Nimeshikwa na Taharuki

Nimeshikwa na Taharuki

Kasie,
kweli wewe sio mtu wa siasa ila huko ulikochagua kwenye mahaba kama panakufaa hivii, sasa kuhusu alichokifanya mh. Sumaye huku kwenye siasa wanaita DEMOKRASIA, na mh.hajakosea chochote ila ametumia haki yake vizuri.
 
Kasie,
Niendelee na moyo huu huu wakati sipewi kitu😜
Hata siku moja si mbaya ntakuwa nakata shurubati la kiwewe kwenye uno lakizee ila lakinyamwezi😋

Nakuapia utasahau hata ukiulizwa mwanasiasa hata mmoja hutamkumbuka ila utakumbuka kenzy ndie mtima wa nyongo,moyo na shina la huba lililojipandikiaza ktk viini vya kila mishipa yako😂

Wewe sio wa kufata nyuki ule asali,wewe ni wakufuata mzinga ule asali nyuki walishakuuma karne hizo now watakiwa kula hao nyuki na asali yake kipengo wewe😜
 
Mweeeh inabidi nitafute darasa la elimu ya siasa nipunguze mkanganyiko nilionao...

Hapo uliposema amefanya kitendo cha kidemokrasia nikilinganisha na tafsiri ya demokrasia ndo nazidi kujichanganya.

Mahaba na Kasie ni damu damuu kama ngozi na nyama, bila kimoja wapo aidha unabaki ngozi na mifupa ila si uchi au ubaki na nyama na mifupa ambapo unakuwa uchi...
 
Sumaye kanipa uhalisia wa Ufipa kulivyo.
 
Niendelee na moyo huu huu wakati sipewi kitu😜
Hata siku moja si mbaya ntakuwa nakata shurubati la kiwewe kwenye uno lakizee ila lakinyamwezi😋
Nakuapia utasahau hata ukiulizwa mwanasiasa hata mmoja hutamkumbuka ila utakumbuka kenzy ndie mtima wa nyongo,moyo na shina la huba lililojipandikiaza ktk viini vya kila mishipa yako😂

Wewe sio wa kufata nyuki ule asali,wewe ni wakufuata mzinga ule asali nyuki walishakuuma karne hizo now watakiwa kula hao nyuki na asali yake kipengo wewe😜

Hujaacha tuu makeke yako khaaa.... nimejikuta nacheka tuu eehehehheee.
 
Kasie
Umesema urudi kwenye kada yako yamahaba af mwishoni unatuonya tusigusane. Are you serious? maha gani bila kugusana?
 
Kasie

Kweli kada yako mahaba,kitu tushasahaugi!! Mi mwenyewe nimetaharukika... unipe haba moja basi roho intulie kasinde
 
Hujaacha tuu makeke yako khaaa.... nimejikuta nacheka tuu eehehehheee.
Nikiacha mimi atakuambia nani...? Mtaje kama yupo niitoe roho yake kwa jisu lenye makali kuwili..

Makeke nimerithi kwa babu! Tena alinifundisha na maneno matamu nikiyamwaga hapa kihoro kitakutoka bure!
Mi ntakapokukuta salamu yangu kwako busu bunifu,busu lenye husuda na kiherehere cha mahaba! Busu ambalo ni ama ukae au unyong'onyee kwa utamu wake!!
Mi ndio ile shekeli itafutwayo,shekeli iliyoshiba madini inayopendwa na vigoli bikira.. Kama uliwahi sikia ule usemi usemao usiache mbachao kwa msala upitao basi mimi ndimi hiyo mbachao!!
Mimi ndio reli yako ikitoka treni hutoenda kokote..
Nivike kidani chako cha huba nikupe utamu wako mahabuba😉
 
Wanakatisha tamaa wenye nia ya kuwa wanasiasa kweli na kulitumikia Taifa hili kwa utii.
Eeenh, nimefuatilia staili yako..., kama mzahamzaha hivi, na kumbe ujumbe mahsusi unauwasilisha.

Staili hiyo sijaona ikitumika sana katika jukwaa hili la JF.

Kuhusu hao wanaohamia CCM, wote, ikiwa ni pamoja na Ngoyai na wale wabunge wanaosemekana kununuliwa - hapa hapana shida ya kuelewa nia zao zilikuwa nini.

Lakini kwa huyu Sumaye, kusema kweli amewashangaza wengi. Mimi nadhani kalainishwa na mitikisiko aliyopata, yale mashamba n.k. Mwisho wa siku akaona hakuna namna, na hasa ukichukulia kuwa matumaini aliyokuwa nayo CHADEMA nayo ndiyo hivyo, yakawa matumaini hewa. Ikabidi amwage manyanga.

Najua husomi taarifa ndefu, nikiangalia aina ya uchangiaji wako, kwa hiyo nisikuchoshe, ila nikuache na hili wazo usiku huu:
Hivi walioko CCM huko leo hii, wakijikuta CCM imekwishapigwa chini (hata kwa miujiza)..., (nilitaka kufanya liwe swali, lakini naona linaelea).
Hebu wafikirie hawa wanachama kindaki ndaki wanaokula tunda la taifa leo hii kwa wao kuwepo huko CCM, hali itakuwaje wakifurumshwa?

Bado sipati njia bora..., acha na ibaki hivyo, nikitumaini utanielewa!
 
hayahaya kumekucha..mwenye nyumba karudi mjini.

mliovamia mashamba ya sumaye mjiandae,halafu mjipange tena kisawasawa na kisaikolojia..

Lukuvii.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eeenh, nimefuatilia staili yako..., kama mzahamzaha hivi, na kumbe ujumbe mahsusi unauwasilisha.

Staili hiyo sijaona ikitumika sana katika jukwaa hili la JF.

Kuhusu hao wanaohamia CCM, wote, ikiwa ni pamoja na Ngoyai na wale wabunge wanaosemekana kununuliwa - hapa hapana shida ya kuelewa nia zao zilikuwa nini.

Lakini kwa huyu Sumaye, kusema kweli amewashangaza wengi. Mimi nadhani kalainishwa na mitikisiko aliyopata, yale mashamba n.k. Mwisho wa siku akaona hakuna namna, na hasa ukichukulia kuwa matumaini aliyokuwa nayo CHADEMA nayo ndiyo hivyo, yakawa matumaini hewa. Ikabidi amwage manyanga.

Najua husomi taarifa ndefu, nikiangalia aina ya uchangiaji wako, kwa hiyo nisikuchoshe, ila nikuache na hili wazo usiku huu:
Hivi walioko CCM huko leo hii, wakijikuta CCM imekwishapigwa chini (hata kwa miujiza)..., (nilitaka kufanya liwe swali, lakini naona linaelea).
Hebu wafikirie hawa wanachama kindaki ndaki wanaokula tunda la taifa leo hii kwa wao kuwepo huko CCM, hali itakuwaje wakifurumshwa?

Bado sipati njia bora..., acha na ibaki hivyo, nikitumaini utanielewa!

Wee kipindi cha uchaguzi 2015 kwa kiasi flani nilivutwa na sekeseke na ushabiki wa uchaguzi. Nilichoweza kujizuia ni kutokuwa kwenye chama chochote ili nisiumie moyo/roho yangu, nilikuwa ikishinda Chadema sawa ikishinda CCM sawa cha muhimu amani iwepo tuendelee kufanya kazi na usiku Mahaba kwama kawaida (kwa sie wazee mchana na asubuhi hatuwezi kumahabika).

Picha hilo la siku CCM ikifa wanachama kindakindaki itakuwaje niliiona ile siku ya kusomwa majina 5 bora ya kinyang'anyiro cha uraisi ndani ya CCM, joto lilikuwa kali aiseeh mle ukumbini baada ya mamvi kutokutajwa weeeh...... ukumbi mzima ulinyweaaaaaaaa nywiiiiiii na wakati wanaingia walikuwa wanaimba kwa nguvu zotee TUNA IMANIII NA LOWAASAAA OOYAAA OYAAA OYAAAA....aahahahahahaa walifurahishwa aiseeh na wengine walilazwa kwa presha wakati Lowasa mwenyewe alikuwa katulia tuliii.

Well siasa pia ina hatua na inakua kama mtia unavyomea, mipasuko na migawanyiko hutokea kwa sababu kadha wa kadha ila inapotokea uma kusapraiziwa ndo hapooo....

Taharuki ingine iliyonisababisha nizidi kuweka mbali siasa na moyo wangu ni siku ile Jiwe anatangazwa kuwa ndo Raisi..... jiji la Dar lilipoa utasema kulitangazwa msiba kila kaya hakukuwa an shamra shamra kuwa Jiwe katangazwa..... ile sadness mie ndo sitaki inikumbe ila kuna mahali najikuta tuu mambo nayafahamu na yananiumiza kichwa aaghh.

Kuhusu makala nasoma sanaa hata iwe ndefu kama reli mradi iwe na mtiririko na kuvutia kuendelea kusoma maana hata mie huwa naandika kinachonijia kichwani nisipoamua kuweka nukta naweza andika page hata tatu.
 
Nikiacha mimi atakuambia nani...? Mtaje kama yupo niitoe roho yake kwa jisu lenye makali kuwili..

Makeke nimerithi kwa babu! Tena alinifundisha na maneno matamu nikiyamwaga hapa kihoro kitakutoka bure!
Mi ntakapokukuta salamu yangu kwako busu bunifu,busu lenye husuda na kiherehere cha mahaba! Busu ambalo ni ama ukae au unyong'onyee kwa utamu wake!!
Mi ndio ile shekeli itafutwayo,shekeli iliyoshiba madini inayopendwa na vigoli bikira.. Kama uliwahi sikia ule usemi usemao usiache mbachao kwa msala upitao basi mimi ndimi hiyo mbachao!!
Mimi ndio reli yako ikitoka treni hutoenda kokote..
Nivike kidani chako cha huba nikupe utamu wako mahabuba😉

Aahahahahaa Kenzy banaa, maneno haya ulipaswa uniambie huku wamparua samaki kisha wamchoma taratiibu akiwiva wamkatia kachumberi halafu usikaribish nile, nikishiba nawezajikuta nimelainika na nyimbo zako maana looh ahhahahaaa

Ila naomba uniunganishe na babu yako kwanza nisemeshane nae halafu ndo tusemeshane nawe.
 
Back
Top Bottom