Nimeridhishwa na mchakato wa ajira za elimu na Afya

Madibira 1

JF-Expert Member
Jan 6, 2023
340
734
Poleni na majukumu,
Hongereni Kwa kuipigania bandari,
Pongezi Kwa watafuta ajira wote Kwa kutokukata tamaa.

Moja Kwa Moja kwenye mada. Mimi ni msaka ajira ambae nilipanga kupambania nafasi ya ualimu mpaka niipate. Bahati mbaya nimekosa Kama siku zote ambazo nimekua nikikosa. Ingawa nimekosa Sina kinyongo na serikali na waendesha mchakato kutokana na Mambo yafuatayo;

1: Kuajiriwa Kwa wakongwe zaidi yangu.
Katika mchakato huu ni kili kuwa marafiki zangu wengi na ndugu ambao wamehitimu vyuo vikuu na vyuo vya ualimu ngazi ya cheti wameajiriwa. Hawa wengi walimaliza mwaka 2015 na 2016 tofauti na Mimi wa 2017, hivyo naamini next time Mimi wa 2017 nitakua kipaumbele.

2: Kuajiriwa Kwa walimu waliokuwa wakijitolea Kwa muda mrefu.
Ingawa serikali haikuwa na data za watu wanaojitolea na maeneo lakini katika eneo ninalotoka, waliokuwa wakijitolea kwa shule za msingi wote wamepata ajira na Kwa upande wa serikali wanne kati ya kumi wameajiriwa. Hivyo naamini kuwa serikali ni sikivu na binafsi nimefurahi maana nimepata kwakugongea vocha. Pia Kuna dada ambae tumesoma nae O-level nae kapata za Afya

3: Kuajiriwa Kwa walimu wa kiingereza kwanza Kwa walimu ngazi ya shahada. Hili kwenye tangazo lilionekana lakini naamini pia wale wa history, kiswahili, geography, bios, chemistry n.k nasi tunafikiriwa huenda next time ikawa zamu yetu.

Hivyo basi mama aendelee kupiga mwingi mpaka umwagike. Nina Imani na Mheshimiwa Rais, Nina Imani na serikali ya Chama Cha mapinduzi, Nina Imani na TAMISEMI na naamini ipo siku Mungu atatenda.

Jamani Kwa mwenye koneksheni ya shule pia mniunganishe, ninauzoefu wa miaka miwili kufundisha shule za msingi masomo yote, na Nina mwaka mmoja wa kufundisha sekondari masomo ya history, kiswahili na civics. Ngazi zote nilifundisha na ninafundisha Kwa kujitolea.
 
Sema upande wa ualimu na sio afya, afya clinical officers walioajiriwa karibu wote ni wa 2019 na 2020 tu wa miaka ya nyuma wote wameachwa.
 
Back
Top Bottom