Nimeshindwa kutoa jibu mchango wenu tafadhali!

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Ni mwaka wa tatu toka afunge ndoa na mumewe, mumewe ni Dereva
kwenye kampuni ya......... (Naistiri) amepatwa na ugonjwa wa kupararaiz
mwaka jana. Baada ya jitihada kubwa za madaktari kwa sasa angalau
anaweza kutembea umbali mfupi, lakini kwa upande wa tendo la ndoa ndio
basi tena.
Anacholalamika mkewe ni kwamba mumewe amekuwa anamtuhumu
na kumtukana kila siku kuwa ana wanaume wengine huko nje, matusi na kero
za huyu mwanaume zimezidi ndo akafikia kuniuliza hili swali afanyeje? aachane nae?
Kinachomkera zaidi ni hayo matusi na kelele za kutuhumiwa mara kwa mara

SWALI LANGU SI LA HUYO MAMA.
Katika hali kama hiyo ya mwanaume kushindwa kufanya tendo la ndoa na Juhudi
za madaktari zimeshindikana mwanamke unafanya nini haliyakuwa bado damu
inachemka na pingu za maisha mshafunga......... Dada zangu nijibuni.
AMANI KWENU
 
Aku anipishe mie...sikutoka kwetu kufata ugali. hawezi kazi simply akae kando, kama damu inachemka kwanini nizeeke kwa kutamani ikiwa yeye hawezi. Domo chafu...kazi hawezi kipi kiniweke?
 
Kwani kusex lazima? Mbona watu tunamiaka kadhaa na tupo fresh bana
watu wangapi hawafanyi
aliapa kifo ndo kitakachowatenganisha
kukosa sex ndani ndo kifo?
Mwambie atulie
 
Siku ya ndoa waliapa kupendana katika shida na raha na kuvumiliana katika magonjwa ..... Nadhani inabidi huyo mama naye aamue kustaafu kabla ya muda wake, kwani hiyo ndiyo maana hasa ya kupendana katika shida na raha.
 
Mpe pole huyo mdada na mwambia ajaribu kumchukulia huyu mumewe,aelewe kua sio rahisi kwa mwanamme wakisawa sawa
ghafla paka wake hawezi kukamata panya,amtafutie mda muafaka amueleze kwa upole na upendo,mwambie ajikaze kwani alipofunga nae ndoa aliyakubali yote kwa raha na dhiki kwa uzima na maradhi sasa huu ndio mtihani wake,na inshallah mwenyezi mungu atamjalie mumewe afya na yeye azidi kumuombea hakuna kubwa kwa mwenyezi mungu.
 
This

Kwani kusex lazima? Mbona watu tunamiaka kadhaa na tupo fresh bana
watu wangapi hawafanyi
aliapa kifo ndo kitakachowatenganisha
kukosa sex ndani ndo kifo?
Mwambie atulie
and this

Siku ya ndoa waliapa kupendana katika shida na raha na kuvumiliana katika magonjwa ..... Nadhani inabidi huyo mama naye aamue kustaafu kabla ya muda wake, kwani hiyo ndiyo maana hasa ya kupendana katika shida na raha.

Viapo viapo...jamani kweli hili lipo, sasa kama kuna hiki kiapo cha uvumilivu kwenye shida na raha sasa na kunyanyasani ni nini. Angekuwa na ustaarabu wa kauli labda ingenipa moyo wa kukaaa. My conclcusion is I don't want to be the victim wa hiki kiapo pia with emotional abuse!
 
ndugu hiyo ni moja ya kupanda na kushuka kwenye maisha ya ndoa, Amwombe Mungu ampe uvumilivu
Kwa upande wa huyo jamaa ashike adabu maana kama ingekuwa mke ndo kaparalize ndani ya siku tatu jamaa ungekuta lishaanza sarakasi na vioja kwenye hiyo ndoa, ungekuta lishamaliza mtaa kwa uchu
 
Aku anipishe mie...sikutoka kwetu kufata ugali. hawezi kazi simply akae kando, kama damu inachemka kwanini nizeeke kwa kutamani ikiwa yeye hawezi. Domo chafu...kazi hawezi kipi kiniweke?
Duh, kwa hiyo ungemkimbia? au ungekuwa naye halafu unacheza Offside Trick?
 
Aku anipishe mie...sikutoka kwetu kufata ugali. hawezi kazi simply akae kando, kama damu inachemka kwanini nizeeke kwa kutamani ikiwa yeye hawezi. Domo chafu...kazi hawezi kipi kiniweke?
Sasa nimeelewa maana ya SIGNATURE yako hapo chini.
 
this

and this

viapo viapo...jamani kweli hili lipo, sasa kama kuna hiki kiapo cha uvumilivu kwenye shida na raha sasa na kunyanyasani ni nini. Angekuwa na ustaarabu wa kauli labda ingenipa moyo wa kukaaa. My conclcusion is i don't want to be the victim wa hiki kiapo pia with emotional abuse!
kiapo cha ndoa ni gambling kama insurance. Pata poteza lolote laweza tokea inabidi ukubali matokeo
 
ndugu hiyo ni moja ya kupanda na kushuka kwenye maisha ya ndoa, Amwombe Mungu ampe uvumilivu
Kwa upande wa huyo jamaa ashike adabu maana kama ingekuwa mke ndo kaparalize ndani ya siku tatu jamaa ungekuta lishaanza sarakasi na vioja kwenye hiyo ndoa, ungekuta lishamaliza mtaa kwa uchu
Labda angeheshimu kiapo cha shida na raha.
 
Pole kwa huyo dada. Mwambie mume wake yuko kwenye wakati mgumu kunakopelekea awe na tabia hiyo. Aongee nae kwa upole na kumthibitishia kua hatamsaliti kwa hali yoyote ile na pia asimpe sababu za kuanza kumshuku maana ndio itaharibu kabisa.
 
Kweli kama alivyosema Kbd hapo kwenye red, inawezekana huyu dada ndo anajenga mazingira ya kutoaminiwa na mumewe. We dada jitahidi kuwa nomo!
 
  • Thanks
Reactions: Kbd
Aku anipishe mie...sikutoka kwetu kufata ugali. hawezi kazi simply akae kando, kama damu inachemka kwanini nizeeke kwa kutamani ikiwa yeye hawezi. Domo chafu...kazi hawezi kipi kiniweke?
kilicho mkuta huyo mume ashum kingekukuta wewe...afu mwenzio anakujibu km unavyojibu wewe....UNGEJISIKIAJE?:ballchain:
 
kiapo cha ndoa ni gambling kama insurance. Pata poteza lolote laweza tokea inabidi ukubali matokeo

I am sorry if we are on different chapter, I don't want to believe marriage ni KIAPO for me I see as CONTRACT and any reason could lead to this contract to end/terminate. Mimi kama mimi, if I have my reasons for which in here ni UNYANYASAJI and my belief allow me to ...why suffering!
 
Sina cha kusema...
Ila huyo mdada mpaka amefikia kukwambia yote hayo...wex ni mshauri(ur prof'sion) na kama laa...
Basi ingekuwa simple kumbeba...
Mumewe anamjua na ndo mana anamgombeza...
Kama kwel ameweza miaka 3 ,hawezi shindwa mmoja mbele..
Aache kusingizia damu,yeye mwenyewe anastawisha Moyo wa tamaa na usaliti..
Hakuna mwanamke hapo..
Miaka mitatu si digree ya kawaida tu,vuta picha mmewe angepata nafasi ya kwenda kusomea nje ya nchi na fani ya udaktari..miaka 5-7..
Damu ingekuaje..
Mim nadhani wakati wa shida ndiyo wakati wa kumwonyesha mwenz wako Unamthamini na kumjali kiasi gani..
 
kiukweli hata ingekukuta wewe ungejisikia vibaya na hali hiyo,na always ungefikiri km jamaa anavyofikiri.kumbuka uliapa kwa shida na raha...sasa wewe unaetaka raha tu hapo ndo kipimo chako shida imefika,kukimbia sio suluu.......ningekuwa mimi mshikaji simuachi na hata km nacheat huko sitofanya mpk ajue,na heshima yake kama mume naiweka palepale....hayo makelele ofcoz inawezekana demu anaonyesha dharau kwanini asiseme?
 
Back
Top Bottom