia ukada na mbaya zaidi kaajiri vijana wenye ukakasi mbele ya jamii.

Matokeo ya maombi yangu ni kusitishwa kwa ajira, kunyanyaswa kwa watumishi wa umma kwa kisingizio cha kuhakiki wafanyakazi hewa.
Maombi yangu yamesababisha wafanyabiashara kunyanyaswa kwa kuongezewa kodi zisizo na ulazima.

Nilitegemea madawa yataongezeka mahospitalini, matokeo yake hata dawa ya chanjo kwa watoto imekosekana. Naona kama maombi yangu yanazidisha ugumu wa maisha kwa wananchi. Kwanini basi niendelee kuomba?

Kama mwaka jana niliishi vizuri, watoto walisoma bila kumwombea rais aliyekuwepo, ajira zilikuwepo wafanyakazi walipanda madaraja bila kumwombea rais aliyekuwepo, wanafunzi walipata mikopo tena wote bila kumwombea rais aliyekuwepo, kuna sababu gani basi kuendelea kumwombea aliyepo?

Nimestisha maombi.

Ni uamuzi wangu sijashinikizwa na mtu.

Quinine.
...prayer is not in the success equation, prayer is a liberation equation. Decision making is the success equation...
 
Attachments

Ulikuwa unampigia kelele Mungu. Kuna watu wanataka kuondokana na natural disasters kila siku ndio wanahitaji kuombewa.
Wewe unaombea......
 
Safi sana mtoa mada kwa kusitisha maombi.
 
Ulikuwa unampigia kelele Mungu. Kuna watu wanataka kuondokana na natural disasters kila siku ndio wanahitaji kuombewa.
Wewe unaombea......
Nitaendelea kuiombea nchi yangu kwa Mungu aiepushe na majanga na watu wabaya wanaoinyemelea.
 
Ni wazo zuri sana. Tuombee Nchi na sio Mtu, nasi sote tumeshathibitisha kuwa kumuombea mtu kunafanya huyo mtu kufanikiwa. Ni vema kuombea Nchi ifanikiwe na hapo makundi yote hata masikini na matajiri tuturidhika na kupendana na hofu iratoweka
 
Alipochaguliwa tu alitusihi Watanzania wote bila kujali itikadi zetu, makabila yetu na dini zetu tumwombee, kwa kile alichosema alichokikuta kule kilihitaji maombi.

Kweli kama Mtanzania nilianza maombi ya nguvu, nilitenga siku moja ya mwezi kufunga kwa ajili yake nikijua kazi aliyonayo ni ngumu na ya hatari.
Pamoja na kufanya hivyo, leo takriban mwaka unakwisha bila kuona faida ya maombi yangu. Maisha ndiyo yamezidi kuwa magumu afadhali ya mwaka jana.

Katika maombi yangu nilitegemea atakuwa rais wa wanyonge kama alivyoahidi.
Nilitegemea atakuwa rais wa vyama vyote, dini zote na makabila yote kama alivyoahidi. Nilitegemea rais atakuja kuwapata mikopo wanafunzi wote kama alivyoahidi.

Nilitegemea maombi yangu yatambadili na kutawala kwa haki kwa kufuata utawala wa sheria, rule of law. Nimesubiri ahadi yake ya ajira kwa vijana kama alivyoahidi, matokeo yake kaajiri vijana kwa kuangalia ukada na mbaya zaidi kaajiri vijana wenye ukakasi mbele ya jamii.

Matokeo ya maombi yangu ni kusitishwa kwa ajira, kunyanyaswa kwa watumishi wa umma kwa kisingizio cha kuhakiki wafanyakazi hewa.
Maombi yangu yamesababisha wafanyabiashara kunyanyaswa kwa kuongezewa kodi zisizo na ulazima.

Nilitegemea madawa yataongezeka mahospitalini, matokeo yake hata dawa ya chanjo kwa watoto imekosekana. Naona kama maombi yangu yanazidisha ugumu wa maisha kwa wananchi. Kwanini basi niendelee kuomba?

Kama mwaka jana niliishi vizuri, watoto walisoma bila kumwombea rais aliyekuwepo, ajira zilikuwepo wafanyakazi walipanda madaraja bila kumwombea rais aliyekuwepo, wanafunzi walipata mikopo tena wote bila kumwombea rais aliyekuwepo, kuna sababu gani basi kuendelea kumwombea aliyepo?

Nimestisha maombi.

Ni uamuzi wangu sijashinikizwa na mtu.

Quinine.
Pengine wewe ni mdhambi mno, maana maombi ya mwenye dhambi ni kelele mbele za Mungu; isipokuwa tu kama anaomba msamaha. Badili maombi mpendwa
 
Ni kweli mimi ni mdhambi kwa vile wewe ni mtakatifu tuambie maombi ya mtu asiye na dhambi yakoje.

Hapa duniani hakuna mtu asiye na dhambi hata aliyetuomba tumwombee definitely anayajua madhambi yake.
 
Endelea kuomba ili mtukufu apunguze jazba.
Aache kushindana na wapinzani wake kila wakati.
 
Mungu anadili na mambo makubwa yaliyo nje ya uwezo wetu kama kushikilia jua,hewa na maji,yaliyo ndani ya uwezo wetu kama kuchagua viongozi tusimlaumu.
 
Mnamuombeaje yule mtu? Anataka tuishi kama mashetani halafu mnamuombea? Mungu ninayemuamini hawezi kubali maombi kwa ajili ya mtu yule:
 
Bongo shida tuu Taifa Stars inafanya mazoezi ikicheza muiombee timu,Rais mumuombee,Yanga na Simba mziombee mnaombea watu wanaojiweza na kusahau wanaohitaji msaada wa kuombewa wagonjwa maombi ya kuzuia ajari,majanga na mengineyo tuungane na Rais kuombea Nchi na si kumuombea yeye tuu..
 
Back
Top Bottom