Nimeshikwa pabaya - wakuu naomba msaada tutani!

Deodat

JF-Expert Member
Sep 18, 2008
1,274
272
Mimi niko hapa ughaibuni (nchi kapuni - for security reasons), kama wengi mnavyojua mara nyingi ukiwa nje ndugu, jamaa na marafiki kule nyumbani bongo huwa wanaomba kila siku ‘uwavute’ nao waje huku. Mwaka jana rafiki yangu kipenzi (tumesoma pamoja tangu shule ya msingi mpaka chuo kikuu pale mlimani) aliniomba nimsaidie kumfanyia mpango mkewe aje hapa kufanya masters degree, nilijitahidi kwa nguvu zangu zote hata kuingia gharama nyingi na hatimaye shemeji yangu kipenzi akafika hapa.

Hapa tulipo sio mji mkubwa sana, una watu elfu 25 tu na watanzania tuko wachache sana na tunafahamiana kwa kiasi kikubwa. Mara nyingi huwa tunakutana na kupiga soga, kunywa na kula pamoja huku tukikumbushana haya na yale hasa kuhusu nyumbani. Hatuna chama rasmi cha watanzania lakini tunashirikiana vizuri sana ila tumekubaliana hatutaanzisha chama kwakuwa mara nyingi mkishakuwa na vyama ndio majungu na ufisadi vinaanza na pia tumekubaliana hatutafungua tawi la nje la chama cha siasa (hasa CCM) labda Chadema tutafikiria.

Stori iko hivi: Katika sisi watanzania tulio hapa kuna jamaa mmoja yeye ni mkongwe hapa, ameeishi kwa miaka saba sasa, ameajiriwa na kitengo kimoja cha serikali kama Strategic Analyst (ana pesa nzuri tu) na ni mtu mkarimu sana kiasi kila mtanzania anayefika hapa huwa anamu-appreciate sana jamaa. Huyu jamaa hana mke, sasa shemeji yangu alipofika nilimtambulisha kwa watanzania wengine akiwepo huyu jamaa, wakazoeana sana, siku za mwanzo nilijua ni kawaida tu lakini baadae niligundua wameanza mahusiano na kwa hivi sasa napoongea shemeji keshahama hostel anaishi kwa jamaa, wanapika na kupakua.

Hicho kitu kimeniumiza sana hasa ukifikiria ni mke wa rafiki yangu. Kwasababu alijua anachokifanya, shemeji sasa ananionea aibu sana kiasi kwamba hata nikimpigia simu hapokei. Wakati naendelea kutafakari nini cha kufanya, nikapokea simu kutoka kwa huyo rafiki yangu (mwenye mke) akinituhumu kuwa mkewe kamtaarifu kuwa mimi nimemtongoza na nataka niwe na mahusiano naye kimapenzi, kwakuwa jamaa anamuamini sana mkewe na anampenda mno, amefedheheshwa sana na taarifa hizo hasa ukizingatia sisi ni marafiki wa siku nyingi, jamaa ameapa ‘kunichinja’ siku tukionana. Nimejaribu kumuelewesha jamaa haelewi.

Wandugu nifanyeje?

(Samahani sana kwa kuweka stori ndeeeefu lakini ilibidi nifanye hivi ili issue iwe clear kidogo)
 
Aisee pole sana haka ndo katabia ka wanawake wengi. Akishakuwa anachukuliwa na jamaa halafu ukamdokeza mmewe, ili kukukata makali atamwambia kwamba ulimtongoza akakukatalia ndo maana umeamua kumsemea hivyo. Hata mimi yamenikuta ndugu yangu wapo hivyo hawa wamama. Huyo shemeji yako ameona afanye hivyo ili kukugombanisha na mmewe na kukunyima nafasi ya wewe kumueleza yanayojiri huko ulaya. Namna pekee ni kunyamaza kimya, wala usitafute hata kuonana na huyo mama, vinginevyo ni kweli rafiki yako atakuua. Pole sana, jitenge na rafiki yako as well as huyo mama. Wala usijisumbue kumuelekeza mmewe kuhusu anayoyafanya huyo mama huko ulaya.
 
ai kumbe ulijitwisha jukumu la kupokea mke wa mtu huko wakati mumewe yuko bongo!
 
Huyu mwanamke hana adabu hata kidogo ooh my ...
Hata hakuonei haya Shemeji yake kaamua kujikabidhi mzima mzima ..hebu muulize kama bado anampenda mmewe?
 
mwalike rafiki yako aje kukutembea na ili amfanyie mkewe surprise ya Xmas:confused2:.
 
kaka mbona hiyo issue simple tuu..fanya hivi..mtumie jamaa nauli na mualiko ili imuwie rahisi kupata visa ya kuja huko kisha andaa vijisent vya kumuweka hapo ughaibuni just for 1 month...TRUTH NEVER LIE...JUST LIKE A BULLET...atayaona mwenyewe na pia itasaidia kunusuru urafiki wenu wa muda mrefu... USIHOFIE SANA VITISHO VYAKE VYA KUKUUA...mwisho wa siku atakuheshimu na kukuamini wewe na sio mwanamke...(ladies mnisamehe nimeadhiriwa na mfumo dume)
 
kaka mbona hiyo issue simple tuu..fanya hivi..mtumie jamaa nauli na mualiko ili imuwie rahisi kupata visa ya kuja huko kisha andaa vijisent vya kumuweka hapo ughaibuni just for 1 month...TRUTH NEVER LIE...JUST LIKE A BULLET...atayaona mwenyewe na pia itasaidia kunusuru urafiki wenu wa muda mrefu... USIHOFIE SANA VITISHO VYAKE VYA KUKUUA...mwisho wa siku atakuheshimu na kukuamini wewe na sio mwanamke...(ladies mnisamehe nimeadhiriwa na mfumo dume)


Walaaa ucjali umetoa ushauri mzuri sana na hauingiliani na mfumo dume
 
Achana nao wote kaa kimya ukweli ataujua tu siku hizi dunia ni kijiji na mapenzi ni upofu kuna siku atajua tu kuna msemo wa kiswahili unasema "mficha moshi, moto utamuumbua" wewe wala usipaniki kata kabisa mawasiliano na wote na muombe Mungu akuepushie na hasira, woga na ugomvi

nakwambia kuna siku isiyo na jina huyo jamaa atakuomba msamaha na kukupigia magoti akishajua kitu gani kilikuwa kinaendelea mkewe alipokuwa nje

(fuata huu ushauri nimeutoa mbali sana kusini kabisa ya medula oblangata)
 
Back
Top Bottom