Nimeridhika na binti nataka nimvishe pete

Too bad Lizzy!Mapenzi hayana alama,pia pete sio alama ya mapenzi,ngoja nikufafanulie kidogo,angalia post inayofuata!

Kwako wewe SIO kwa wengine NDIO.
Kila mtu anafanya kitu kuendana matakwa pia mapenzi yake. Sio wewe wala mimi mwenye haki ya kumwambia sababu inayomsukuma kufanya anachotaka kufanya SIO kwasababu tu wewe au mimi siamini hivyo.

Kwahiyo wewe mpe ushauri wa wapi akanunue pete na vipi ampe mwenzake badala ya kupinga kitu kisichohitaji upinzani.
 
Lizzy,si muamulii cha kufanya huyu mtu,ninachotaka ajue ni kama anafanya kitu anachokijua ama la,HAKUNA alama ya mapenzi huu ni ukweli haijalishi nani ana mtazamo au maoni gani!WEWE pamoja na mimi tuliamini hivyo,kwamba pete ni alama ya upendo,hatukuwahi kuhoji KIVIPI,ungejiuliza wala usingesema ulichosema!HIVI hisia ina alama kweli?
 
nyie vijana nyie,
akili mbovu sana.
 
AGAIN. . . .. UKWELI WAKO sio UKWELI WA WATU WENGINE.Usilazimishe watu wengine kuwa na mawazo kama yako. Toa mawazo yako umpe mtu nafasi ya kujiamulia mwenyewe na sio kukomaa kwamba unachojua wewe ndio ukweli pekee uliopo. Ukweli unatofautiana kati ya watu na watu kutokana na mazingira, malezi na uelewa binafsi. . . kumbuka hivyo kila wakati ukiwa unajaribu kupinga kike anachofanya/amini mtu mwingine.
 

Duuh; kama annual income yako ni 36m then pete ni 4.5m du, ni kavitz!
 
Mpeleke kwa mama ntilie halaf agiza ugali harage mbili kubwa, maliza mchezo na ka pete kako ka buku tano. Ukikaona kamechukia hiyo situation kapige kibuti hapo hapo njoo JF anzisha sredi ya kutafta mchumba mwengine.

Analysis:
Kama kamechukia hali ya kimaskini ya hapo kwa mama ntilie basi ujue huko mbele ya safari mzembe ukifulia basi kadada kanakutema. (hapa greti thinka nimeona beyond greti thinking capacity)

Nipongezeni
 
hizi pete za kuvalishana uchochoroni, au niseme za suprise bila kuwashirikisha wazazi mara nyingi huwa hazina mashiko. Nafikiri ingekuwa vyema ukajipanga ukaenda kujitambulisha kwao ikifuatiwa na kumvalisha hiyo pete. pete nzuri zinapatikana Mitaa ya Indra Gandhi karibu na maeneo ya Clock tower.
 
Nenda mitaa ya Indira Gandhi Sonara ya Kasmani.. Ila ongeza kidogo fungu. Lakini pia ujue size ya kidole chake, usije ukakosea size
 
Lizzy,sijui hutaki kuelewa au ni kweli huelewi!Narudia tena,UKWELI NI UKWELI haujalishi nani anaelewa nini kuhusu huo ukweli,huwezi ukasema eti ukweli wangu ni tofauti na ukweli wa mtu mwingine,hakujawahi kuwa na ukweli wa aina mbili ukweli ni mmoja tu!Kati yangu mimi na wewe tunapozungumza mambo yanayokinzana hatuwezi kuwa wote wakweli,mmoja LAZIMA atakua sio mkweli,ili aonekane mimi na wewe nani mkweli tuelelezane tunachojua kuhusu pete halafu tutaona ni nani anafuata jambo bila kujiuliza.Huwezi ukasema jua linazunguka dunia halafu ukadai huo eti ni ukweli wako!Simlazimishi huyu jamaa aamini ninachozungumza yeye mwenyewe ataamua aidha aendelee kufanya mambo kwa mazoea au aanze kujiuliza maana halisi ya pete!
 

Sidhani kama naweza kuendelea kubishana na wewe. Subiri nikimaliza kuandika pepa yangu ya ToK labda ntakutumia kopi.Kwa kumalizia narudia kusema kwamba UKWELI wako sio lazima uwe WANGU.

So long!
 
Ok Lizzy inasikitisha sana unapoamua kubisha badala ya kujifunza,unazungumza zaidi ubishi badala ya kutoa maelezo ya kutetea unachoamini,bahati mbaya huwa sipendi ubishi coz ubishi hauna maana yoyote zaidi ya kupoteza muda,unaweza kuchagua kukaa ndani ya kiberiti na ukaamua kuamini nje ya hapo hakuna maisha na ukaamini hivyo na huo ukawa "ukweli" wako!Nashangaa hukujibu nilipokuuliza kama hisia zina alama!!!!Kitu kingine ni kuwa sijui kama unajua historia ya alama!An way uchaguzi wako ndo utakufanya uwe wa namna gani!
 

..yaani ikemewe.
 

Mhhh mi siamini nguvu za giza
 
Duh ntankosa malaika wangu kwa mambo ya kupima maji teteteeee
 
Kwani ni lazima kuendelea na majadiliano na wewe?Nimechagua kutokufanya hivyo kwa sababu ni upotevu wa muda so just let it be ehhh.
 
.......Umeshatoa posa? Mahari je? Raha ya pete uvishwe siku ya kutoa mahari..........mbele ya wazazi na ndugu. Sasa sijui utaratibu wa kwao huyo dada, ila ingekuwa vizuri kufanya utaratibu na makubaliano ya ndoa ili pete mvishane kiheshima.
hii safi sana,niliitumia pia!hayo mambo ya kizungu tuyaache jamani
 
Good comment Lizzy.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…