Nimeshtuka baada ya kuiona Dodoma, kwanini imeitwa jiji?

Nimeshtuka baada ya kuiona Dodoma, kwanini imeitwa jiji?

Dodoma makao makuu ipo kisiasa zaidi kuliko hali halisi ya sasa kwa wakati ule wa Nyerere kiusalama na kiutawala ilikuwa ni sahihi, lkn sio sasa sababu ya maendeleo ya technologia,ikiwemo mawasiliano, kufunguliwa ofisi za kikanda kwa ajili ya kusogeza huduma kwa wahitaji,kwa sasa ni rahisi sana kufika dar kutokea popote kuliko kufika Dodoma kama utatumia usafiri wa ndege
 
Sifa kubwa ya majiji yote duniani ni mpango mji unaotekelezeka, usimamizi madhubuti ukianikizwa na usafi wa mazingira. Dodoma tangu mwanzo ina mpango mji ambao haukuwahi kusimamiwa vizuri. Kwa kuwa sasa uamuzi wa kuhamia Dodoma umeishaanza kutekelezwa, tutegemee kuona mabadiliko ya mji wa Dodoma katika kipindi cha miaka mitano hadi kumi ijayo.
 
mbona Tanga ni hivyo tu, mfano pale mabanda ya papa nyumba za udongo zipo,kwa minchi ndo usiseme, kuanzia barabara ya 12 nyumba za zamani. Vijijini ndo balaa ni tofauti na kilimanjaro (wachaga wanajenga sana nyumbani). Maji bombani yanatoka machafu yenye vumbi(hii ni kawaida ukija Tanga usishangae). Baiskeli mpaka mjini tena ndo boda boda, ukivuka barabara utasubiri gari ipite, bajaji ipite, pikipiki ipite na baiskeli ipite ndo uvuke.
Usiku usishangae ajali za baiskeli maana ni nyingi na hazina taa.
Kwenye traffic light usishae kukuta mpaka baiskeli na pikipiki zinasubiri green light
Lakini Tanga ndo mkoa mzuri wa kutumia private car maana hakuna foleni barabarani
Aiseee kweli TZ bado Sana, mkuu ukiangalia stendi ya mabasi ya jiji la idodomya utacheka kabla ilikuwa katikati ya mji lakini kwa sasa wanaipeleka nanenane ni mbali Sana na mji hakuna miundombinu bora mfano stendi mpya ni vumbi kama upo wilayani.
 
Aiseee kweli TZ bado Sana, mkuu ukiangalia stendi ya mabasi ya jiji la idodomya utacheka kabla ilikuwa katikati ya mji lakini kwa sasa wanaipeleka nanenane ni mbali Sana na mji hakuna miundombinu bora mfano stendi mpya ni vumbi kama upo wilayani.
Nasikia wakazi wa dodoma bado hawana uwezo wa kumiliki nyumba bora (sehemu nzuri ya kisasa yakuishi) nyumba zilizopo ni mali ya serikali. Nyumba za taasisi ila maeneo wanayoishi watu bado sana
 
Miongoni mwa kigezo cha mji kupandishwa hadhi na kuwa jiji ni upatikanaji wa "public toilet" vyoo vya jamii vya kulipia, swali kwa mtoa mada hivi kwani dodoma hakuna public toilet??
 
Huyu mpuuuzi anadhani magorofa na road reserve ndio zinafanya mji unapewa hadhi ya jiji. Elimu iko kiganjani mwago. Henu google na utaona ni kwanini Bukoba sio jiji.
Acha ushamba dogo
 
Naombeni nitoe Ushuhuda wa Safari yangu hii ambayo niliianza juzi j5 hadi hivi leo ndio natoka hapa Dom ila WHY DODOMA KUITWA JIJI??? Nimepata shock sana wazee wa tafakuri ya JIJI sio kwamba alisema jiji amekosea ila HADHI ya jiji wote tuliowahi kutembelea majiji makubwa barani Africa tunalifahamu nini maana ya neno JIJI.
Sasa naomba niwape nilichokiona mimi pale DOM aisee hata kama wakoloni walisema pale ndio katikati ya Tz basi sawa ila sio kila katikaki ya NCHI lazima pasimikwe kuwa jiji,

Sijaona vitu hivi vinavyotambulisha JIJI

[emoji117] Barabara za lami za viwango?

[emoji117] Maghorofa mwanzo hadi katikati ya mji?

[emoji117] Mataa ya kuongozea magari ya kutosha?

[emoji117] Road reserve ya kutosha?

[emoji117] Pale Bungeni taa zake hazitoshi kabisa na
tena zingine haziwaki kabisaaaaa??

[emoji117] Maeneo ya kuingilia pale Bunge mkono wa
kushoto kutoka Dar maeneo yake ni
machafu, Nyasi zinatunza hadi Nyoka.

[emoji117] Vumbi na Baridi kwa kipindi hichi ni baadhi
ya mada nyongeza tu.


Naombeni nanyi mloyaona pale panapoitwa JIJI tujuzane hapa maana najua viongozi wa Serikali hapa wapo watasikia hichi kilio chetu wanaTanzania.....

kiben10 wa Zinjathropus wa History F2
Ni jiji kwa serikali ya kijamaa ya CCM, ingekuwa bunge lipo jijini Dar maazimio ya kipuuzi yasingekuwa yanapitishwa, maana wabunge wangekuwa wanafungiwa ndani au kupigwa wakitika, ila serikali imepelekwa porini Dom ili wajiamulie chochote wanachotaka, na mazuzu ya Dom hawajui cha kufanya
 
Akili za jamaa ako Jiwe. Aantaka akiondoka akumbukwe

period!
 
Back
Top Bottom