Nimesitisha kumuombea Rais

Nimesitisha kumuombea Rais

Kama kweli ulikuwa unaomba hutakiwi kukata tamaa.
Usitizame nyuma, endelea na maombi.
MUNGU ATAJIBU KWA WAKATI WAKE.
Mkuu sijakata tamaa ila nimeamua kujiombea mwenyewe.
 
Kumuombea mtu mwenye ulinzi mkubwa twenty four seven wa uhakika, huduma zote za muhimu anapata kwa uhakika na familia yake huo ni unaaa in Mremaz voice kiongozi anayelilia kuombewa akitekeleza majukumu yake naye ni mnaa tu anayetafta visingizio tu. Na ndo maana maana yamegeuka laana
 
wafilp 4:6 ."msijisumbue ktk neno lolote Bali katk kila neno kwa kuomba kusali pamoja na kushukuru"OMBA KWA AJIRI YA TANZANIA USICHOKE MUNGU ATAJIBU MAOMBI YAKO.
Ujue Watanzania husali zaidi ya miaka hamsini ili mambo yaende lakini ndo yanadumaa, tusipende kutumia maneno matakatifu kuhalalisha ujinga, vitu vingine vinahtaji actions zaidi tusiwe ka wajima kusali tu huku hatutaki kutekeleza majukumu yetu, hapo itakuwa kupoteza mda na kumwomba mungu baali asiyejibu.
 
Alipochaguliwa tu alitusihi Watanzania wote bila kujali itikadi zetu, makabila yetu na dini zetu tumwombee, kwa kile alichosema alichokikuta kule kilihitaji maombi.

Kweli kama Mtanzania nilianza maombi ya nguvu, nilitenga siku moja ya mwezi kufunga kwa ajili yake nikijua kazi aliyonayo ni ngumu na ya hatari.
Pamoja na kufanya hivyo, leo takriban mwaka unakwisha bila kuona faida ya maombi yangu. Maisha ndiyo yamezidi kuwa magumu afadhali ya mwaka jana.

Katika maombi yangu nilitegemea atakuwa rais wa wanyonge kama alivyoahidi.
Nilitegemea atakuwa rais wa vyama vyote, dini zote na makabila yote kama alivyoahidi. Nilitegemea rais atakuja kuwapata mikopo wanafunzi wote kama alivyoahidi.

Nilitegemea maombi yangu yatambadili na kutawala kwa haki kwa kufuata utawala wa sheria, rule of law. Nimesubiri ahadi yake ya ajira kwa vijana kama alivyoahidi, matokeo yake kaajiri vijana kwa kuangalia ukada na mbaya zaidi kaajiri vijana wenye ukakasi mbele ya jamii.

Matokeo ya maombi yangu ni kusitishwa kwa ajira, kunyanyaswa kwa watumishi wa umma kwa kisingizio cha kuhakiki wafanyakazi hewa.
Maombi yangu yamesababisha wafanyabiashara kunyanyaswa kwa kuongezewa kodi zisizo na ulazima.

Nilitegemea madawa yataongezeka mahospitalini, matokeo yake hata dawa ya chanjo kwa watoto imekosekana. Naona kama maombi yangu yanazidisha ugumu wa maisha kwa wananchi. Kwanini basi niendelee kuomba?

Kama mwaka jana niliishi vizuri, watoto walisoma bila kumwombea rais aliyekuwepo, ajira zilikuwepo wafanyakazi walipanda madaraja bila kumwombea rais aliyekuwepo, wanafunzi walipata mikopo tena wote bila kumwombea rais aliyekuwepo, kuna sababu gani basi kuendelea kumwombea aliyepo?

Nimestisha maombi.

Ni uamuzi wangu sijashinikizwa na mtu.

Quinine.
Vuta subira. Usichoke kuomba.
 
Wajinga wengine watakuja hp na kuanza kucomment ulizoea vya bure ndio maana unalalama kumbe Cy, kiukweli maisha yamekuwa magumu
 
Omba bila kuchoka kwamaana hujui siku wala saa.
Mwombe Mungu na si vinginevyo
 
wafilp 4:6 ."msijisumbue ktk neno lolote Bali katk kila neno kwa kuomba kusali pamoja na kushukuru"OMBA KWA AJIRI YA TANZANIA USICHOKE MUNGU ATAJIBU MAOMBI YAKO.
Kwa sasa nimeyaelekeza maombi yangu kuiombea Tanzania isiangamie.
 
Mkuu endelea kuomba. Mungu hujibu kwa wakati wake. Na miaka mifano kwa Mungu ni kama siku moja tu! Kuwa na subira!
 
Siwezi kumuombea Mwanasiasa hata siku moja, bora niombe kwa ajiri ya familia yangu, na kwa jamii kwa ujumla.
 
Alipochaguliwa tu alitusihi Watanzania wote bila kujali itikadi zetu, makabila yetu na dini zetu tumwombee, kwa kile alichosema alichokikuta kule kilihitaji maombi.

Kweli kama Mtanzania nilianza maombi ya nguvu, nilitenga siku moja ya mwezi kufunga kwa ajili yake nikijua kazi aliyonayo ni ngumu na ya hatari.
Pamoja na kufanya hivyo, leo takriban mwaka unakwisha bila kuona faida ya maombi yangu. Maisha ndiyo yamezidi kuwa magumu afadhali ya mwaka jana.

Katika maombi yangu nilitegemea atakuwa rais wa wanyonge kama alivyoahidi.
Nilitegemea atakuwa rais wa vyama vyote, dini zote na makabila yote kama alivyoahidi. Nilitegemea rais atakuja kuwapata mikopo wanafunzi wote kama alivyoahidi.

Nilitegemea maombi yangu yatambadili na kutawala kwa haki kwa kufuata utawala wa sheria, rule of law. Nimesubiri ahadi yake ya ajira kwa vijana kama alivyoahidi, matokeo yake kaajiri vijana kwa kuangalia ukada na mbaya zaidi kaajiri vijana wenye ukakasi mbele ya jamii.

Matokeo ya maombi yangu ni kusitishwa kwa ajira, kunyanyaswa kwa watumishi wa umma kwa kisingizio cha kuhakiki wafanyakazi hewa.
Maombi yangu yamesababisha wafanyabiashara kunyanyaswa kwa kuongezewa kodi zisizo na ulazima.

Nilitegemea madawa yataongezeka mahospitalini, matokeo yake hata dawa ya chanjo kwa watoto imekosekana. Naona kama maombi yangu yanazidisha ugumu wa maisha kwa wananchi. Kwanini basi niendelee kuomba?

Kama mwaka jana niliishi vizuri, watoto walisoma bila kumwombea rais aliyekuwepo, ajira zilikuwepo wafanyakazi walipanda madaraja bila kumwombea rais aliyekuwepo, wanafunzi walipata mikopo tena wote bila kumwombea rais aliyekuwepo, kuna sababu gani basi kuendelea kumwombea aliyepo?

Nimestisha maombi.

Ni uamuzi wangu sijashinikizwa na mtu.

Quinine.
Wewe ulikuwa lofa nanialikuambia shetani ukimwombea mema kwa mungu atapokea shetani aombewi mema bali maovu hivyo usiache kumwombea kwa mungu siku zote daima dumu
 
Hata usipomuombea wewe,wengi tunaompenda mungu anapokea maombi yetu
Nyie muombeeni mbowe azidi kutafuna ruzuku
Alipotuomba tumwombee mbona hakuchagua, wewe ndio unaanza kubagua watu wa kumwombea.
 
Jambo litarajiwalo linapo chelewa moyo huugua. Tuwaombee viongozi wetu, tusikate tamaa tuwaombee, bwana , awajalie viongozi wetu hekma na busara katika utendaji wao.
 
Alipotuomba tumwombee mbona hakuchagua, wewe ndio unaanza kubagua watu wa kumwombea.
si umeondoa mwenyewe?kwenda,sie tunasonga mbele,kamuombee mbowe azidi kuchota milioni 150 kwa mwezi bila kushtukiwa
 
Back
Top Bottom