Nimepoteza Muda tu Form 5

Nimepoteza Muda tu Form 5

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Posts
2,649
Reaction score
4,756
Jamani nashauri kama kuna mtu yeyote ana ndugu yake amemaliza form 4 mwaka jana...asijisumbue kumtafutia shule eti kusoma advance(form 5 na 6)...hiyo level ni ya matesobna kupoteza muda tu...

Cheti cha form 6 hakina kazi popote zaidi ya kuombea chuo tu degree...yaani hiyo ni hata ukifaulu...ukikosa mkopo basi na elimu yako mpaka form 6 huwezi enda kampuni yoyote ukaomba kazi ukapewa...

Lakini aliyemaliza form akaunga college yoyote inayotambulika kwa ubora akajiunga akasoma zake miaka 3(ambayo imeongezeka just miez kadhaa tu ya ule muda unaopoteza form 5 na 6)...akitoka anakuwa na cheti ambacho kina umuhimu popote...kwanza anapata ujuzi...pili anaajiriwa popote na anasikilizwa ukilinganishwa na aliyesoma form 6...tatu kupitia cheti hicho hicho cha DIPLOMA anaombea nafasi za DEGREE bila shida yoyote kama aliyemaliza form 6...

Yaani alisoma mpaka advance...akizingua chuoni...basi ndo hana namna...

Ila aliyesoma diploma...akizingua chuoni degree basi anaweza kutumia cheti chake cha diploma kusurvive mjini...

KWANZA UKUBALI UKATAE...MWENYE ELIMU YA DIPLOMA NDIYE ANAYEPATA AJIRA KWA WINGI NA HARAKA ZAIDI KULIKO MWENYE DEGREE...KWA SABABU...

1. Wenye degree maofisini ni Ma Attendants... Wenyewe ndio wafanyaji kazi...ukilinganisha na MABACHELOR HOLDERS ambao ni MaDecision Makers...
Sasa huwezi kuwa na madecision makers wengi na watendaji ni wachache...

2. Maboss wanawapenda madiploma hawasumbui mishahara na kujiona classic alafu ni wachapakazi...alafu ndio wengi...ila mabachelor holders ni WASUMBUFU..

NIMEJIONEA...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu ya msingi+o level ilishindwa kuupa ubongo wako uwezo wa kuchanganua faida na hasara za kusoma A LEVEL ndipo ufanye maamuzi, matokeo yake ndio haya majuto unayoyajutia leo. Adui wako ni akili yako mwenyewe
 
Cheti cha form 6 hakina kazi popote zaidi ya kuombea chuo tu degree...yaani hiyo ni hata ukifaulu...ukikosa mkopo basi na elimu yako mpaka form 6 huwezi enda kampuni yoyote ukaomba kazi ukapewa...
Mkuu hiyo ndiyo kazi ya cheti cha form 6, sasa sioni tatizo liko wapi. Hii ndiyo njia kuu kwa wanaolenga kusoma degree Tanzania ndio maana ukichambua vitabu vya TCU Admission Guidelines utaona zaidi ya 90% ya nafasi za vyuo vikuu hujazwa na watu wenye advance.
Wengi wanaokwenda certificate na diploma ni kwa sababu ya ufaulu mdogo ingawapo wapo wenye ufaulu mzuri walio amua kupitia njia hiyo. Kwa hiyo Advance haiko kwa kila aliyemaliza F4.
Na kuna degree programu ambazo wale ambao hawakupitia advance msala unakuwa mkubwa sana-wenyewe wana sema una struggle kwa hali ya juu ukilinganisha na walio pitia Advance hivyo tuwe makini katika kuchagua njia ya kupita.

Kila mhitimu wa F4 anatakiwa ajitathmini ni njia ipi inamfaa kutokana na mazingira yake na kile anachotafuta. Zote/diploma na Advance zinaweza kuwa njia sahihi.

KWANZA UKUBALI UKATAE...MWENYE ELIMU YA DIPLOMA NDIYE ANAYEPATA AJIRA KWA WINGI NA HARAKA ZAIDI KULIKO MWENYE DEGREE...KWA SABABU...

1. Wenye degree maofisini ni Ma Attendants... Wenyewe ndio wafanyaji kazi...ukilinganisha na MABACHELOR HOLDERS ambao ni MaDecision Makers...
Sasa huwezi kuwa na madecision makers wengi na watendaji ni wachache...

2. Maboss wanawapenda madiploma hawasumbui mishahara na kujiona classic alafu ni wachapakazi...alafu ndio wengi...ila mabachelor holders ni WASUMBUFU..

NIMEJIONEA...

Hapa naona unachapia, kwenye nyekundu hueleweki kabisa (wenye degree na mabachelor holders).
 
Jamaa Kajenga Hoja Zimesimama, Lakini Watu Wanamtusi Bila Hoja,,, Jengeni Hoja
Nina imani nimejenga hoja kwenye kutoa msimamo wangu na hakuna tusi ndani ya kile nilicho kiandika. Lakini ni kweli ingawapo sikubaliani na hoja kuu anayojenga mleta uzi hakuna sababu ya kumtusi yeye binafsi badala ya kujadili hoja zake.
Alichosema mtoa mada kina mantiki kubwa sana japo kuna manunda yamekuja speed kumtusi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nawe unatukana kama hao wengine.
 
hoja zake mbona zimenyooka? ushawai kuona matangazo mangapi ya ajira kigezo wanahitaji form 6 holder?

na pia umewahi kuona matangazo mangapi ya ajira ambapo kigezo wanahitaji diploma holder ?
Piga shule bwana mdogo! Utaaibika mjini hapa na elimu yako ya kubangaiza!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana kuliko piriton!!
Watu mliofeli kidato cha NNE mnashida sana kisaikolojia....wengi wenu ni vichaa kabisa ila hamjathibitishwa tu na daktari.
Wenye elimu ya kuungaunga wana inferiority complex

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndo unamatatizo ya kisaikolojia, na unadhani kwa vile ulifaulu kidato cha nne unahaki ya "kujudge" wengi kumbe ndo jinga kabisa, jifunze kuheshimu mawazo ya watu wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Wenye degree maofisini ni Ma Attendants... Wenyewe ndio wafanyaji kazi...ukilinganisha na MABACHELOR HOLDERS ambao ni MaDecision Makers...
Sasa huwezi kuwa na madecision makers wengi na watendaji ni wachache...
Jamii Forums mobile app
Hapa kuna walakin, bachelor holder ni yupi na mwenye degree ni yupi?
 
hoja zake mbona zimenyooka? ushawai kuona matangazo mangapi ya ajira kigezo wanahitaji form 6 holder?

na pia umewahi kuona matangazo mangapi ya ajira ambapo kigezo wanahitaji diploma holder ?
Waambie na uform 6 wako kwa mfano ukadisco chuo...nan atakupokea...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom