Nimesitisha kumuombea Rais

Nimesitisha kumuombea Rais

Alipochaguliwa tu alitusihi Watanzania wote bila kujali itikadi zetu, makabila yetu na dini zetu tumwombee, kwa kile alichosema alichokikuta kule kilihitaji maombi.

Kweli kama Mtanzania nilianza maombi ya nguvu, nilitenga siku moja ya mwezi kufunga kwa ajili yake nikijua kazi aliyonayo ni ngumu na ya hatari.
Pamoja na kufanya hivyo, leo takriban mwaka unakwisha bila kuona faida ya maombi yangu. Maisha ndiyo yamezidi kuwa magumu afadhali ya mwaka jana.

Katika maombi yangu nilitegemea atakuwa rais wa wanyonge kama alivyoahidi.
Nilitegemea atakuwa rais wa vyama vyote, dini zote na makabila yote kama alivyoahidi. Nilitegemea rais atakuja kuwapata mikopo wanafunzi wote kama alivyoahidi.

Nilitegemea maombi yangu yatambadili na kutawala kwa haki kwa kufuata utawala wa sheria, rule of law. Nimesubiri ahadi yake ya ajira kwa vijana kama alivyoahidi, matokeo yake kaajiri vijana kwa kuangalia ukada na mbaya zaidi kaajiri vijana wenye ukakasi mbele ya jamii.

Matokeo ya maombi yangu ni kusitishwa kwa ajira, kunyanyaswa kwa watumishi wa umma kwa kisingizio cha kuhakiki wafanyakazi hewa.
Maombi yangu yamesababisha wafanyabiashara kunyanyaswa kwa kuongezewa kodi zisizo na ulazima.

Nilitegemea madawa yataongezeka mahospitalini, matokeo yake hata dawa ya chanjo kwa watoto imekosekana. Naona kama maombi yangu yanazidisha ugumu wa maisha kwa wananchi. Kwanini basi niendelee kuomba?

Kama mwaka jana niliishi vizuri, watoto walisoma bila kumwombea rais aliyekuwepo, ajira zilikuwepo wafanyakazi walipanda madaraja bila kumwombea rais aliyekuwepo, wanafunzi walipata mikopo tena wote bila kumwombea rais aliyekuwepo, kuna sababu gani basi kuendelea kumwombea aliyepo?

Nimestisha maombi.

Ni uamuzi wangu sijashinikizwa na mtu.

Quinine.
Mwanabodi hongera sana kw kuwa na Moyo wa kujitolea
Mungu akupe baraka zake.
Mungu huwa hamtupi mwombaji:
Mat 7: 7-8 na
kwa wale wengine Isa 43: 25-26.


Mkuu Wac wac wangu, Hayo maombi yasije kuwa yalikwenda kule kwingine....


 
Kwa hiyo umekaa unasubiri akuite fulani njoo ufanye kazi hii au unatafuta kazi haupati?
 
kwa sasa Kila mtu ajiombee mwenyewe,,,,siombei mtu mimi
Mwanabodi punguza hasira.
Tunakumbushwa kuwasalia na wengine..
Kilicho kizuri kula na nduguzo bila kusahau marafiki....
Hapa JFs ni sehemu ya marafiki zako.
 
Ubarikiwe sana n Mungu akuzidishie uhai kwa kujitambuwa kama ulikuwa unamwombea Kiongozi ambaye ni mbaguzi kama huyu basi ulikuwa umebeba laana kuu,utamwmbeaje mtu mwenye chuki na matajiri eti motto wa tajiri hata awe na division one ya tatu hatasomeshwa na serikali ,wazee hawatapewa kazi na yeye,wachaga na anyakyusa hawezi kuwapa kazi kwenye serikali yake,wanawake atawafikiria wa mwisho kwenye serikali yake huyu Mungu amemuona kwamba si wakuivusha nchi hii ndio maana laana na mabalaa yanaikumba nchi kwa ajili yake matetemeko, ukame,mauaji ya wakulima na wafugaji n.k
 
Waombaji hawachoki kusubiri... Kumbuka nabii Daniel aliomba siku ngapi?
 
Waombaji hawachoki kusubiri... Kumbuka nabii Daniel aliomba siku ngapi?
Inategemea unaombea kitu gani, kama ni uzima wa milele sawa sintochoka lakini kama ni kumwombea mtu nitachoka.
 
Tujiombee wenyewe maana hatujui kesho yetu itakuwaje kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe
 
Tuombe Mungu atupe kiongoz anayemtaka yy sio tunaomtaka sisi kisa alikudanganya atakuwa rais WA wanyonge..moyo WA mtu Giza nene.huenda yy anasema wataisoma no Na nyie mlikiri kwa vinywa vyenu chichiem mbele kwa mbele acha waisome no sasa kinywa kimeumba..mnaisoma no ombea MUNGU AWAPE RAIS
 
Maombi yamezidi tunaemuombea anaelekea kuwa LISHETANI KAMILI bora muombe kwa mungu wa ghamboshi
 
Mwanabodi punguza hasira.
Tunakumbushwa kuwasalia na wengine..
Kilicho kizuri kula na nduguzo bila kusahau marafiki....
Hapa JFs ni sehemu ya marafiki zako.
Mkuu ww acha tu,,,,,mwanzoni nlihisi nnaweza kuombea hawa watu ila kadiri wanavyonisomesha 1,2,3,4,5,6,,,,,,,sitaki hata kusikia na nnajiombea mwenyewe
 
ISAYA 43: 26


Aliyeona Huo Msitari Atusomee!!
 
Kwanza nakupongeza kwa ujasiri wa kumuombea Mwenyekiti wa ccm , chama ambacho kimeleta kila aina ya dhiki kwenye nchi hii , binafsi sijawahi na wala sitakuja kuthubutu ujinga huo .
Mkuu niliweka matumaini yangu rehani nikitegemea mabadiliko.
 
Back
Top Bottom