Nimeshindwa kumsoma!!!!!

Mcheza Karate

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
690
350
Wadau, wakati nipo chuo nilikutana na mrembo mmoja tukiwa mwaka mmoja lakini vitivo tofauti, tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi, tulipomaliza chuo mwaka jana tukawa tumepangwa vituo vya kazi ktk mikoa tofauti, lakini tukawa tunawasiliana huku kila mmoja wetu akimpa hope mwenziwe kuwa ndio wake wa maisha, lakini juzi nilimtaarifu kuwa naenda kwake(Iringa) ambako ndo kituo chake cha kazi kilipo, akanijibu kuwa ana safari hivyo nisije. Nikawa kichwa nazi nikaja jana, nikampigia simu akaja hapa hotelini nilipofikia, nikaanza kukagua simu yake ya mkononi ili nijiridhishe lakini nilikuta message za mapenzi kama za wanaume 6 tofauti huku message yangu hata moja hamna, zote kafuta. Nilipomuuliza kuhusu safari kajibu kuwa "pole sana kwa yote". Nimeshangaa zaidi jana alivyokuwa anarudi kwake jioni ile hakuthubutu hata kunikaribisha kwake, leo asubuhi kaja hapa chumbani(hotelini) asubuhi tangu saa 4 analia tu hadi muda huu huku hatoi hata neno moja kila nikimuuliza sababu ya kulia huku hata mimi akinitia woga, kajibu tu "sistahili kuwa hata mbwa wako, mi sikufai, pole kwa ukatili niliokufanyia". Je wadau huyu binti nimfanyeje? Na mimi nimependa?
 
Maswali mengne munayotuuliza wana Jf hayana tija,wewe mtu hajakwambia kinachomliza unataka ushauriwe,ushauriwe nini?alafu umesoma hadi chuo zen una kazi alafu unauliza vitu visivyoeleweka!
 
Sasa anakulilia ili iweje?Mwambie kama hastahili aende na njia zake.
 
  • Thanks
Reactions: mka
Wengine mahusiano ya mbali hawayawezi, mkalishe chini muongee na mnaweza kufikia muafaka
 
ebwana weee mapenzi ya mbali ni usanii tuu....wewe just chachua ya mara ya mwisho na sepa.
 
naamini kwa maneno yake hayo,inaonekana amekusaliti,kimapenz. anakuchanganya pamoja na wengine.
kama una roho ngumu, endelea naye
 
Je wadau huyu binti nimfanyeje? Na mimi nimependa?

Kwa vile bado unampenda tukikushauri umwache utasema tunakuonea wivu. Hafafu thread yako utata mtupu. Kwenye heading unasema umeshindwa kumsoma, lakini kwenye maelezo unadai kwenye simu yake umekuta messages za mapenzi toka kwa wanaume kama sita tofauti na kwamba kulikuwa hakuna messages zako hata moja. Sasa hapo umeshindwa kumsoma nini? Kama namna gani vipi tafuta miwani ili uweze kumsoma vizuri. Natumani umenielewa.
 
ebwana weee mapenzi ya mbali ni usanii tuu....wewe just chachua ya mara ya mwisho na sepa.

Achakachue aondoke na viwavi jeshi kabisa yaani jitu lina misume sita yote yake!!!!!!

Huyo demu ameshasema hakufai kwa sababu anajijua anayotenda na aliyotenda hivyo chukua ushauri wake na mfariji tu ili muachane kistaarabu.

Mademu wa aina hiyo hawafai hata kwa kulumangia kwa kachumbari, jikaze najua ni ngumu kufanya deviation ya mapenzi kw mtu unayempenda haraka kama ninavyofikiri lakini ukweli ndiyo huo.
 
'Hivi kila nnachofanya mbona kinabuma, aaah eh kichwa kinauma' *in Chege's voice*

Mwana kesho tafuta namna ya kuenjoy xmass au chukua ndinga sepa. Hapo huna lako.
 
Wadau, wakati nipo chuo nilikutana na mrembo mmoja tukiwa mwaka mmoja lakini vitivo tofauti, tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi, tulipomaliza chuo mwaka jana tukawa tumepangwa vituo vya kazi ktk mikoa tofauti, lakini tukawa tunawasiliana huku kila mmoja wetu akimpa hope mwenziwe kuwa ndio wake wa maisha, lakini juzi nilimtaarifu kuwa naenda kwake(Iringa) ambako ndo kituo chake cha kazi kilipo, akanijibu kuwa ana safari hivyo nisije. Nikawa kichwa nazi nikaja jana, nikampigia simu akaja hapa hotelini nilipofikia, nikaanza kukagua simu yake ya mkononi ili nijiridhishe lakini nilikuta message za mapenzi kama za wanaume 6 tofauti huku message yangu hata moja hamna, zote kafuta. Nilipomuuliza kuhusu safari kajibu kuwa "pole sana kwa yote". Nimeshangaa zaidi jana alivyokuwa anarudi kwake jioni ile hakuthubutu hata kunikaribisha kwake, leo asubuhi kaja hapa chumbani(hotelini) asubuhi tangu saa 4 analia tu hadi muda huu huku hatoi hata neno moja kila nikimuuliza sababu ya kulia huku hata mimi akinitia woga, kajibu tu "sistahili kuwa hata mbwa wako, mi sikufai, pole kwa ukatili niliokufanyia". Je wadau huyu binti nimfanyeje? Na mimi nimependa?

Inaonyesha wewe hutaki kukubaliana na ukweli uliodhahiri...usikute mwenzio keshazoa gonjwa somewhere sasa guilty consciousness imemtawala na inamuwasha moyoni ndo maana analia na pengine anajutia...TAFAKARI KISHA UFANYE MAAMUZI!!
 
wewe wa kipekee msg za wanaume 6 tofauti halafu unauliza ufanyaje? Huogopi maradhi?au hujipendi?
 
Sampuli ya wanawake wa hivyo husababisha ikufike siku ukawasha torch ya simu yako umulikie kuitafuta simu hiyohiyo uliyonayo mkononi ! Hafai msikitini ! Hafai kanisani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom