Nimepoteza ufunguo wa gari

Nimepoteza ufunguo wa gari

JF Member

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
8,204
Reaction score
11,364
Wakuu nimepoteza ufunguo wa gari. Toyota.

Nifanyeje?
Sina spare.
 
Uko wapi nije kukufungulia? Ni waya tu inatowa lock ila nikikuwashia gari kuitowa hapo ilipo itabidi uipaki nyumbani ununuwe ignition switch nyingine.
Iko nyumbani tayari. Shida ufunguo siuoni Siku ya tatu sasa.

Asante kwa ushauri pia
 
Iko nyumbani tayari. Shida ufunguo siuoni Siku ya tatu sasa.

Asante kwa ushauri pia
Jitahidi upate upenye kwenye kioo cha mlango, unaweza kutoa raba/mpira unaozunguka kioo then ingiza waya ili ufyatue lock.
Utafungua bila shida, imenitokea mara mbili kufungia ufunguo na niliweza kufanya hivyo
 
Inategemea na gari/model/mwaka.
Kama ni model ya zamani zaidi unaweza ukachongewa kama ni model mpya funguo zina chip ndani funguo hizi za kuchonga kawaida hazistart gari, funguo inabidi ifanyiwe programming na nadhani kwa kuwa ushapoteza inakuwa kasheshe, waone Manji Keys kisutu mtaa wa Zanaki.
Manji Key Master
 
Jitahidi upate upenye kwenye kioo cha mlango, unaweza kutoa raba/mpira unaozunguka kioo then ingiza waya ili ufyatue lock.
Utafungua bila shida, imenitokea mara mbili kufungia ufunguo na niliweza kufanya hivyo
Si rahisi kihivyo kama unavyotaka kumuaminisha.
 
Iko nyumbani tayari. Shida ufunguo siuoni Siku ya tatu sasa.

Asante kwa ushauri pia
Home mitaa gani? Kama funguo imepotea jipange ununue ignition switch mpya ufunguliwe mlango ibadirishwe tu, kama gari ipo nyumbani mbona poa tu.
 
Back
Top Bottom