Nimeshikwa na Taharuki

Nimeshikwa na Taharuki

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,801
Reaction score
43,177
Habarini za jioni,

Wengi wenu JF wanafahamu Kasie si mdau wa siasa, imetokea tu nipo mahali nikajikuta nashuhudia hii habari ya Mh. Sumaye kurudi CCM. I was like what the hell is going on!

Mchana wa leo nimeshuhudia Mheshimiwa Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu Bw. Fredrick Sumaye akipokea kadi ya CCM huko Dodoma huku amevaa vazi la CCM.

Akili ya Kasie ikaniambia, huyu baba ni mmoja wa waliotumwa kwenda CHADEMA kuvuruga?

Ina maana CHADEMA ilikuwa ni tishio kiasi hicho? au watu wanafata maslahi? na kama wanafata maslahi inamaana CHADEMA pia kulikuwa na maslahi na sasa yameisha na wanarudi CCM?

Hivi hata mtu aliyefika nyadhifa za juu bado anatafuta maslahi huku na huko?

Kama ndivyo mbona hakuna wanaotoka vyama upinzani na kwenda kuvuruga CCM kisha warudi CHADEMA? au wapo ila nilipitwa.... yaani najiuliza maswali halafu nakosa majibu khaaaah...

Nimejikuta nakumbuka usemi wa, ukianza kula nyama ya mtu huachi kamwe.... na ukianza kuhama hama makanisa, huachi kamwe, na huku kuhamahama vyama vya siasa jee.

Acha nirudi kwenye kada yangu ya Mahaba.

Kwaherini na muwe na siasa njema maana hata sielewi.

NB: Natumai mnajihadhari na mlipuko wa gonjwa la Covid19 linalotikisa dunia tangu mwaka jana mwishoni. Naomba niendelee kusisitiza, msiache kunawa mikono, kutokutoka nje ya nyumba yako / ofisi iwapo mtoko huo sio lazima.

Na unapokuwa eneo la mjumuiko kilazima basi jitahidi kuwa walau mita moja mbali na binadamu mwingine na kutogusagusa mahala mahala (surfaces), bila kusahau kunawa mikono na sabuni kila mara kwa maji yanayotiririka. Sanitaiza iwe mbadala wa maji na sabuni.

Kasinde.
 
Aliambiwa sumu haionjwi kwa ulimi mkuu, wewe hapo ungebaki?
Na ukute alizoea kuonja vitu kadhaa kwa ulimi, mfano labda uviza kule.
 
Umeandika;
'Wengi wenu JF wanafahamu Kasie si mdau wa siasa, imetokea tuu nipo mahali nikajikuta nashuhudia hii habari ya Mh. Sumaye kurudi CCM...... I was like what the hell is going on...!! ''

Unashangaa Sumaye kurudi CCM? Ulishangaa alipojiunga CHADEMA?

Nilishangaa kidogo na sikuweka uzi sababu niliona ni mpenda mageuzi kwelikweli na kwenda kwake Chadema nilikuchukulia kuwapa support, ujuzi au siri ndogondogo zinazotumiwa an CCM ili washinde ukizingatia yeye alikuwa CCM miaka kadhaa na sikuhofia kama alifata maslahi maana kufikia kuwa na wadhifa wa Waziri Mkuu wa nchi una nafasi ya kupata vingi tuu.

Ila tangu waliohama CCM na kuhamia Chadema badala ya kufanya Chadema kisonge mbele badala yake kimerudi nyuma na kuvurugwa na kuchanyatika ukijumlisha na Zito bin kuhamia ACT bin Slaa kukimbia nchi na mapicha picha ya kila rangi....

Nashangaa sababu wakati huu ndo Chadema kinahitaji msaada ili walau nacho kisimame kifua mbele kupambana na uchaguzi, badala yake wanahama na kurejea walikotoka...
 
Kasie,
Mpenzi unazidi kujizeesha tu njoo nikupeti huku ule raha chichiem itakufanya ushindwe hata kutembea waachie siasa zao nasi tule mapenzi yetu au unasemaje kipengo wangu..?
 
Naona siasa n mchezo ambao ukiuingia unashindwa kuacha, hua nashindwa kuelewa kwann wazee kama wale ambao washakua na nyadhifa kubwa wanajidharirisha? Nawaza tu ukiona umezinguliwa chama chako kaa nyumban fanya mambo mengine pamoja na kulea wajukuu.
 
S

Sumaye/ Chadema alifukuzwa kama kuku.

Aiseeeh, basi nimepitwa ni vile si mfatiliaji wa siasa, lakini hiyo inanifanya nijiulize tena... mwanzoni aliondoka CCM kwenda Chadema ili afanyaje? lengo lake lilikuwa ni nini?

Kama angefika Chadema na kuwapa mawaidha namna ya kuenenda kama back up wangemfukuza?

Na kama hawakumsikiliza badala yake walimtumia na kumkera si angeondoka mwenyewe kabla ya kufukuzwa? Dalili ya mvua si inaonekana?

Well kuna akili inaniambiaga iko siku tutakuja kusikia Mbowe amehamia CCM.....!! sijui kwanini.
 
Aliambiwa sumu haionjwi kwa ulimi mkuu, wewe hapo ungebaki?
Na ukute alizoea kuonja vitu kadhaa kwa ulimi, mfano labda uviza kule.

Sasa alifanya nini hata aambiwe maneno ya kutishia amani hivyo? Au kuna kitu gani alitaka kufanya hata wamwambie hivyo? Kama hakuwa na nia mbaya si angejitetea na kujitakasa tuu???

Kwani CCM alionja sumu gani? nazidi kupata maswali yasiyo na majibu...
 
Mpenzi unazidi kujizeesha tu njoo nikupeti huku ule raha chichiem itakufanya ushindwe hata kutembea waachie siasa zao nasi tule mapenzi yetu au unasemaje kipengo wangu..?

Aahahahahaha Kenzyy, hapa Dadii ameshanibembeleza hadi nimepoa maana mchana ndo nilikuwa mwekunduuuu kwa hasira, japo sina chama chochote wala si mshabiki wa siasa ila kuna mambo ukiyasikia najikuta tuu nahemka yaani....

Asante sana kwa kujitolea kunipoza Kenzy, uendelee na moyo huohuo usikate tamaa eehehehee.

Kasie Matata.
 
Naona siasa n mchezo ambao ukiuingia unashindwa kuacha, hua nashindwa kuelewa kwann wazee kama wale ambao washakua na nyadhifa kubwa wanajidharirisha? Nawaza tu ukiona umezinguliwa chama chako kaa nyumban fanya mambo mengine pamoja na kulea wajukuu.

Kabisa yaani, wangekuwa wanafanya kama unavyosema naona vyama vya siasa vingekuwa na utulivu wa hali ya juu na hata vijana wanaongia kwenye siasa wangejifunza mema kutoka kwao.
 
Kweli hujui kitu afadhali ukaendelee kuwafunda vijana juu ya utamu uliopo pale kati na namna ya kuurina.

Sent using Jamii Forums mobile app

Asante kwa angalizo, kiukweli napitwa na mengi tuu yanayoendelea kwenye siasa sababu kama machache nnayojikuta nayafahamu yananipa hasira na mihemko je ningejua yote si ningekuwa mtu wa kulipuka kila leo...??

No wonder kwenye siasa watu huwa wanajibizana kwa maneno ya kejeli na matusi.
 
Back
Top Bottom